Wakala kuomba simu yako kuhakiki

Wakala kuomba simu yako kuhakiki

Huo utaratibu hakuna. Ila je, unaelewa taratibu sahihi kabisq za miamala ya simu inavyopaswa kuwa?

Wakati inaanza, M-PESA walikuwa na kitabu cha logbook. Mteja akitoa fedha, anajaza taarifa zake muhimu ikiwemo namba ya muamala, kiasi, kitambulisho chake, sahihi,nk.

Hii yote iliweka ili kuepusha usumbufu mwingi. Wizi vile vile.

Sasa siku hizi kuna wimbi kubwa sana la kurudisha miamala. Mteja anaenda kwa wakala. Anaomba kutoa fedha, anapewa go ahead.

Anachofanya, anamtumia mwenzake namba ya kutolea. Anapewa hela na kuondoka. Kisha akishaondoka mahali hapo, anawasiliana na mwenzake simu inapigwa huduma kwa wateja kuzuia muamala..

Wanachoangalia mtandaoni, kwanza wanaushililia huo muamala immediately. Kisha watapiga simu kwa wakala kujiridhisha. Wakala ukisema umetoa hela, wanawaunganisha na mteja. Mzungumze.

Mteja anakataa, wakala naye anabisha. Sasa wanarudi kwenye location. Mteja katoa fedha yupo Narung'ombe huko. Wewe wakala upo Dar. Wapi na wapi?

Ukijitetea pengine alitoa namba kwa nduguye, basi unakosa. Umejaza logbook? Jibu hapana.

Mteja anarudishiwa fedh zake na wakala kula hasara .

Mantiki ya kuona sms ni kujiridhisha tu. Sidhani kama kumuonyesha sms chap bila kumkabidhi simu yako, ukaamua kuziba salio kwa kidole ni jambo gumu.

Si haki, lakini wana sababu yenye mashiko kidogo. Vinginevyo tuwe tunajaza vitabu vya miamala.
 
Ishu ya sms sidhani kama ina mashiko.

Wakala HARUHUSIWI kwa namna yeyote kumpa mteja hela kwa kuwa eti yeye kapata sms, huku wakala bado.

Wanaofanya hivyo wanafanya tu kuwasaidia. Ila wanakosea.
 
Wakala huwa anajiridhisha tu haraka pale ambapo mteja amepata sms halafu yeye hajapata.
Ili kurahisisha mambo inabidi aangalie sms kwako.
Mbona kuna muda unatoa pesa hupati sms kwa wakati lakini wakala anapata! Ni mtandao tu.

Kwanza akikuomba simu ili ajiridhishe kwa sababu hajapata sms halafu wewe ukakataa ombea tu liwe ni eneo la kwenu ambako unafahamika, vinginevyo utaonekana una tatizo hata mbele ya wateja wengine.

Ukiona huwezi kumpa simu kwa ajili ya privacy subiri mpaka pale na yeye atakapopata sms maana ndio uthibitisho sahihi sio uanze kumpangia eti aangalie salio kwake kama limeongezeka. Hayo ni mahesabu ya jioni.
 
Sasa mnaogopa nini?, au umetoa ten ( 10,000), anaona sms pale salio lako ni buku jero?...
 
Back
Top Bottom