Pre GE2025 Wakati CCM ishaanza kampeni za Urais wa uchaguzi Mkuu wa mwakani, je upinzani unangoja Nini kumtangaza mgombea wake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini Kwa sasa, ni dhahiri kuwa CCM ishaanza rasmi kumnadi mgombea wake wa Urais wa mwakani, ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Tumeshuhudia katika ziara alizofanya majuzi kwa madai kuwa ni ziara za kiserikali katika mikoa ya Rukwa na Morogoro, ambapo ziara hizo bila mashaka yoyote ni za kampeni ya Urais wa mwakani mwaka 2025 na si za kiserikali, kama wanavyodai wenyewe CCM.

Tukizingatia kuwa ujumbe wa Rais, katika ziara hizo ulikuwa na mawaziri kadhaa na Kila wanapotembelea, kazi kubwa ilikuwa ni kuwapa nafasi hao mawaziri wake Ili waeleze miradi ambayo wameitekeleza katika maeneo yao.

Hao mawaziri wanaoambatana na Rais, hawajapungua kumi!

Najaribu kufikiria ni kwanini sasa, CCM ndiyo wameona ni muda muafaka wa mawaziri hao kunadi kazi walizozifanya na miradi waliyoiteleleza na siyo kabla ya hapo??

Niwaombe wapinzani nao wasibweteke, ni lazima waunganishe nguvu hivi sasa na wamtangaze mgombea wao wa upinzani, ambaye naye atafanya kazi Moja ya kuzunguka nchini kote na kuanza kujinadi akiwa mgombea wa upinzani, kinyume Cha hapo itakuwa "Too Late"

Nakumbuka kuwa mwaka 2015, wakati upinzani wa nchi hii, ulipotoa upjnzani mkubwa sana Kwa CCM, katika historia ya toka siasa za vyama vingi uanzishwe, mwaka 1992, nyakati hizo vyama vya upinzani viliungsnisha nguvu ya pamoja, katika umoja waliouita UKAWA, na kumweka mgombea mmoja, ambaye alikuwa marehemu Edward Lowassa.

Kitu kingine ambacho Kambi ya upinzani inapaswa ifahamu ni kuwa, wao wanalazimika kuunganisha nguvu zao Ili kupambana na hiki chama kikongwe Cha CCM ambacho kimeotesha mizizi katika vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Matokeo ya kuunganisha nguvu hizo Kwa upande wa upinzani, ni ushindi mkubwa sana walioupata kuanzia wenyeviti wa mitaa na vitongoji, madiwani, wabunge na hata mgombea Urais, Kwa tiketi ya UKAWA, hayati Edward Lowassa, alivuna kura nyingi (pamoja na kumuibia) ambazo hazikuwahi kupatikana katika chaguzi zote katika historia ya toka uanzishwe mfumo huu wa vyama vingi.

Ni lazima vyama vya upinzani vitambue ukweli huu kuwa UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU
 
Halima mdee ndo anaweza kidogo kumnyapisha Samia Hao wengine hawawezi kuosogelea Moto wa dk Samia watapelezwa vibaya mno.
 
Kwa mambo yanayoendekea hapa nchini Kwa sasa, ni dhahiri kuwa CCM ishaanza rasmi kumnadi mgombea wake wa Urais wa mwakani, ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Tumeshuhudia katika ziara alizofanya majuzi kwa madai kuwa ni ziara za kiserikali katika mikoa ya Rukwa na Morogoro, ambapo ziara hizo bila mashaka yoyote ni za kampeni ya Urais wa mwakani mwaka 2025 na si za kiserikali, kama wanavyodai wenyewe CCM.

Tukizingatia kuwa ujumbe wa Rais, katika ziara hizo ni mawaziri kadhaa na Kila wanapotenbelea, kazi kubwa ni kuwapa nafasi huo ujumbe wake wa mawaziri, waeleze miradi ambayo wameitekeleza katika maendo yao.

Hao mawaziri wanaoambatana na Rais, hawapungui kumi!

