BARUA YA WAZI KWA KAKA ZANGU WAOAJI
Kaka mpendwa habari za furaha yako, habari za kila njema lako! Hongera kwa kuzaliwa mwanaume na hongera kwa mengi ambayo siwezi kuyasema hapa kwa kuandika pekee.
Leo naomba kuwaongelea yule single mother wenye THAMANI. Yawezekana mnawaogopa kwasababu fulani au mmeaminishwa vibaya na jamii zenu kuhusu single mother lakini si wote
Naomba uelewe single mother ni dada zetu, binamu zetu, mama zetu nk najua hili unalijua yawezekana hata wewe yuko mdada amekuwa single mother kwasababu yako au zake binafsi. Siwezi jua kwa nini mlitengana ila ipo sababu
KAKA ANGU MWEMA unaweza kumkimbilia asiye na mtoto na akawa AZAM TV burudani kwa wote ndani ya ndoa akakuzalia watoto wasio wa damu yako kwahiyo uswahukumu kwa mapito yao, hali zao si kila single mother ni mbaya au ana sifa za hovyo kama ujuavyo
Kaka mpendwa wapo single mother wenye THAMANI na wenye nia kweli ya kuwa wake wa mume mmoja. Wapo single mother wapambanaji na wenye uchungu na maisha, wasiojali ugumu au hali ya maisha wao wanachojua ni kuhakikisha familia inapata mahitaji. Siongelei single mom WADANGAJI
Kaka MPENDWA achana na kauli za kuwa single mother hupasha VIPORO na wazazi wenza hapana inategemea na mtazamo au huruka za mwanamke husika. Single mother mwenye THAMANI hujua THAMANI yake wala hawezi kurudia MATAPISHI. Single mother anajua kunyenyekea, kuishi kulingana na maisha yapatikanayo, anayo IMANI na pendo kubwa linalomwangika akupea hutolijutia
SWALA la kupasha viporo hata single father wapo wanaopasha viporo kwahiyo kwenye swala la kupasha viporo hata wanaume wapo wenye tabia hiyo. Kwahiyo si wanawake tu kaka wapo single mother wenye AKILI timamu wale wanaojielewa wale MALI SAFI kabisa wapo
Kaka mpendwa ukikutana na single mother anayejielewa utawashawishi hata jamaa zako wawaoe maana hawatajuta. Single mother hata akiwa na shape huwa haimpi kiburi, hata akiwa na pesa hazimpi kiburi, hata akiwa na nini hawezi kuona kuwa ni kitu cha kujivunia ila huhitaji kuiishi NDOTO yake ya kuwa mke wa mtu na mama bora wa familia atakayoipata
Kaka angu nikutoe HOFU achana na maneno ya watu kuhusu single mother kuwa hafai kuwa mke. SINGLE MOTHER na wengi wamepuvuka KIROHO na KIAKILI. Hawana pruu pruu nyingi
Kuna single mother ni wazuri kila idara kuanzia mahakamani, jikoni, kichwani (akili za maisha) hawana mambo mengi. Mapito, maumivu yao yamewafundisha na kuwajenga kuwa watu imara. Kuna single mother wanajielewa sana wanajipenda ukimpata utaenda kutoa sadaka
KAKA ANGU mwema tabia ya kupasha viporo hata asiye na mtoto anaweza kupasha viporo au kuchepuko mbona tunawoana huku mtaani sio single mother ila wanarukaruka sana na wamezaa na watu wengine wakiwa ndani ya ndoa wapo pia wanaopasha viporo na ex wao
Mbona wanawake wao hawawazii vibaya hao single father kuwa hawafai au wao wanapasha viporo mbona wanawake tunawatazama vibaya kama wao hawana akili, hawajitambui, wasaliti mkatae kwasababu yeye si chaguo lako tu kaka
HAPA SIONGELEI SINGLE MOM WADANGAJI MAKURUMBEMBE WAGALATIA ILA SINGLE MOTHER WENYE THAMANI WALE MALI SAFI