..Sisi Watanzania tunapenda sana kulalamika.
..EAC ya kwanza ilivunjika mwaka 1977.
..EAC mpya ilizaliwa mwaka 1999.
..Sasa tujiulize kwanini hatukujiimarisha ktk hiyo miaka 22 tuliyokuwa nje ya jumuiya?
..Halafu toka 1999 mpaka hivi tunavyozungumza ni miaka 20+ lakini bado Watanzania tuna malalamiko yaleyale kama ilivyokuwa mwaka 1977.
..Naipenda sana Tz na ninapenda tunufaike kutokana na mashirikiano na majirani zetu, lakini wakati mwingine nadhani Watanzania tunatumia muda mwingi kulalamika na hali hiyo inatuzuia kutafuta mbinu za kunufaika na fursa zilizoko ktk jumuiya.
cc
Nguruvi3,
Kichuguu
Mkuu nakubaliana nawe 101%. Watanzania bado wanalalamika kuhusu resources zilizotumika katika ukombozi
Nilishangaa sana watu na tena viongozi wakubwa tu wakisema muda wa kutumia rasilimali kwa wengine umepita
Ukweli kwa tulioona ni kwamba Tanzania haikutumia rasilimali kukomboa nchi za SADC.
Tanzania ilitoa hifadhi lakini siliha zilitoka nchi nyingine. Waliokwenda kutafuta ni Wapigania Uhuru, Tanzania iliwapa passport na logistic. Misaada ya wakimbizi ilitoka nje, Tanzania ilikuwa host tu wa Makambi ya wakimbizi
Lakini pia watu lazima waelewe, tulitumia rasilimali kidogo kwa usalama wetu.
Watu wa Mtwara wanajua hali ilikuwaje wakati huo Mreno akiwepo. Hivyo, tulikuwa na chaguo la kutafuta usalama au tukabiliane na madhila.Jiografia haikutuweka sawa na Kenya au Uganda.
Ushiriki wetu katika ukombozi ulikuwa kwa faida yetu.
Ukombozi ulitupa fursa ya SADC na ushirika na Zambia ilikuwa kielelezo cha awali.
Tumeshindwa kutumia fursa hizo sasa tunalalamika rasilimali za ukombozi.
Msumbiji ilikombolewa miaka 45 iliyopita ,tunalalama tu kwamba tumetumia rasilimali badala ya kutafuta fursa.
Tukirudi EAC nako ni kama JokaKuu alivyooeleza. Sisi tuna fursa ya kuwa wazalishaji wakubwa wa chakula na soko lipo tayari. Badala ya kuchangamkia fursa bado tunalalama Kenya na EAC ya 1977.
Katika EAC ya 1977 haukubeba mzigo wowote. Wakati tunatumia bidhaa za Maswiani na Jinja, Blue Band na Lifebuoy etc Nyerere alianza kutujengea uwezo wa viwanda ambavyo tulishindwa kuviendeleza na kuviuza kama si kugeuza maghala. Kenya au Uganda wanahusika vipi?
Tumezidi kulalamika hatuna new ideas. Watanzania siyo creative kwa namna nyingi.
Hatuwezi kuishi kwa historia, lazima tubadilike! tuwe wabunifu na tuelewa majirani zetu si maadui ni washindani
Jiulize kwanini Kahawa ilimwe Kagera , soko liwe Uganda? Kwanini Iliki ilimwe K'njaro soko liwe Kenya?
Kwanini tuagize mchele Korea badala ya Kenya na Uganda kuagiza kutoka Mbarali?
Kwanini mahindi yaoze maghalani Mbeya wakati Kenya kuna njaa? wakati Burundi na Kongo wanahitaji?
Kwanini tupige debe la SGR ya Mwanza halafu tushindwe kutumia SGR ya Tazara kusafirisha bidhaa?
Tukwama wapi ku negotiate na Zambia hata kama ni kuwalipa kidogo ili tunafaike zaidi?
Tuache kulalama, tunakiwa tukimbie na wenzetu .