Huu ndo uwajibikaji tunaouhitaji hapa nchini, well done mheshimiwa, kama vipi ungeamuru huyo askari awachakaze kwa rsasi kabisa kwani maganda waliyotupa barabarani, yanasababisha mashimo katika barabara zetu tulizojenga kwa fedha nyingi na kisha wananchi wanapoona mashimo barabarani wanasema tumekula rushwa.
Hongera waziri, huu ni mfano mzuri kwa mawaziri wengine na hasa waziri wa nishati na madini, huyu anatakiwa kumkamata jirani yangu anayefungulia muziki wake kwa sauti ya juu na hivyo kusababisha mgao wa umeme mtaani kwetu, waziri wa mawasiliano aige pia, awakamate wauzaji wa simu pale kariakoo kwani maduka yao wameyapanga karibukaribu sana na hivyo kutuchanganya wateja, kwanini wasiweke maduka yao mbali kama vilivyo vituo vya mafuta ili bei ipungue.
Hongera waziri, umefanya vizuri kwani maganda hayo ungeyakanyaga ungechafua mdundo wako ulioung'arisha kwa dola za kimarekani