Najaribu kufikiria ni kwanini sasa, CCM ndiyo wameona ni muda muafaka wa mawaziri hao kunadi kazi walixozifanya na miradi waliyoiteleleza.

Niwaombe wapinzani nao wasilale, ni lazima waunganishe nguvu hivi sasa na wamtangaze mgombea wao wa upinzani, ambaye naye atafanya kazi Moja ya kuzunguka nchini kote na kuanza kujinadi akiwa mgombea wa upinzani, kinyume Cha hapo itakuwa "Too Late"

Nakumbuka kuwa mwaka 2015, wakati upinzani wa nchi hii, ulipotoa upjnzani mkubwa sana Kwa CCM, katika historia ya toka siasa za vyama vingi uanzishwe, mwaka 1992, nyakati hizo vyama vya upinzani viliungsnisha nguvu ya pamoja, katika umojs waliouita UKAWA, na kumweka mgombea mmoja, ambaye alikuwa marehemu Edward Lowassa.

Kitu kingine nacho Kambi ya upinzani inapaswa ifahamu ni kuwa, wao wanalazimika kuiunganisha nguvu zao Ili kupambana na hiki chama kikongwe Cha CCM.

Matokeo ya kuunganisha nguvu hizo Kwa upande wa,upinzani, ni ushindi mkubwa sana walioupata Kambi ya upinzani, kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wabunge na hata mgombea Urais, Kwa tiketi ya UKAWA, hayati Edward Lowassa, alivuna kura nyingi (pamoja na kumuibia) ambazo hazikiwahi kupatikana katika chaguzi zote katika historia ya toka kianzishwe mfumo huu wa vyama vingi.

Ni lazima vyama vya upinzani vitambue ukweli huu kuwa UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU
Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa sijui unataka wapinzani waunganishe nguvu ili iweje?
 
Usikate tamaa.

Nikukumbushe kuwa mwaka 2015, pamoja na kuiba kote kura, walikofanya CCM, lakini wapinzani walipata kura nyingi sana
 
Naunga mkono hoja yako kuwa Kambi ya upinzani inapaswa impendekeze Tundu Lissu, kuwa mgombea wake👋👋
Na tumeshamuonya Samia akituibia Kura safari hii tunaingia Mabarabarani na kutumia Nguvu ya Umma.

People's Power...NO HATE NO FEAR.
 
Usikate tamaa.

Nikukumbushe kuwa mwaka 2015, pamoja na kuiba kote kura, walikofanya CCM, lakini wapinzani walipata kura nyingi sana
Sijakata tamaa bali nimelipuuza hilo zoezi litwalo uchaguzi.
 
Kwa mambo yanayoendekea hapa nchini Kwa sasa, ni dhahiri kuwa CCM ishaanza rasmi kumnadi mgombea wake wa Urais wa mwakani, ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Tumeshuhudia katika ziara alizofanya majuzi kwa madai kuwa ni ziara za kiserikali katika mikoa ya Rukwa na Morogoro, ambapo ziara hizo bila mashaka yoyote ni za kampeni ya Urais wa mwakani mwaka 2025 na si za kiserikali, kama wanavyodai wenyewe CCM.

Tukizingatia kuwa ujumbe wa Rais, katika ziara hizo ulikuwa na mawaziri kadhaa na Kila wanapotenbelea, kazi kubwa ilikuwa ni kuwapa nafasi hao mawaziri wake Ili waeleze miradi ambayo wameitekeleza katika maeneo yao.

Hao mawaziri wanaoambatana na Rais, hawajapungua kumi!

Najaribu kufikiria ni kwanini sasa, CCM ndiyo wameona ni muda muafaka wa mawaziri hao kunadi kazi walixozifanya na miradi waliyoiteleleza na siyo kabla ya hapo??

