Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Katibu wa CHADEMA kata ya Tabata, Jacob Emily inadaiwa ameumizwa alipokua akiyazuia majina yaliyoletwa na watu wa CCM yasiingizwe kwenye daftari la uandikishaji wapiga kura. Watu wa CCM inadaiwa wakamvamia na kumjeruhi.
Inasemekena Polisi - Tabata walikuwapo karibu kabisa, Wametulia tu.
Jacob Roman Emily ni Katibu Kata wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) @ChademaTz
kwa Kata ya Tabata amejeruhiwa kwa viwembe na kundi la vijana wakati alipokuwa akienda kutoa taarifa juu ya uwepo wa watu wanaoandikisha wananchi kinyume na utaratibu.
Emily anaeleza kuwa alikuwa kwenye majukumu yake ya kupitia kwenye vituo vilivyopo katika kata hiyo ili kuona utekelezaji wa majukumu wa mawakala wa chama chake na alipofika kituo cha kujiandikishia kilichopo Tabata Shule nje ya kituo akakuta kundi la watu ambao amedai ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM) @ccm_tanzania
wakiandikisha wananchi ambao tayari wameshajiandikisha kituoni hapo.
Baada ya kuhoji juu ya uandikishaji huo aliondoka ili kwenda kushtaki kwa mamlaka husika ambayo ni Mtendaji wa Mtaa huo, akiwa njiani ndipo vijana hao wakaja kumshambulia na mmoja akamjeruhi kwa kumchana na kiwembe eneo la shavu la kulia.
Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA jimbo la Segerea Shadya Abubakari ameeleza kuwa wameripoti tukio hilo kwa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Upelelezi kutoka Kituo cha Polisi Buguruni alifika eneo la tukio huku hatua zikichukuliwa ikiwemo kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja.
PIA SOMA
- LGE2024 - Dar es Salaam: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024