Hallo AD.Hujambo mami wangu? Nafurahi kukuona tena hapa MMU baada ya kusoma thread moja kwamba ulikutana na Ban Ki Moon. Kama ni kweli pole sana na karibu 'home' yetu ya JF.Turudi kwenye thread yako.
Saikolojia ya wanaume inatofautiana sana na ile ya wanawake.Mtazamo, mwelekeo na mawazo ya mwanaume ni je, napambana na maisha ipasavyo? Ni wapi kuna deal safi zaidi kuliko hili la sasa? Mawazo haya yanamzamisha kwenye dunia yake peke yake na ni vigumu kwake kutoka huko na kuzingatia jambo tofauti. Mwanamke yeye mawazo yake ni kutunza, kupendezesha na kuratibu. Ndo maana ni rahisi sana kwa mwanamke kukumbuka sikukuu ipi inakuja tarehe ipi na kama amejiandaa ipasavyo: mavazi, mlo nk. Wanaume wengi hawapo kabisa kwenye hii dunia ya ceremonies/festivals. Kwa hiyo AD usiwashangae sana wakaka na wababa kwa kushindwa kwenda sambamba na mabirthday nk. Halafu kumbuka tunaishi Tanzania ya mwaka 2012 ambayo sh 10,000 huwezi kwenda nayo sokoni kariakoo kutafuta mahitaji ya mlo wa jioni na kutoka ukiwa na furaha! Wanaume wana msongo wa mawazo, na mapressure makali.Hiyo birthday yako itakaa kwenye kichwa kipi? Hapa nazungumzia kwa ujumla tu jinsi hali ilivyo.Wengine hata ukimkumbusha inakuwa ugomvi.
Kwa hiyo AD ni vitu viwili ndivyo vinawakorofisha akina kaka na wababa: jinsi walivyoumbwa na hali mbaya ya uchumi.
Birthday yako lini nikutumie mkungu wa ndizi toka Moshi.