Niwaombe wapinzani nao wasibweteke, ni lazima waunganishe nguvu hivi sasa na wamtangaze mgombea wao wa upinzani, ambaye naye atafanya kazi Moja ya kuzunguka nchini kote na kuanza kujinadi akiwa mgombea wa upinzani, kinyume Cha hapo itakuwa "Too Late"

Nakumbuka kuwa mwaka 2015, wakati upinzani wa nchi hii, ulipotoa upjnzani mkubwa sana Kwa CCM, katika historia ya toka siasa za vyama vingi uanzishwe, mwaka 1992, nyakati hizo vyama vya upinzani viliungsnisha nguvu ya pamoja, katika umoja waliouita UKAWA, na kumweka mgombea mmoja, ambaye alikuwa marehemu Edward Lowassa.

Kitu kingine ambacho Kambi ya upinzani inapaswa ifahamu ni kuwa, wao wanalazimika kuunganisha nguvu zao Ili kupambana na hiki chama kikongwe Cha CCM ambacho kimeotesha mizizi katika vyombo vya usalama na ulinzi nchini.

Matokeo ya kuunganisha nguvu hizo Kwa upande wa,upinzani, ni ushindi mkubwa sana walioupata Kambi ya upinzani, kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wabunge na hata mgombea Urais, Kwa tiketi ya UKAWA, hayati Edward Lowassa, alivuna kura nyingi (pamoja na kumuibia) ambazo hazikiwahi kupatikana katika chaguzi zote katika historia ya toka uanzishwe mfumo huu wa vyama vingi.

Ni lazima vyama vya upinzani vitambue ukweli huu kuwa UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU
nadhani hapa tatizo ni uelewa na ufahamu juu ya nini maana ya chama tawala ...

hivi sasa kuna serikali kazini iliyopewa dhamana na jukumu la kuongoza nchi kupitia sanduku la kura...

na kinachotekelezwa na serilikali hiyo sikivu ya CCM ni ilani ya uchaguzi ya chama ya hicho,
na kinachoendelea hivi mh.Rais Dr.Samia Suluhu Hassan nikujaribu kukagua utekelezaji na hatua zilizofikiwa na zilizobaki katikati mambo mbalimbali ya maendeleo na kuwashukuru waTz kwa kukipa ridhaa chama cha Mapinduzi na kuwaeleza nina na matarajio ya baadae...

kwahivyo ni uposhaji kusema ati CCM imeanza kampeni za uchaguzi mkuu ujao 2025,

kufanya kampeni Lazima uwe na kitu kinaitwa ilani au mkataba mkononi, kilichosheheni ahadi, mipango na uelekeo wa serikali itakayoundwa, endapo chama husika kitachaguliwa kushika dollar na kuongoza serikali...

by the way,
upinzani unakwenda kueleza, kukagua au kushukuru nini kwa wananchi kama sio fujo tu na kutokuelewa vyema dhana ya chama tawala madarakani 🐒
 
Hivi Kwenye hizo ziara za kiserikali unazodai kuwa ni zenye kukagua miradi, ndiyo iwe za kukipigia debe chama Cha CC??😗
 
Ni lazima vyama vya upinzani vitambue ukweli huu kuwa UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU
Unazungumzia "umoja" gani hasa?' Subsidiaries' wa CCM? Huo ni umoja wa nguvu kweli?

Hata hivyo, sehemu kubwa ya CHADEMA sasa hivi ipo CCM; sasa sijui unataka muungano wa aina gani tena.

Mada yako, pamoja na kwamba sijasoma yaliyo humo katikati ya anddiko lenyewe; ni kama unahoji kwa nini CCM wawe tayari kwenye kampeni, huku CHADEMA na hao wengine wakiwa bado kwenye usingizi wa pono!

Sasa jiulize kwa nini hali iko namna hiyo? Kwa nini CHADEMA hawastuki?

Na siyo hivyo tu, umesikia CHADEMA wakihoji lolote kuhusu Tume ya uchaguzi; au utaratibu mzima wa uchaguzi utakavyo kuwa? Wewe ishara zote hizi hazikupi majibu ni wapi CHADEMA walipo sasa hivi?

