Wakati kwako vyuma vimekaza, tayari mwezako ashanunua hii ya mwaka 2017

kwa mimi ninavyofaamu rr velar ni base version ya evoque .......so yeah uyo ni tajiri kwetu maskini kwao ...
 
Nilikua namkubali sana huyo jamaa kipindi hicho. Daaah!!! Sijui na mimi nilikua bado fala.

Jamaa aliotea hela ndefu akachanganyikiwa kabisa!

Zile show off zilikua sio za kitoto aisee!Watu walikoma na roho zao!

Sasa hivi kafulia,magari kaacha kuonesha,kaamua kwenda CCM!Amefungua baa na duka la mpesa analiita The Don's Finances,aisee hizi sanaa!

Hakujua reality ya kua dili hua haziwezi kuunganisha moja baada ya ingine kwa speed aliyokua anadhani.

Sasa hivi ndio anakomaa na ile 1Bilion ya Tigo,ambayo ina wanga wengi kwenye mgao..atavuta kadhaa hapo ila sio ya kununua Range Rover 2019 Brand New 0km!

Namuombea apige ingine ndefu atuoneshe vile vituko,nimevimiss sana!
 
Ukiona Velar plate numbered Bujibuji usishangae sana. Haya ndio maisha ninayoishi
 
*MISEMO YA WATU WENYE WIVU/HUSDA*

1.Siwezi kununua gari kwa mkopo.
2.Huyo bwana wake ni mkubwa kuliko yeye, alifuata pesa tuu!
3.Iphone kitu gani, simu simu tuu bora mawasiliano.
4.Siwezi kula chakula cha kwenye fridge.
5.Anajifanya amesoma lakini hata haolewi.
6.Siwezi kuendesha Vits, bora nitembee kwa miguu
7.Kuolewa ni stress tuu bora nikae single.
8.Microwave inaleta cancer.
9.Anaendesha V8 halafu anaishi uswazi.
10.Hiyo nguo anajifanya amenunua laki tatu wakati ni elfu thelathini tuu kariakoo.
11.Hiyo Kazi aliipata baada ya kutembea na bosi.
12.Hata kama ana degree, maisha yake sawa tuu na yetu.
13.Kwani Mercedes ina miguu mitano, gari gari tuu!
14.Siwezi kununua gari wakati sina nyumba.
15.Anaenda gym kila siku lakini ana umbo bayaaa!
16.Anajifanya kuongea kizungu wakati kwao shamba tuu.
17.Anaringaaa! Ataachwa tuu huyo.
18.Ana umbo zuri lakini hajui kuvaa.
19.Usione amenenepa hivyo anatumia ARV.
20.Hakuna jipya kwenye ndoa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji38]UKIONA HUWA UNAWAZA NA KUSEMA MANENO HAYA, NI MAWAZO YA KIMASIKINI, UJUE UNA IBILISI WA HUSDA NDANI YA MOYO WAKO. PAMBANA NA HALI YAKO NDUGU[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nahisi utakapomuona mtu kanunua Lamborghini Urus au Bentley Bentayga ndio utaenda jumba jeupe kabisa kumchongea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…