Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati nikitafakari maendeleo ya wanasayansi wa Uingereza kutumia DNA za watu watatu tofauti ili kuzalishaji mtoto mmoja kwa lengo la kuzuia magonjwa ya kurithi yasiyoambukiza na kutibika, nikawaza sisi Tanzania wanasayansi wetu wanasaidiwa vipi na CCM kufanya tafiti mbali mbali kwa maslahi ya Taifa.
Wakati wenzetu waliowekeza kwenye tafiti za kisayansi wanaelekea kwenye matumizi makubwa ya Artificial Intelligence (AI) kwenye kujiletea maendeleo yao, sisi chama kilichoko madarakani vikao vyao vyote wanawaza nini cha kufanya ili kuizuia CHADEMA kufanya siasa kwa ufanisi.
Hii nchi haiwezi kuendelea kwa kufanya siasa za ghiliba ama kwa kutowekeza kwenye Elimu na tafiti za kisayansi. Ujinga Maradhi na Umaskini wa Watanzania utaondolewa kwa kuwa na chama chenye kipaumbele cha kufanya tafiti za kisayansi, na siyo CCM hii yenye kutumia zaidi ya asilimia tisini na tisa (99%) ya muda wake kuwaza mbinu gani haramu watatumia ili kubaki madarakani.
La kuvunda halina ubani!!