DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Mhe. Hassan Bomboko amefanya ziara ya kuwatembelea na kuzungumza na maafisa wasafirishaji (waendesha bodaboda na Bajaj) Wilayani humo na baadae alipata nafasi ya kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Bajaj uliohudhuriwa na zaidi ya madereva bajaji 650
"Nimesikiliza Kero zao, tumezungumza na Tumekubaliana katika namna bora ya usimamizi wa Taratibu za uendeshaji vyombo hivi katika Halmashauri ya wilaya ya Hai. Nimeelekeza mamlaka ya mji mdogo kuacha mara moja kuwasumbua madereva bajaji na boda boda na badala yake wawatengee maeneo ya vituo vya kupakia abiria"- Alisema DC Bomboko.
Aidha DC Bomboko ametoa elimu kwa madereva Bajaj kuhusu umuhimu wa kutumia haki ya msingi ya kushiriki uchaguzi, na nimetoa rai kwao kuwa mabalozi watakaohamasisha wananchi kwenda kuchagua.