Hata wakati CCM wakitekeleza mipango ya ushindi huko mitaani, kama wanavyofanya sasa hivi kupitia kwa wizara ya Tawala za Mikoa, na wajumbe wa mitaani wakishughulika mitaani, umesikia sauti yoyote toka CHADEMA? Waziri Masabuni, yule wa mapolisi anapojigamba kwa mipango ya kutumia jeshi hilo wakati wa chaguzi, umesikia sauti yoyote toka CHADEMA?
 
Na tumeshamuonya Samia akituibia Kura safari hii tunaingia Mabarabarani na kutumia Nguvu ya Umma.

People's Power...NO HATE NO FEAR.
Hiyo "nguvu ya umma" mtaitoa wapi, wakati mnasambaratishwa sasa hivi kabla ya yote?

Kama kutatokea "nguvu ya umma", hiyo nguvu kamwe haitatokana na maandalizi yaliyofanywa na CHADEMA.

Wengi wenu mmekwisha nunuliwa, ndiyo maana chama hakijihusishi na lolote wakati 'critical' kama huu kuelekea kwenye chaguzi.
 
Uwezekano wa kuondolewa madarakani CCM na chama au muungano wa vyama vya upinzani kwenye ngwe hii ya uchaguzi inazidi kuwa hafifu zaidi baada ya CHADEMA kuwa 'compromized'.

Matumaini pekee yaliyo baki wazi ni njia mbadala za kuikomesha CCM, ambazo hazihusiani na vyama vya kisiasa.

Inawezekana sana.
 
Bado Mimi naamini kuwa, ingawaje wapo baadhi ya viongozi wachache wa upinzani, ambao inaelekea wameshapokea rushwa, lakini bado vile vile naamini wapo viongozi makini wa upinzani kama Tundu Lissu, ambao hawayumbishwi na hayo mapesa ya Abdul
 
Hivi Kwenye hizo ziara za kiserikali unazodai kuwa ni zenye kukagua miradi, ndiyo iwe za kukipigia debe chama Cha CC??😗
sio kupigia debe CCM,
ni lazima kuielezea CCM kwa wananchi kwasababu ndio iliyopewa dhamana ya kuongoza nchi...

yaani ushinde uchaguzi, then uweke mikono nyuma kusubiri uchaguzi mwingine hali ya kua ilani yako ya uchaguzi ndio dira na uelekeo wa serikali. utajuaje sasa kama inatekelezwa ama laah bila kukagua mara kwa mara nchi nzima?

katiba ya nchi iko wazi kabisa kwamba "the winner takes all" kwenye uchaguzi...

wapinzani hawakushinda uchaguzi wanakwenda kueleza nini kwa wananchi na hata katiba haijawaelezea chochote baada ya kushindwa? 🐒
 
Uwezekano wa kuondolewa madarakani CCM na chama au muungano wa vyama vya upinzani kwenye ngwe hii ya uchaguzi inazidi kuwa hafifu zaidi baada ya CHADEMA kuwa 'compromized'.

Matumaini pekee yaliyo baki wazi ni njia mbadala za kuikomesha CCM, ambazo hazihusiani na vyama vya kisiasa.

Inawezekana sana.
kujipa matumaini na kuijipotosha mwenyewe kizembe ndio huku sasa 🐒
 
Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini Kwa sasa, ni dhahiri kuwa CCM ishaanza rasmi kumnadi mgombea wake wa Urais wa mwakani, ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Tumeshuhudia katika ziara alizofanya majuzi kwa madai kuwa ni ziara za kiserikali katika mikoa ya Rukwa na Morogoro, ambapo ziara hizo bila mashaka yoyote ni za kampeni ya Urais wa mwakani mwaka 2025 na si za kiserikali, kama wanavyodai wenyewe CCM.

Tukizingatia kuwa ujumbe wa Rais, katika ziara hizo ulikuwa na mawaziri kadhaa na Kila wanapotembelea, kazi kubwa ilikuwa ni kuwapa nafasi hao mawaziri wake Ili waeleze miradi ambayo wameitekeleza katika maeneo yao.

Hao mawaziri wanaoambatana na Rais, hawajapungua kumi!

