Wakati gani bunge la Tanzania lilikuwa bunge?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kuna malalmiko, kuwa siku hizi bunge si bunge. Ni afadhali la miaka ya nyuma.

Kuna minong'ono, kuwa bunge la sasa ni mfano tu wa bunge, kwa maslahi ya watawala. Hata wengine wamediriki kutamani bunge livunjwe.

Kwani ni wakati gani bunge la Tz lilishawahi kuwa bunge?

Inasemekana, kuna wakati bunge lilipokuwa bunge, lilikuwa na uwezo wa kuitikisa Serikali hadi ishike adabu. Lilishawahi kumtoa machozi kiongozi mkubwa. Liliweza kumwajibisha mtu mkubwa bila kujali ukubwa wake. Hilo lilikuwa bunge, alau, inavyosemekana.

Inadaiwa, eti kwamba bunge la sasa lipo mfukoni mwa Serikali. Ndiyo maana, pamoja na kudaiwa kuwa bunge ni mhimili unaojitegenea, mkubwa wake hawezi kufurukuta mbele ya mwenyekiti wa mhimili uliojicjimbia zaidi. Haruhusiwi kuwa na mtazamo tofauti na WA Serikali.

Inasemekana, bunge ambalo ni chombo cha kutunga Sheria, lenyewe halifuati Sheria.

Malalmiko yamekuwa mengi sana, ya watu kudai kuwa bunge la sasa si bunge.

Swali: kama bunge la sasa si bunge, ni lini bunge lilikuwa bunge?
 
Mimi sijui lakini nakubaliana na wewe kuwa bunge la sasa ni kibogoyo lililowekwa mfukoni na ule mhimili uliojichimbia zaidi.Mfano tumeona spika ndugai alipotoa maoni yake binafsi alivyoshughulikiwa na ule mhimili.kama tungekuwa na bunge imara asingejiuzulu maana hakuna kosa alilofanya.
 
Nasikia, mkuu wa mhimili uliojichimbia zaidi si bosi wa mkuu wa bunge. Ni mihimili inayojitegemea. Iweje familia moja iipangie nyingine namna ya utendaji kazi?

Mimi siyo mwanasheria, lakini inasemekana, bunge ni mhimili unaojitegemea, na unao wajibu wa kuusimamia ule mhimili uliojichimbia zaidi. Iweje anayesimamia amwogope anayesimamiwa?
 
Kuna malalmiko, kuwa siku hizi bunge si bunge. Ni afadhali la miaka ya nyuma.

Kuna minong'ono, kuwa bunge la sasa ni mfano tu wa bunge, kwa maslahi ya watawala. Hata wengine wamediriki kutamani bunge livunjwe.

Kwani ni wakati gani bunge la Tz lilishawahi kuwa bunge?

Inasemekana, kuna wakati bunge lilipokuwa bunge, lilikuwa na uwezo wa kuitikisa Serikali hadi ishike adabu. Lilishawahi kumtoa machozi kiongozi mkubwa. Liliweza kumwajibisha mtu mkubwa bila kujali ukubwa wake. Hilo lilikuwa bunge, alau, inavyosemekana.

Inadaiwa, eti kwamba bunge la sasa lipo mfukoni mwa Serikali. Ndiyo maana, pamoja na kudaiwa kuwa bunge ni mhimili unaojitegenea, mkubwa wake hawezi kufurukuta mbele ya mwenyekiti wa mhimili uliojicjimbia zaidi. Haruhusiwi kuwa na mtazamo tofauti na WA Serikali.

Inasemekana, bunge ambalo ni chombo cha kutunga Sheria, lenyewe halifuati Sheria.

Malalmiko yamekuwa mengi sana, ya watu kudai kuwa bunge la sasa si bunge.

Swali: kama bunge la sasa si bunge, ni lini bunge lilikuwa bunge?
Awamu ya kwanza,Awamu ya pili,Awamu ya tatu na Awamu ya nne kulikuwa na Bunge lakini kuanzia 2015 hadi sasa chini ya Job Ndugai na Tulia Ackson hakuna Bunge ila ni maigizo tu kuwa kuna Bunge.
 
Bunge la tisa...Mabunge mengine ya nyuma sikuyafuatilia.....

Kuanzia kwa Ndugai ndio hapo bunge lilianza kuharibika na sasa limekuwa hovyo kuliko neno lenyewe hovyo.

