Wakamatwa na Waziri kwa kutupa maganda barabarani

Wakamatwa na Waziri kwa kutupa maganda barabarani

serikali ya kikwete bwana, sasa watu watatembea na majuko ya uchafu kama wehu, kwa nini wasiweka mabin kwanza ndio wakamate watu, harafu mimi nadhani faini ndio suruhisho, au hii ni kuwapiga mkwara wana arusha
kuna siku haki itatembeaka lakini watoto wetu watakuwa katika majonzi kutokana na history zenu
 
Ashakum si matusi, lakini uyo waziri hamnazo (hayawani). Yaani kuwakamata watupa maganda ndio lazima uende na askari wawili na mmoja kati ya hao ana AK47? Halafu unawaita waandishi wa habari eti waje kukupiga picha huku umevaa suti na kuonyesha simu ya kiganjani (mtindo uliopitwa na wakati)?. Kweli wabongo tunao mawaziri!

Sawa, ni vizuri kuhimiza usafi wa jiji, lakini sio kihivyo. That is too much!

Halafu yule asiye na bunduki ni senior superitendent of police, ni cheo kikubwa kweli kushika watu wanaotupa maganda ya ndizi. Auxillary police watafanya kazi gani.

Anyway ni muendelezo wa maigizo ya viongozi wetu, wala msishangae
 
Waziri tupe high level strategy, kama kuna haja ya kamatakamata achia wenye kazi hiyo. Unataka kuua nzi kwa mzinga?

Is this the best use of your time ?
 
Huu ndo uwajibikaji tunaouhitaji hapa nchini, well done mheshimiwa, kama vipi ungeamuru huyo askari awachakaze kwa rsasi kabisa kwani maganda waliyotupa barabarani, yanasababisha mashimo katika barabara zetu tulizojenga kwa fedha nyingi na kisha wananchi wanapoona mashimo barabarani wanasema tumekula rushwa.
Hongera waziri, huu ni mfano mzuri kwa mawaziri wengine na hasa waziri wa nishati na madini, huyu anatakiwa kumkamata jirani yangu anayefungulia muziki wake kwa sauti ya juu na hivyo kusababisha mgao wa umeme mtaani kwetu, waziri wa mawasiliano aige pia, awakamate wauzaji wa simu pale kariakoo kwani maduka yao wameyapanga karibukaribu sana na hivyo kutuchanganya wateja, kwanini wasiweke maduka yao mbali kama vilivyo vituo vya mafuta ili bei ipungue.

Hongera waziri, umefanya vizuri kwani maganda hayo ungeyakanyaga ungechafua mdundo wako ulioung'arisha kwa dola za kimarekani
 
A most hilarious post.
 
  • Thanks
Reactions: Obe
TAMISEMI kuna scandals kibao za ubadhirifu wa fedha za umma, Waziri anakimbizana na watupa maganda. Kazi ipo.
 
Jamani tumtendee haki waziri,Kosa moja halifanyi kosa jingine kuwa halali.Kwa wale waliosoma sheria za mazingira wanaelewa wajibu unaotolewa na sheria ile kwa kila raia.Tusiende kwa ushabiki,na tukubaliane kuwa Waziri kama raia yeyote anayo haki kumwajibisha mvunja sheria yeyote.Tukiongozwa na dhana ya ondoa kibanzi kwenye jicho lako kabla ya kuondoa cha mwingine hatutafika.
 
Back
Top Bottom