Wakati Duniani viongozi wa nchi wanaanzia miaka 40 huku kwetu viongozi wanaanzia miaka 60 kuendelea; tutapata maendeleo?

Wakati Duniani viongozi wa nchi wanaanzia miaka 40 huku kwetu viongozi wanaanzia miaka 60 kuendelea; tutapata maendeleo?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Dunia inabadilika sana, inakwenda kasi sana. Siyo Dunia ya busara na heshima tena bali ni Dunia ya akili mpya zinazoweza kutatua changamoto.

Hakuna Sehemu Duniani maendeleo yanaletwa na busara na hekima na hakuna uhusiano kati ya umri na busara. Kama ujanani ulikosa busara na hekima siyo rahisi kuvipata uzeeni.

Tanzania viongozi wanatokana na busara na hekima siyo na utashi au uwezo wakufanya kazi. Hali hii imepelekea mashirika mengi kupewa wazee waliostaafu, bodi nyingi kupewa wazee na sasa vyama vya siasa vimeanza kuwaza kuwapa nafasi wazee kuliko vijana.

Maoni yangu, ni kosa chama cha mapinduzi kutegemea Wasira, Ponda, Sumaye nk kuwa Makamu mwenyekiti wa chama. Tuanze kutafakari namna yakuwapa vijana hizi nafasi kuongeza ushindani.

Asilimia 80 ya wajumbe wa bodi ni wazee, Wakuu wa taasisi ni wazee, washauri wa viongozi wakuu wa nchi ni wazee na wote hawa hakuna aliyefanya vizuri ujanani. Hawa wazee wanaweza kuwa sehemu ya maamuzi ya hoja za ulimwengu wa sasa.

Tunatakiwa sasa tuanze kufocus kwenye vijana wenye 30 yrs kama walivyoaminiwa akina Salim Ahmed Salim....tukiwapa madaraka vijana itatusaidia kujua viongozi wa wakuu watakaoendana na wakati wa sasa.

Upo wakati naamini mtu kama January Makamba ni kiongozi mzuri aliyezaliwa kwenye jamii yenye roho mbaya. Upo wakati naamini akina MtaKa ni viongozi wenye maono wanaoharibiwa na mfumo. Upo wakati naamini kijana kama Nassary alikuwa kiongozi mzuri ila amefichwa asisaidie nchi, upo wakati naamini Mnyika ni akili kubwa isiyo pewa nafasi kutokana na chama same applies kwa akina NONDO ni

Kutafakari upya kuanza kuwaacha wazee wale pensheni vijana wapate ajira
 
sample size yako ni nchi ngapi??? na hizo nchi umechagua methodology gani kuzipata
 
Back
Top Bottom