Wakati Diamond akiwasihi Watanzania kutosapoti show za Promota Victor, Kiba na MwanaFA busy na show

Wakati Diamond akiwasihi Watanzania kutosapoti show za Promota Victor, Kiba na MwanaFA busy na show

Ujue kuna watu kama Sugu na Jide hawataki kabisa kufanya kazi na Clouds, lakini Nassib kafanya nao Fiesta na kazi zingine.
Maonesho ni mkataba ambao unaweka makubaliano mezani, hutaki unaacha au unataka unaingia mkataba.
Sio ajabu Clouds kushindwana na Jide lakini wakawezana na TI na Davido. Huwezi lazimisha mgomvi wako awe mgomvi wa wote.
Mbona Nassib alikubali kufanya naye kazi licha ya kuyajua malalamiko ya Ambwene na Khalid? Na walilalamika hadharani wote tukajua.
Si unaona walimu hulalamika kwa kuchelewa mishahara au mishahara midogo, lakini zikitangazwa nafasi za kazi za walimu, bado watu watajitokeza.
Kuna msemo usemao, ukiona umedhulumiwa au kudhulumika basi ujue kuna mahali ulizembea hadi ukaacha mwanya wa kudhulumiwa au kudhulumika.
Yawezekana Mwana FA amejua alikozembea hadi akadhulumiwa, na sasa kawa makini na amerudi kufanya naye biashara. Muziki ndio kazi yake ni lazima aifanye.
Woga wako ndio umasikini wako, leo anafukuzwa kazi rafiki yako na kesho unaajiriwa wewe. Ni vema kubadili fikra zetu hasa kwenye masuala ya kazi na kuingiza vipato.
Ova
 
Back
Top Bottom