Nina uhakika Leo hii tungepata kuwa na kura ya maoni kama bunge la sasa linatija ama livunjwe....,Asilimia 99 watataka livunjiliwe mbali...

NB: Bunge kama mhimili ni Jambo zuri kuwepo...ila Wabunge tulonao ndio Hovyo
 
Ukweli ndiyo huo.
 
Kuna minong'ono, kuwa bunge la sasa ni mfano tu wa bunge, kwa maslahi ya watawala. Hata wengine wamediriki kutamani bunge livunjwe.

BINADAMU AKIKOSA MBADALA HUWA ANAKUWA MNYAMA, TUWAOMBE WANASIASA WASIANZE KUWAFANYA WATANZANIA KUFIKIRI VIBAYA, chonde chonde.
 
Kuna malalmiko, kuwa siku hizi bunge si bunge. Ni afadhali la miaka ya nyuma.

Kuna minong'ono, kuwa bunge la sasa ni mfano tu wa bunge, kwa maslahi ya watawala. Hata wengine wamediriki kutamani bunge livunjwe.

Kwani ni wakati gani bunge la Tz lilishawahi kuwa bunge?

Inasemekana, kuna wakati bunge lilipokuwa bunge, lilikuwa na uwezo wa kuitikisa Serikali hadi ishike adabu. Lilishawahi kumtoa machozi kiongozi mkubwa. Liliweza kumwajibisha mtu mkubwa bila kujali ukubwa wake. Hilo lilikuwa bunge, alau, inavyosemekana.

Inadaiwa, eti kwamba bunge la sasa lipo mfukoni mwa Serikali. Ndiyo maana, pamoja na kudaiwa kuwa bunge ni mhimili unaojitegenea, mkubwa wake hawezi kufurukuta mbele ya mwenyekiti wa mhimili uliojicjimbia zaidi. Haruhusiwi kuwa na mtazamo tofauti na WA Serikali.

Inasemekana, bunge ambalo ni chombo cha kutunga Sheria, lenyewe halifuati Sheria.

Malalmiko yamekuwa mengi sana, ya watu kudai kuwa bunge la sasa si bunge.

Swali: kama bunge la sasa si bunge, ni lini bunge lilikuwa bunge?
Enzi zile Spika akiwa Samwel Sita., kikosi kilikuwa kina Dr Silaa., Antipas Lisu, Zito Kabwe na wengine wengi daah atleast sirikali ilikuwa inaumiza kichwa., lakin leo hii wabunge wa zari la mentali full kugonga meza tu.
 
Kuna minong'ono, kuwa bunge la sasa ni mfano tu wa bunge, kwa maslahi ya watawala. Hata wengine wamediriki kutamani bunge livunjwe.

BINADAMU AKIKOSA MBADALA HUWA ANAKUWA MNYAMA, TUWAOMBE WANASIASA WASIANZE KUWAFANYA WATANZANIA KUFIKIRI VIBAYA, chonde chonde.
Acha zako Bunge siyo mahali pa kupiga pesa pekee bali ni kwa ajili ya kuendeleza Amani na Mshikamano wa nchi.Leo Bunge limekuwa ndiyo chanzo cha Matabaka tabaka kwa sababu tu ya kutosimamia sheria vizuri.
 
Enzi zile Spika akiwa Samwel Sita., kikosi kilikuwa kina Dr Silaa., Antipas Lisu, Zito Kabwe na wengine wengi daah atleast sirikali ilikuwa inaumiza kichwa., lakin leo hii wabunge wa zari la mentali full kugonga meza tu.
Chacha mwamba wangwe hatari nanusu
 
Chacha mwamba wangwe hatari nanusu
Enzi hizo nahis mwana msoga alikuwa hapati usingizi., ila 2025 raia tuanze harakati mapema za kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja ili tuchague vichwa vyenye akili na vyenye kulitetea Taifa lenye asili ya Tanganyika.
 
Tanzakiza hakuja wahi kuwa na Bunge na mahakama bali vivuli vya mihimili kwenye katiba kibogoyo.
 
Enzi hizo nahis mwana msoga alikuwa hapati usingizi., ila 2025 raia tuanze harakati mapema za kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja ili tuchague vichwa vyenye akili na vyenye kulitetea Taifa lenye asili ya Tanganyika.
Wewe mwamba wa msoga ukiona nywele ndefu hajazishughulikia ujue kimeumana walimchachafya kweli kweli
 
Back
Top Bottom