Wajuzi wa mambo ya ujenzi

Mkuu tunaomba ufafanuzi kidogo hapa, Hiyo laki 8 anasuka msingi mpaka kufikia hatua gani? Labda ni kwenye lenta, nk..tunaomba ufafanuzi
 
Nimekuelewa sana sana mkuu, ubarikiwe sana
 
Kwenye msingi Kuna lenta(lintel)?? Alfu hiyo prince beam ndio nini wewe??
Hivi kwa nini watu mnajifanya wataalamu kwenye kila kitu hata Kama hamjui??
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Pole sana, juu ya msingi huwa tunamimina lenta/ beam tena tunasuka nondo 4, kreki utaisikia kwa jirani.
Kwa ujenzi ni nyumbani kwangu nimesomea nasio kanjanja kama wewe.
Nina vyeti na uzoefu sio wa nchi hii.
Ukitaka kuhakikisha njoo unitembelee kwenye miradi yangu.
Iwe Dar, Arusha, Tanga na Kilimanjaro.
Ninaongea nikijuacho sipigi ramli ewe kenge mwenzangu[emoji28]
 
Ukipita mtaani utaona nyumba inang'a baada yamwaka nyufa kibao ukweli ndohuo nyumba nyingi nimbovu lakini kwakuwa wenye nyumba wengi niwasomi nawanajua watayaona mbele
Kweli kabisa
 
Hivi labour charge inapatikana vp!? Si unaangalia kwanza gharama za material alafu mnapigia asilimia tatu ya gharama za material!?
Kwa msingi ni ngumu kupata gharama za fundi kwa kutumia asilimia kwasababu zifuatazo;
1. Kupima msingi hakuna manunuzi
2. Kuchimba msingi hakuna manunuzi.

Katika msingi fundi akupe mchanganuo kama ifuatavyo;
1. Kuchimba msingi/mita bei gani na jumla yake
2. Kumwaga ka zege cha chini sh ngapi/mita
3. Tofali bei gani kuzijenga
4. Nguzo za baraza
5. Kujaza udongo na kushindilia
6. Kupanga maww kwa floor kama atatumia bei yake pia
7. Atamimina floor/ jamvi kwa bei gani.

Ukitumia vigezo hivi utajua wapi umwpigwa au umefanyiwa bei nzuri
 
Hahaha
Hajui kuwa sio lazima ujengee mawe pia.
Watu wanakariri tu hawajui hizi ni fani za watu
Usiwe kama robot mzee mawe nimetaja tu na sijamlazimisha atumie cha muhimu ni material ya msingi lazima yawepo katika ujenzi
 
Uko sahihi umeenda mbali mm ni lasaba mkuu .swala laelim linaingiaje mkuu lakini ninahakika kuna watu humu wanaelimu pengine zaidi yako wanasoma kwashida mwisho wanaelewa kusudio langu
Hata Kama ni la Saba, jitahidi Kuandika vizuri. Mbona Mimi nilipomaliza la Saba nilikuwa naandika vizuri tu?
 
Mkuu tunaomba ufafanuzi kidogo hapa, Hiyo laki 8 anasuka msingi mpaka kufikia hatua gani? Labda ni kwenye lenta, nk..tunaomba ufafanuzi
Lenta ya wapi Tena wewe? Kusoma hujui? Nazungumzia msingi tu
 
Ungesomea usingesema kwenye msingi Kuna lenta, hivi unaelewa maana ya lenta/lintel??
HAKUNA kitu nachochukia Kama Mtu kujifanya anajua kwenye Jambo ambalo halijui.
Kasome Tena lenta/lintel ni nini alafu njoo hapa
 
Huyo mtupe fundi haizidi laki tano (500,000/)
Au nunua material then ita day workers hiyo utaelewana nao kila siku fundi 20,000/ tu utajenga siku mbili tu au uza tofali hapo boss kila tofali sh250 au Mia tatu tu (300) hapo anajenga tofali nyingi ndio anatoka na mkwanja
 
Ungesomea usingesema kwenye msingi Kuna lenta, hivi unaelewa maana ya lenta/lintel??
HAKUNA kitu nachochukia Kama Mtu kujifanya anajua kwenye Jambo ambalo halijui.
Kasome Tena lenta/lintel ni nini alafu njoo hapa
Hivi lenta ni nini?
Hii ni beam kwa kiingereza.
Beam ya juu ya msingi inaitwaje?
Ungewezaje kumweleza mtu ambaye hajui maana ya beam badala ya kutamka kwa lugha aliyozoea, unaujuaji wa kiduwanzi isijifanye mwelewa.
 
Hata Kama ni la Saba, jitahidi Kuandika vizuri. Mbona Mimi nilipomaliza la Saba nilikuwa naandika vizuri tu?
Ili usipate tabu sehemu nilipoandika mimi usisome, humu tunapita ili tujifunze tusivyovijua halafu unataka kusema watu wote wanaopita humu huwajui makosa yangu ya uandishi,jifunze kupuuza mkuu.
 
Kwenye msingi Kuna lenta(lintel)?? Alfu hiyo prince beam ndio nini wewe??
Hivi kwa nini watu mnajifanya wataalamu kwenye kila kitu hata Kama hamjui??
Hii kila mtu kijifanya mjuaji mwalimu wao jiwe
 
uwiano wa 1:6 ni sawa na mfuko mmoja wa cementi kwa ndoo ndogo ngapi za mchanga? pia kwa uwiano wa 1:8 na 1:4 naomba msaada kwa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…