Wakati Jack Cliff Akiwa Jela , Mumewe Abambwa Akijiachia Kimapenzi Na Miss Tz

Wakati Jack Cliff Akiwa Jela , Mumewe Abambwa Akijiachia Kimapenzi Na Miss Tz

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Jack+cliff.jpg


SIRI imefichuka! Mume (bado talaka) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukamatwa na unga, Jacqueline Fitzpatrick Cliff, Abdulatif Fundikira ‘Tifu' anadaiwa kumnasa kimalavu Miss Tanzania 2011, Salha Israel.


mumewajack.JPG

Mume wa Jack Patrick akiwa na Salha Israel.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu, wawili hao hivi sasa wako kwenye ‘mahaba niue' na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani wazazi wa pande zote wamebariki ndoa hiyo. "Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa karibu tunaona ni jambo la heri," kilisema chanzo hicho
mumewe Jak 2 .jpg

wakati wa harusi yao.

Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena. Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye anaweza kuwa mke bora (wife material) na kuamini kuwa hawezi kumtenda kama alivyofanyiwa huko nyuma.[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Tiff ili kupata ukweli wa madai hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema kulizungumzia hilo kama yatakuwa tayari ataweka wazi. "Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini mambo yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu," alisema Tifu.
3JACK1.jpg

Mwanamitindo Jack Patrick.

Kwa upande wake Salha Israel alipopatikana kwa njia ya simu na kuelezwa kuwa Ijumaa Wikienda lina hadi picha zao za kimahaba alifunguka: "Ni kweli namfahamu, ni mtu wa karibu lakini ni sawa na kaka yangu pia. Hayo mengine labda mumuulize yeye."
 
Fifty fifty, hata jack pia alishamfanyia hivo mme wake...
 
Huyu Tifu si alikuwa rumande issue ya madawa? Kweli mwenye hela .....
 
Safi sanaaa hapa ule msemo wa malipo hapahapa duniani naona umefanya kazii aisee wamuwache ale rahaa ,hawa mastaa ushuz ni kuwapa mimba kwanzaa ndio unawaoaaa
 
Picha ya kwanza ina nyengeshana !
 
jux kwani ni nani nilisikia vibaya
 
jux kwani ni nani nilisikia vibaya

Ni mpenzi wake Jack anaishi kwaooo kazi yake kubwa kuvaa pamba mpya na kununua gari basi kulala anarudi kwa mama yake
 
What goes around

Mi sidhani kama hii habari itamstua ebu msikie kauli yake aliyowahi kuitoa mwenyewe
"Nilikosea, nikakurupuka kuolewa mapema bila kumchunguza tabia mpenzi wangu, uhusiano wetu ulidumu miezi mitano tu kisha tukafunga ndoa, lakini matokeo yake tabia hazikuendana na ndoa ikakosa uhai ndani ya muda mfupi," alisema Jack.
 
Siku hizi mkinunua nguo mpya za ndani mnajipiga picha mnazianika hadharani
 
Back
Top Bottom