Wakandarasi Wanawake wamshukuru Mwenyekiti Chatanda kwa kuwapambania katika fursa za miradi

Wakandarasi Wanawake wamshukuru Mwenyekiti Chatanda kwa kuwapambania katika fursa za miradi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandarasi Wanawake Kanda ya Kati na Mashariki Tanzania Bi. Hidaya Abri amemshukuru Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda kwa kuendelea kuwapambania wakandarasi wanawake kupata mitaji inayowawezesha kufanikisha Utekelezaji wa tenda za wadau wa Maendeleo ikiwemo Serikali.

🗓️ Mei 16, 2024
📍 Dodoma

 
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania(UWT) Ndg. Mary Chatanda amewahimiza Wakandarasi wanawake kuchangamkia Fursa ya Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili waweze kuimarisha mitaji na ufanisi wa kazi zao, hatua ambayo itawawezesha kuaminiwa zaidi na hata kukabidhiwa miradi mikubwa zaidi ya kitaifa.

Chatanda ameyasema hayo Mei 16, 2024 wakati wa kikao cha wakandarasi Wanawake kilichofanyika Makao makuu ya UWT Dodoma.

"Tulipozungumza kwa mara ya kwanza katika Kikao chetu mlisema Kuna changamoto ya mitaji katika makampuni yenu sasa Rais Samia amesikia kilio chenu na ndio maana nawahamasisha wakandarasi wote wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo hii”Amesema mwenyekiti Chatanda na kuongeza

"UWT imefurahi kuona wakandarasi wanawake wanapata tenda kwenye miradi mbalimbali katika Wilaya na Mikoa nchi nzima,hii ni moja ya juhudi za UWT kuhakikisha wanawake wanapata tenda za Ujenzi wa Barabara kwa wingi."

IMG-20240516-WA0070.jpg
IMG-20240516-WA0074.jpg
IMG-20240516-WA0076.jpg
IMG-20240516-WA0072.jpg
IMG-20240516-WA0066.jpg
IMG-20240516-WA0064.jpg
IMG-20240516-WA0068.jpg
IMG-20240516-WA0060.jpg
IMG-20240516-WA0062.jpg
IMG-20240516-WA0058.jpg
 
Back
Top Bottom