Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Tusimlaumu JK bure kwenye hili. Mtatatizo ya procurement method yetu yamejali sana mambo ya CYA kuliko ufanisi. Tunapendelea open tenders kwenye miradi kwa kuogopa kuwa ukifanya vinginevyo utaonekana umekula. Tatizo la open tenders ni kuwa makandarasi wa maana hawaingii maana wanajua toka wali hawawezi kushindana na makandarasi uchwara kutoka China na kwingineko. Tukumbuke kuwa kutenda kuna gharama zake. Ndiyo maana Skanska aliishafunga virago na Noremco wanasuasua. Kama tunataka ubora na ufanisi ni lazima tuangalie uwezekano wa kutumia zaidi limited tenering ambapo makandarasi watakuwa pre-qualified. Technocrats wetu waanze kufanya hivi bila kuogopa shutuma za kula na mafisadi.
Kwa wale ambao wanadhani solution ni kuwapa wazawa badala ya wageni wanakosea. Ukweli ni kuwa ni makandarasi wachache wazawa wenye uwezo wa kitaalamu na kiufundi wa kuzimudu kazi hizi! Dhana ya makandarasi wetu wengi ni kupunguza gharama kwa kuajiri wataalamu wachache ( ni makandarasi wangapi wazawe wenye Quantity Surveyors qualified na wanaopewa madaraka kamili ya ku'price tenda zao?)na kutegemea zaidi kupenyeza rupia ili wapate engineer's estimate. Wakiipata hii wanafanya kila njia kufanya tenda yao iwe chini ya hii bila kujali gharama zao halisi! Mimi naamini makandarasi wetu walio makini badala ya kugombea hizo tenda kubwa wangejenga uwezo wao katika specialised areas ili waweze kushirikiana na hao wageni kama sub-contractors.
Mwisho, namuunga mkono mhandisi Mmasai kuwa uwezo wetu wa kutayarisha tenda documents pamoja na kusimamia mikataba una walakin mkubwa. Inabidi tufanye jitihada kubwa katika maeneo haya maana bila tenda air-tight na usimamizi makini tutaendelea kuliwa!