Najaribu kufikiria ni kwanini sasa, CCM ndiyo wameona ni muda muafaka wa mawaziri hao kunadi kazi walizozifanya na miradi waliyoiteleleza na siyo kabla ya hapo??

Niwaombe wapinzani nao wasibweteke, ni lazima waunganishe nguvu hivi sasa na wamtangaze mgombea wao wa upinzani, ambaye naye atafanya kazi Moja ya kuzunguka nchini kote na kuanza kujinadi akiwa mgombea wa upinzani, kinyume Cha hapo itakuwa "Too Late"

Nakumbuka kuwa mwaka 2015, wakati upinzani wa nchi hii, ulipotoa upjnzani mkubwa sana Kwa CCM, katika historia ya toka siasa za vyama vingi uanzishwe, mwaka 1992, nyakati hizo vyama vya upinzani viliungsnisha nguvu ya pamoja, katika umoja waliouita UKAWA, na kumweka mgombea mmoja, ambaye alikuwa marehemu Edward Lowassa.

Kitu kingine ambacho Kambi ya upinzani inapaswa ifahamu ni kuwa, wao wanalazimika kuunganisha nguvu zao Ili kupambana na hiki chama kikongwe Cha CCM ambacho kimeotesha mizizi katika vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Matokeo ya kuunganisha nguvu hizo Kwa upande wa upinzani, ni ushindi mkubwa sana walioupata kuanzia wenyeviti wa mitaa na vitongoji, madiwani, wabunge na hata mgombea Urais, Kwa tiketi ya UKAWA, hayati Edward Lowassa, alivuna kura nyingi (pamoja na kumuibia) ambazo hazikuwahi kupatikana katika chaguzi zote katika historia ya toka uanzishwe mfumo huu wa vyama vingi.

Ni lazima vyama vya upinzani vitambue ukweli huu kuwa UMOJA NI NGUVU na UTENGANO NI UDHAIFU
Serikali iliyopewa ridhaa na umma inawajibika wakati wowote kueleza imefanya nini katika yale iliyoahidi ilipoomba ridhaa ya kuongoza dola!

Kwa hiyo siyo sahihi na sioni mantiki yoyote hata kusema ziara za Mhe. Rais na mawaziri ni kampeni. Ziara za kuimarisha Chama zinafanywa na Katibu Mkuu na Sekretarieti yake, ambazo ni kama zile za kina Mbowe na Lissu mikoani. # Wewe hutaki kujua serikali imefanya nini? 🙏🙏🙏
 
Je Kwa kauli ya Rais kutamka hadharani huko katika jimbo la Kilosa, kutamka kuwa katika uchaguzi ujao wa ubunge anawataka wananchi wa jimbo Hilo wamchague Mbunge Palamagamba Kabudi kuwa mgombea wao, hivi hiyo nayo unaweza iita kuwa ni katika kuelezea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali yake ya CCM??
 
Hiyo "nguvu ya umma" mtaitoa wapi, wakati mnasambaratishwa sasa hivi kabla ya yote?

Kama kutatokea "nguvu ya umma", hiyo nguvu kamwe haitatokana na maandalizi yaliyofanywa na CHADEMA.
Nguvu ya Umma itatokana na huu Umma tunaoutetea japokuwa ni kazi ngumu kwa sababu huu Umma wenyewe UMEZEZETESHWA kwa muongo mingi.

Bangladesh all over again in East Africa ✌️
 
Bado Mimi naamini kuwa, ingawaje wapo baadhi ya viongozi wachache wa upinzani, ambao inaelekea wameshapokea rushwa, lakini bado vile vile naamini wapo viongozi makini wa upinzani kama Tundu Lissu, ambao hawayumbishwi na hayo mapesa ya Abdul
Na mbaya zaidi, hawa (umetaja huyo mmoja tu, ambaye hakuna anayemtilia mashaka) ndio sasa wanaotafutiwa njia za kuwadhibiti, kwa kuvitumia hivyo hivyo vyama tunavyo viita vya upinzani!
 
Back
Top Bottom