Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Mume wa Jack Patrick akiwa na Salha Israel.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu, wawili hao hivi sasa wako kwenye ‘mahaba niue' na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani wazazi wa pande zote wamebariki ndoa hiyo. "Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa karibu tunaona ni jambo la heri," kilisema chanzo hicho Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena. Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye anaweza kuwa mke bora (wife material) na kuamini kuwa hawezi kumtenda kama alivyofanyiwa huko nyuma.[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Tiff ili kupata ukweli wa madai hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema kulizungumzia hilo kama yatakuwa tayari ataweka wazi. "Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini mambo yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu," alisema Tifu.
Mwanamitindo Jack Patrick.