Wakala wa Vipimo Tanzania na Zambia kushirikiana kusimamia matumizi sahihi ya vipimo

Wakala wa Vipimo Tanzania na Zambia kushirikiana kusimamia matumizi sahihi ya vipimo

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Wakala wa Vipimo Tanzania na Zambia kushirikiana kusimamia matumizi sahihi ya vipimo

Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) na Zambia (ZMA) zimesaini mkataba wa miaka mitatu (3) wa kushirikiana katika usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo ambapo utekelezaji wake umeanza mara tu baada ya kusainiwa.

Kusainiwa kwa mkataba huo ni sehemu ya maono ya viongozi wakuu wa nchi wa Tanzania na Zambia ambapo katika siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu kuapishwa kwake amefanikisha utiaji saini baina ya taasisi ya WMA na ZMA kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara hususani kwenye sekta ya vipimo.

Awali, Wakala wa Vipimo Zambia (ZMA) na wadau wa sekta ya mafuta wa Zambia walifanya ziara ya kikazi nchini Tanzania ambapo walishuhudia namna Serikali ya Tanzania imeiwezesha Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi yake ya WMA kununua vifaa vya kisasa na ujenzi wa kituo kikubwa Afrika Mashariki na Kati cha kuhakiki vipimo katika eneo la Kibaha, Pwani.

Chini ya Makubaliano hayo, mataifa hayo mawili yatatambua matokeo ya vipimo, vyeti vya uthibitisho, idhini za aina (type approvals), na uthibitishaji wa kisheria kutoka upande mmoja hadi mwingine. Mpango huu unatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa vikwazo vya kitaalamu katika biashara, kuboresha ulinganifu wa udhibiti, na kuongeza usahihi wa vipimo katika biashara kwa lengo la kuwalinda walaji wa pande zote.

Hafla ya utiaji saini imefanyika jijini Lusaka, Zambia tarehe 11 Desemba, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali na wataalamu kutoka nchi zote mbili. Kwa upande wa Tanzania Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lut. Jen Mathew Mkingule, alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, na upande wa Zambia wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Chipoka Mulenga (Mb.)
 

Attachments

  • publer-1765697069587.jpg
    publer-1765697069587.jpg
    79.1 KB · Views: 33
  • publer-1765697071465.jpg
    publer-1765697071465.jpg
    74.5 KB · Views: 31
  • publer-1765697072637.jpg
    publer-1765697072637.jpg
    79.1 KB · Views: 35
  • publer-1765697073764.jpg
    publer-1765697073764.jpg
    74.2 KB · Views: 39
  • publer-1765697074941.jpg
    publer-1765697074941.jpg
    99.9 KB · Views: 27
  • publer-1765697076340.jpg
    publer-1765697076340.jpg
    94.6 KB · Views: 30
  • publer-1765697077510.jpg
    publer-1765697077510.jpg
    98 KB · Views: 29
  • publer-1765697078769.jpg
    publer-1765697078769.jpg
    84.9 KB · Views: 31
  • publer-1765697080026.jpg
    publer-1765697080026.jpg
    73.2 KB · Views: 35
  • publer-1765697081255.jpg
    publer-1765697081255.jpg
    61.8 KB · Views: 29
  • publer-1765697082478.jpg
    publer-1765697082478.jpg
    75.2 KB · Views: 30
  • publer-1765697083744.jpg
    publer-1765697083744.jpg
    83.2 KB · Views: 32
  • publer-1765697085180.jpg
    publer-1765697085180.jpg
    84.4 KB · Views: 34
  • publer-1765697086372.jpg
    publer-1765697086372.jpg
    96.2 KB · Views: 32
Back
Top Bottom