Wakamatwa na Waziri kwa kutupa maganda barabarani

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh Aggrey Mwanri (mwenye suti) akiwa anasimamia kuwaweka chini ya ulinzi vijana watatu aliowakamata kwa kosa la kula maembe na kutupa maganda barabarani jijini Arusha.

DSC04581.JPG

Kwa habari zaidi: MICHUZI: mh. mwanry awajia juu viongozi wa manispaa ya arusha
 
Mwanri tunaomba uanzie DSM,ntakupa na maeneo, kwa mtogole,tandale sokoni,kkoo,mwenge,temeke stereo,tandika,buguruni sokoni, viongozi wetu msiwe wanafiki,lile jiji letu la DSM mbona hamfanyi hayo na ndo mnashinda mle mnafatilia michongo yenu pale bandarini/kiwanja cha ndege na mnapishana na mavi na maji yenye mikojo pale upanga kwenye majumba ya wahindi??ama ndo mnataka kuamsha hasira za wana-arusha?
 
Hizi ni zama za usanii na unafiki.................
ebo we jamaa vipi??????????
mimi nampa big up sana jamaa, vitu vidogo vidogo sana hivi lakini madhara yake ni makubwa , hivi jimmy paka hapao Arusha kuna madustbin lakini? kama yapo basi huyu mkuu wa mkoa ana haki ya kufanya hivyo na inabidi adhabi iweke , i mean wapigwe fain kali, nampa tano huyu mkuu wa mkoa
 
Mwanri tunaomba uanzie DSM,ntakupa na maeneo, kwa mtogole,tandale sokoni,kkoo,mwenge,temeke stereo,tandika,buguruni sokoni, viongozi wetu msiwe wanafiki,lile jiji letu la DSM mbona hamfanyi hayo na ndo mnashinda mle mnafatilia michongo yenu pale bandarini/kiwanja cha ndege na mnapishana na mavi na maji yenye mikojo pale upanga kwenye majumba ya wahindi??ama ndo mnataka kuamsha hasira za wana-arusha?
sasa wewe ushaambiwa mkuu wa mkoa wa Arusha-the geneva of Africa wewe unaleta stori zako za manzeshe na kiwalani.. wapi na wapi bana ni kama umetoka nje ya topic yaani hapa ni kama vile umempa bibi kidude ashuke mistari kwenye bit la Jay Z
 
Mkuu sio kama natetea uchafu... lakini kwangu kiongozi anayewaacha mafisadi wanatamba huku akikimbizana na watupa maganda ni msanii na mnafiki.
 
Kuna mengi sio ufisadi tuu. Big up Mheshimiwa na hata hapa Dar ukiwaona wakamate wakalipe faini ya sh. 50,000!
 
Unafiki tu na kutafuta umaarufu wa kijinga akamte wanaoiba kwenye halmashauri pesa za walala hoi sio hawa wanyonge.....very cheap
 
ebo we jamaa vipi??????????
mimi nampa big up sana jamaa, vitu vidogo vidogo sana hivi lakini madhara yake ni makubwa , hivi jimmy paka hapao Arusha kuna madustbin lakini? kama yapo basi huyu mkuu wa mkoa ana haki ya kufanya hivyo na inabidi adhabi iweke , i mean wapigwe fain kali, nampa tano huyu mkuu wa mkoa

Ni kweli Mwanri anajitutumua. Sitetei uchafu lakini kama hakuna dustbins ama mahala pa kutupa uchafu watu watupe wapi sasa? Nadhani Mwanri na Wizara yake wanatakiwa waweke miundombinu ya utupaji takataka ikiwa ni pamoja na dustbins ili mtu akitupa hovyo takataka wakati dustbin ipo achukuliwe hatua kali. Uchafu umetapakaa Tanzania nzima kwa kuwa hakuna mahala pa kutupa takakata na pia ukusanyaji wa taka ngumu katika miji yetu nao ni kichekesho, magari tya kukusanya taka yanasambaza taka mitaani inabidi nayo yakamatwe.
 
Hivi jamani tunamambo mangapi yamuhimu kwa maisha ya mtz? Mbona hawa viongozi siwahelewi? Wanafanya mambo ya ajabu sana. Tunashindwa kuwafatilia walarushwa na kuwanaviongozi waadilifu tunakaa kupambana na mambo ya ajabu.

wananiuzi hawa jamaa we acha tu.
 
sasa wewe ushaambiwa mkuu wa mkoa wa Arusha-the geneva of Africa wewe unaleta stori zako za manzeshe na kiwalani.. wapi na wapi bana ni kama umetoka nje ya topic yaani hapa ni kama vile umempa bibi kidude ashuke mistari kwenye bit la Jay Z

simaanishi Arusha isiwe Geneva mkuu ila naongelea ukubwa wa tatizo ndo maana nasema aanzie dar watu wanavyotupa chupa za mikojo barabarani,akaangalie jinsi mitaro inavyoziba kwa taka n.k,kwani wewe huioni dar inavyotoa uvundo kila kona kipindi cha mvua
 
Mwanri ameonesha mfano,sasa manispaa ya jiji la arusha na miji mingine igeni mfano huu jaman hata usafi nao una tushinda?
 
