Wajuzi wa masuala ya ujenzi naombeni ushauri wenu

Wajuzi wa masuala ya ujenzi naombeni ushauri wenu

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Wakubwa shikamooni, madogo mambo vipi, poleni wote na makali ya tozo. Mimi ni kijana wa kiume miaka 30 makazi yangu kwa sasa yapo Iringa

Twende moja kwa moja kwenye point., katika kuchanganyika vizuri na watu kuna jamaa kanisaidia kunipa msaada wa molds za kutengeneza maua na mikanda ya gypsum, nimesaidiwa pia eneo la kazi, sehemu ya kuifadhi bidhaa na mifuko kadhaa ya gypsum powder, nimefanikiwa kukopa mbao na miti kwa ajiri ya kutengeneza majukwaa kwa makubaliano ya kulipa hapo mbeleni biashara ikianza kusimama kuna mtu nilimfanyia kazi akakubali kunidhamini kwa mali kauli tu..

Changamoto pekee niliyobakiwa nayo ni kuleta mifuko ya unga na baadhi ya molds huku Iringa kutokea dar na kulipa vijana wa kazi na huduma ya maji kwa ajiri ya shughuli nzima, hali ni ngumu kwa kweli ila napambana angalao ifikapo september nianze uzalishaji

Sasa ninachoomba ni ushauri kwa wajuzi wa mambo ya ujenzi na hardware.. namna ya kuwavutia wateja, ubunifu, njia kuongeza mauzo na faida na suala zima la usimamizi, mambo yakienda vizuri niongeze nini n.k..

Naombeni ushauri na mchango wa mawazo yenu wakuu
 
Back
Top Bottom