Wakala wa Farid Mussa aingia mitini Spain

Wakala wa Farid Mussa aingia mitini Spain

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
Winger wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania Farid Musa amefaulu majaribio yake kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Hispania ambako tayari pia amefaulu vipimo vya afya na kinachosubiriwa ni makubaliano kati ya klabu hizo mbili ili kukamilisha deal.

Lakini nyuma ya pazia, kuna story kwamba wakalaambaye alitakiwa kusimamia kila kitu kuhakikisha Farid anafanya majaribio akiwa nchini Hispania alilala-mbele kwa madai kwamba mteja wake hana vigezo ambavyo alivitarajia.

Yusuf Bakhresa ambaye yupo Spain na Fafrid ameitonya Shaffih Dauda kuwa mawakala wengine ni wababaishaji baada ya wakala huyo kutimkia kusikojulikana na kumuacha faridi kwenye ‘mataa’.

“Wakala John Sorzano aliyetakiwa kumsimamia Farid Musa kufanya majaribio nchini Hispania alimtelekeza, baada ya Faridi kutua Hispania yule wakala akamtufuta mtu mwingine ili amsimamie Faridi. Baada ya huyo wakala kumuona Faridi akaema hana viwango kwahiyo wote wakamtelekea”, anasema Yusuf ambaye ilibidi avae majukumu ya kuhakikisha Farid anapata nafasi ya kufanya amajariio kwenye klabu ya Tenerife.

“Kwa bahati nzuri mimi (Yusuf) nilikuwa hapa, ikabidi nianze kumtunza Farid. Nikafanya mawasiliano na viongozi wa Tenerife wakakubali kumpa nafasi ya kuendelea kufanya majaribio, baada ya Farid kuonesha uwezo mkubwa wakamkubali. Wale mawakala wakapata taarifa kwamba dogo amekubalika, waanza kuja kutaka kusimamia dili”.

“Mimi nimewapiga chini na nimeuambia uongozi wa Tenerife uandike barua rasmi kwa Azam. Muda wowote watatuma offer kwa klabu ya Azam na kufanya bishara ya kumuuza Farid”.
 
Ndio hao hao promota anadipu, wanaangalia matumbo Yao tu.
 
Asee apo kwenye heading nikajua dili lime shndikana
Kumbe safi, dogo akaze sasa



Dogo akubali tu hela yoyote hata akipewa Euro 500 kwa wiki, mafanikio hayaji kirahisi. Na hao Azam wasilete tamaa wambariki kijana hata bure aende tu. Uzalendo muhimu.
 
Dogo akubali tu hela yoyote hata akipewa Euro 500 kwa wiki, mafanikio hayaji kirahisi. Na hao Azam wasilete tamaa wambariki kijana hata bure aende tu. Uzalendo muhimu.
Yes wana cho weza kufanya Azam ni kutengeneza mkataba utakao fanya farid hat akija kwenda malaga au atletico au hata akija Yanga tena wao wata pata asilimia kadhaa ya pesa , faida endelevu hyo
 
Isije kua udaku then baada ya mda tunamuona chamanzi na hua wanarudi kimya kimya
 
Waandishi wa kibongo bana heading si indirectly proportional na contents ya ndanii..
 
Wabongo kwa kupenda short cut ni hatari. Haya sasa inabidi Tv yetu imuandalie mapokezi
 
Back
Top Bottom