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh Aggrey Mwanri (mwenye suti) akiwa anasimamia kuwaweka chini ya ulinzi vijana watatu aliowakamata kwa kosa la kula maembe na kutupa maganda barabarani jijini Arusha.

DSC04581.JPG

Kwa habari zaidi: MICHUZI: mh. mwanry awajia juu viongozi wa manispaa ya arusha

Dar es Salaam maji ya mavi yametapakaakila mahali. mbona hatuoni akichukua hatua zozote. Hiyo ni janja ya kuwatisha vijana wa Arusha ambao ni wakereketwa wa CHADEMA.
 
Hivi jamani tunamambo mangapi yamuhimu kwa maisha ya mtz? Mbona hawa viongozi siwahelewi? Wanafanya mambo ya ajabu sana. Tunashindwa kuwafatilia walarushwa na kuwanaviongozi waadilifu tunakaa kupambana na mambo ya ajabu.

wananiuzi hawa jamaa we acha tu.

Hana lolote la maana Waziri huyu wa TAMISEMI kwani kwenye wizara yake ndiyo kuna uozo kuliko wizara yeyote ile hapa nyumbani Tanzania;lkn yeye MWANRI priority yake kubwa ni kuwakamata wanaotupa takataka Arusha!

Juzi tu Mbunge Mrema kama Mwenyekiti wa Kamati inayokagua Wizara ya TAMISEMI kazitaja hadi kwa majina Wilaya zilizochota mabilion ya hela kwa mishahara hewa lkn MWANRI hatujamsikia akiwakamata watendaji hao vigogo!

Madhara ya kutupa takataka ARUSHA hayaingii hata tone kwa madhara ya kutowakamata MAFISADI wenzao wanaotafuna hela zetu!
 
Mwanri tunaomba uanzie DSM,ntakupa na maeneo, kwa mtogole,tandale sokoni,kkoo,mwenge,temeke stereo,tandika,buguruni sokoni, viongozi wetu msiwe wanafiki,lile jiji letu la DSM mbona hamfanyi hayo na ndo mnashinda mle mnafatilia michongo yenu pale bandarini/kiwanja cha ndege na mnapishana na mavi na maji yenye mikojo pale upanga kwenye majumba ya wahindi??ama ndo mnataka kuamsha hasira za wana-arusha?

Atakuwa analipa kisasi kwa wana Arusha kuikataa CCM. Nina mpinga Mwanry kwa sababu zifuatazo
  1. Serikali ya mji inatakiwa kuweka Litters kila baada ya mita 200, je Arusha kuna Litters?
  2. Serikali inatakiwa ku-promote usafi kwa matangazo na kuelimisha wananchi ubora wa kuweka mji safi je serikali ya Arusha imefanya hivyo?
  3. Serikali inatakiwa kuweka bayana adhabu za kutupa taka ovyo kwenye mabango je Arusha wamefanya hivyo
  4. Kuweka mji kuwa msafi hakuhitaji polisi na bunduki kutishia watu bali ni elimu kwa umma na usimamizi wa sheria za jiji bila upendeleo na kuzitangaza zijulikane kwa wananchi siyo kuziweka kwenye ma-shelf tu
Mwanry alichokifanya kwa hawa vijana ni power show up, kuwa wao wana silaha na wanaweza kufanya chochote kile. Kama kweli yeye ni mchapa kazi aanzie na jiji la Dar.
 
Ashakum si matusi, lakini uyo waziri hamnazo (hayawani). Yaani kuwakamata watupa maganda ndio lazima uende na askari wawili na mmoja kati ya hao ana AK47? Halafu unawaita waandishi wa habari eti waje kukupiga picha huku umevaa suti na kuonyesha simu ya kiganjani (mtindo uliopitwa na wakati)?. Kweli wabongo tunao mawaziri!

Sawa, ni vizuri kuhimiza usafi wa jiji, lakini sio kihivyo. That is too much!
 
Mimi nadhani anastahili kupongezwa
Apongezwe kwa lipi kwanza akishindwa kusimamia kesi hiyo mahakamani awalipe fidia hao watu walipao kodi kwa jasho na yeye ndie anakula jasho lao kwani alitaka watupe wapi hizo taka na dustbin hakuna au alitaka weziweke kwenye mifuko ya makoti kisha wazitupe kwenye vyoo vyao?

Awashike kina RA na EL awafilisi kisha aweke dustbin kila kona ya miji kama anataka usafi
 
Ana mamlaka gani kisheria ya kukamata mtu na kumweka chini ya ulinzi?
 
Back
Top Bottom