Wakati filbert bayi anavunja rekodi za mbio, nyerere alivunja rekodi ya kuwaonea tz

Wakati filbert bayi anavunja rekodi za mbio, nyerere alivunja rekodi ya kuwaonea tz

Naomba wapiga makofi wa Nyerere waniambie Kama kweli Nyerere ni raisi mwema anayependa watu wake baada ya kusema yaliyomtokea Mzazi wangu:

1. 1965- Mali Yake sasa ni ya serikali. Hajapewa hata senti Moja hata baada ya kuikana pasi ya mkoloni na kuwa raia wa nchi huru ya Nyerere. Kosa lake? Kufanya kazi kwa bidii bila ya kuiba na kuweza kutajirika . Alipoteza nyumba na Magari na biashara Zake zote.

2. 1980- sokoine na Nyerere wakaamua kuwa wafanyabiashara wote ni wezi na kuwapora Mali zao tena Kama Hawana risiti. Utapata risiti wapi Wakati huruhusiwi kuleta Mali au kuwa na dola??
Wananchi hao hao wanaompigia makofi na kumwita baba wa taifa walikuwa wanapewa Sukari, unga na Mchele kwa resheni na walalahoi wanalala na kufa na Njaa vijijini.

3. Muhimbili Hamna dawa lakini yeye anakimbizwa ulaya kutibiwa na Wakoloni. Na Mpaka Leo tunasumbuka na Kuishi Maisha Mafupi duniani.

4. Wananchi chini Yake walikuwa Hawana Haki ya kuchagua Chama cha siasa wala kumpinga maneno Yake . Hamna ruhusa kusafiri wala kufikiri darasani. Kwa kifupi nchi aliitawala Kama kijiji chake. Mimi binafsi napata kichefuchefu nikisikia watu wanampigia makofi.
 
Kwa wapenda wa historia

Sote tunayakumbuka majina kama vile Filbert Bayi na Nyerere.

Isipokuwa tofauti zao kubwa ni hii

wakati Fibert Bayi anavunja rekodi za mbio na kuipatia sifa kem kem tz, nyerere alivunja rekodi ya kuwadhalilisha na kuwafanya wa tz wajinga kwa ndoto zake za azimio la arusha owekwa

video ya filbert bayi alipovunja rekodi ilowekwa 1957

https://www.youtube.com/watch?v=IvKX22TOCCA

hasa mikoa ya kusini halihikandamiza mahendereo
 
Nyerere halikuwa mbinfsi na wivu wakijinga na mroho wa wamwezie kwann kapata kiukweli nyerere hamshukuru mungu kwa kujitoa mapema kwenye siasa nahamii inchi hii yeye ndiye haliyehalibu hunapokonya viwanda na hunafukuza wawekezaji wakati wananchi wako bado hawajasoma
 
Wakati wa Nyerere tulikuwa tunavaa makatambunga tukijiona wajanja, maisha haya.
 
Kwa wapenda wa historia

Sote tunayakumbuka majina kama vile Filbert Bayi na Nyerere.

Isipokuwa tofauti zao kubwa ni hii

wakati Fibert Bayi anavunja rekodi za mbio na kuipatia sifa kem kem tz, nyerere alivunja rekodi ya kuwadhalilisha na kuwafanya wa tz wajinga kwa ndoto zake za azimio la arusha owekwa

video ya filbert bayi alipovunja rekodi ilowekwa 1957

https://www.youtube.com/watch?v=IvKX22TOCCA

Utafiti wako siyo kamili... Filbert Baye alitokana na Nyerere ...! kumbuka timu ya Olympic ya Tanzania ilikua inakaa Kilmanjaro Hotel na serikali ilikua inalipa kila kitu kwa wachezaji kuanzia mazoezi mpaka malazi yao....! Bayi peke yake angewezaje?

Nyerere kuliamini Azimio la Arusha ilitokana kwanza na imani yake ya maendeleo kwa watanzania wote....miaka ile kiongozi mbinafsi angeweza kujibinafsisha kila kitu bila pingamizi yoyote... !
Inafikiri Nyerere angekua na akili ya Lowassa au Kikwete kunamtanzania yeyote angeweza hata kumiliki bajaji? Barabara zingejengwa, shule za kata tele na bajaji za wajawazito kibao tu....lakini Nyerere alianza na kuwa himiza watanzania wawe wakombozi halisi wa maisha yao na akalazimisha dola imtumikie Mwananchi.
Azimio la Arusha limekua chachu ya maendeleo kwa hata mataifa tofauti na Tanzania....! Azimio la Arusha ambalo lilitaka njia kuu za uchumi kumilikiwa na Serikali halikukosea ....serikali ya China ndivyo inavyo endeshwa na kila mtu anatambua uchumi wa China ulipo....mwaka 2008 kuanguka kwa uchumi wa DUNIA serikali zote za nchi za kibepari zilimiliki njia kuu za uchumi za mataifa yao ili kunusuru uchumi uliokua unaanguka mfano Marekani, Uingereza n.k.
Ardhi hii siyo mali ya mtu km ilivyo Kenya na kwingineko ardhi ni mali ya Watanzania wote (serikali) .... km nyerere angetaka kujimilikisha Bonde lote la Ngorongoro angeshindwa vipi?

Toa tathmini kamili tuone wapi unaelekea ....!
 
Back
Top Bottom