Wakala kuomba simu yako kuhakiki

Wakala kuomba simu yako kuhakiki

Joined
Jun 16, 2024
Posts
45
Reaction score
56
Hivi ni sahihi kwa wakala kuomba simu yako ya mkononi kuangalia sms ya muamala kama imeingia? Binafsi mimi naona ni kuvunja privacy au taarifa za siri za mtu kwani sms ya muamala inaonyesha kiasi kilichobaki kwenye account ya mteja.
1: mteja alietoa hela na kubakiza kiasi kikubwa sana kwenye simu yake inaweza kuhatarisha maisha au usalama wa mtu huyo
2: mteja aliyebakiza kiasi kidogo sana kwenye simu yake mfano katoa Tsh2000=/ kabakiza Tsh 5 inaweza kupelekea kudharauliwa na kusemwa kwa wahudumu au mawakala wasiotambua umuhimu wa kuficha taarifa binafsi za mteja. Mimi pia ni mmoja kati ya watu ambao huwa tunakosa raha kabisa pale wakala anapoomba simu yako ajiridhishe kuangalia sms ya uthibitisho.

1:Swali langu ni sahihi wakala kuomba simu ya mteja?
2:utaratibu ni upi?
 
Mimi nipo pamoja na wewe kuwa huu si uungwana. Ila nafikiri Kuna mazingira yanawalazimu watoa huduma kufanya hivyo, ikiwemo kutoa pesa na ujumbe usimfikie mtoa huduma kwa wakati Kutokana na tatizo la kimtandao. Kwa case kama hiyo itabidi mtoa huduma ahitaji simu ya mteja ili kuokoa muda wa mteja.
 
Hivi ni sahihi kwa wakala kuomba simu yako ya mkononi kuangalia sms ya muamala kama imeingia? Binafsi mimi naona ni kuvunja privacy au taarifa za siri za mtu kwani sms ya muamala inaonyesha kiasi kilichobaki kwenye account ya mteja.
1: mteja alietoa hela na kubakiza kiasi kikubwa sana kwenye simu yake inaweza kuhatarisha maisha au usalama wa mtu huyo
2: mteja aliyebakiza kiasi kidogo sana kwenye simu yake mfano katoa Tsh2000=/ kabakiza Tsh 5 inaweza kupelekea kudharauliwa na kusemwa kwa wahudumu au mawakala wasiotambua umuhimu wa kuficha taarifa binafsi za mteja. Mimi pia ni mmoja kati ya watu ambao huwa tunakosa raha kabisa pale wakala anapoomba simu yako ajiridhishe kuangalia sms ya uthibitisho.

1:Swali langu ni sahihi wakala kuomba simu ya mteja?
2:utaratibu ni upi?
Msg ya muamala inaweza kuwa haijafika kwake. Kuokoa muda anaangalia kwako kama msg inaonesha anakupa hela yako. Unaweza kuamua usimpe ukasubiri hadi msg imfikie,uamuzi ni wako.
 
Lakini sisi baadhi ya watanzania huwa tunarahisisha sana mambo kama haya na ndo maana tunaingiaga kwenye matatizo bila kujua kama vile kutapeliwa, kutekwa, na wakati mwingine kuuawa sidhan kama nchi nyingine wanafanya hivi at least kuwe na utaratibu wa mteja kumpa wakala namba za msimbo ( mfano WYWVSY99) Halaf mtoa huduma awe na mfumo maalumu wakuhakiki kama msimbo huo ni valid au sio valid kuliko kumpa mtu simu yako. Ikumbukwe hyo ni simu ya mkononi simu binafsi
 
Kama huna haraka unaweza kusubiri hadi meseji ifike kwake. Kumpa simu yako si sahihi kabisa ila itategemea na mazingira ya tukio lenyewe.
 
Hiyo ishu huwa ni kama wakala hajapata sms ya uthibitisho kua umetoa pesa.
Na anaomba kuthibitisha kupitia simu yako huku yeye akiendelea kusubiri sms ifike kwake.

Unaweza kukataa kumpa simu na ukakaa kusubiri sms imfikie yeye.

Sidhani kama huwa wanalazimisha, kama anakulazimisha umpe aone sms huyo atakua sio mstaarabu na anakiuka sheria na taratibu za uwakala.
 
Lakini sisi baadhi ya watanzania huwa tunarahisisha sana mambo kama haya na ndo maana tunaingiaga kwenye matatizo bila kujua kama vile kutapeliwa, kutekwa, na wakati mwingine kuuawa sidhan kama nchi nyingine wanafanya hivi at least kuwe na utaratibu wa mteja kumpa wakala namba za msimbo ( mfano WYWVSY99) Halaf mtoa huduma awe na mfumo maalumu wakuhakiki kama msimbo huo ni valid au sio valid kuliko kumpa mtu simu yako. Ikumbukwe hyo ni simu ya mkononi simu binafsi
Uko sahihi kabisa, na kama ni hivyo kwa ajili ya usalama basi huna budi kusubiri mpaka ujumbe utakapofika kwa mtoa huduma.
 
Mtandao kusumbua kupo ila mpaka kufikia wakala kutaka simu yangu ajisomee hiyo haipo na siwezi kuruhusu,
kila leo mnatangaziwa matangazo ya kuepuka matapeli kumbe huwa mnajipelekaga wenyeww kwenye mikono ya matapeli
Hujajibu swali langu lkn.
 
endapo ni ishu ya mtandao na msg ya uthibitisho kwake hajaipata basi muhimu
ni kutaja kiasi ulichotoa halafu yeye wakala ndio atizame kwenye simu yake kama
salio limeongezeka kwa hesabu hizo.
 
Yani mie nipate sms halafu wakala asiipate, mawakala wenyewe sio wa kuwaamini eti umpe simu yako watz tunachukuliaga vitu kirahisi sana, yeye wakala hata kusimama kwenye eneo lake bila kuwa na cha kufanya anakuitia mwizi, yeye mwenyewe hawezi kamwe kukupa simu yake ili uhakiki sms
Hujajibu swali langu lkn.
Nimekujibu sijawahi kukutana na tukio la namna hiyo, na likinikuta kuna namba zinazofuata baada ya imethibitishwa nitamtajia hizo
 
Mtandao kusumbua kupo ila mpaka kufikia wakala kutaka simu yangu ajisomee hiyo haipo na siwezi kuruhusu,
kila leo mnatangaziwa matangazo ya kuepuka matapeli kumbe huwa mnajipelekaga wenyeww kwenye mikono ya matapeli
Mm nina kiofisi cha tigopesa.
Kuna wakati nikiwa free naenda nasaidiana na kijana.
Kuna mteja anatoa hela sms ya muamala haimfikii wakala.
Kwa mazingira haya nini kifanyike?
 
Hiyo ishu huwa ni kama wakala hajapata sms ya uthibitisho kua umetoa pesa.
Na anaomba kuthibitisha kupitia simu yako huku yeye akiendelea kusubiri sms ifike kwake.

Unaweza kukataa kumpa simu na ukakaa kusubiri sms imfikie yeye.

Sidhani kama huwa wanalazimisha, kama anakulazimisha umpe aone sms huyo atakua sio mstaarabu na anakiuka sheria na taratibu za uwakala.
Ndivyo navyojua mie.
 
Back
Top Bottom