Wakati nchi nyingine zinafikiria jinsi ya kusaidia biashara zisife, Serikali ya awamu ya 5 ndio inainyongelea mbali sekta binafsi

Wakati nchi nyingine zinafikiria jinsi ya kusaidia biashara zisife, Serikali ya awamu ya 5 ndio inainyongelea mbali sekta binafsi

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Posts
5,636
Reaction score
8,777
Wandugu; ukisoma taarifa kutoka nchi mbali mbali utakutana na habari zinazoelezea hatua zinazochukuliwa na serikali za nchi zao kupunguza makali ya athari za corona.

Hebu jisomee hapa:

Sasa rudi hapa kwetu, umesikia habari yeyote ya kujaribu kusaidia sekta binafsi ili zisife? Arusha ambayo kwa kiwango kikubwa sana sana inategemea biashara ya utalii sasa hivi imesimama kiuchumi na anguko lake halipo mbali. Lakini pamoja na ukweli huo, TRA wanalazimisha kampuni zijikadirie kuwa zitapata faida mara mbili au tatu kulinganisha na mwaka jana!

Serikali ya jiwe ijiandae, mwezi May huu ujao wakiweza kukusanya angalau 20% ya VAT na 10% ya PAYE/SDL kulinganisha na walichokusanya mwezi wa February mwaka huu wafanye sherehe kujipongeza.
 
Kosa kubwa linalofanya wa-Tz kugeuzwa geuzwa kama chapati ni kukubali kuwa "wanyonge". Kila wafanyalo wanajua wanyonge hawana nguvu-kiakili,kimawazo na utashi.
 
Cha ajabu na kushangaza utasikia...

Serikali imevuka malengo yake ya ukusanyaji wa mapato...




Cc: mahondaw

Nasubiri serikali ituambie imevuka malengo kuanzia mwezi ujao. Mlimsikia jiwe juzi akidai kuwa hawezi kuiweka lockdown Dar es Salaam kwa kuwa "collection ya revenue by percentage inazidi 80%".

Asichojua ni kuwa imports zinazotakiwa kwenda (kwa mfano Mwanza na Arusha) zinachangia kwenye hiyo "percentage yake. Kwa maana hiyo mfanyabiashara aliepo Arusha akiona hauzi hataagiza tena huo mzigo ambao unatakiwa kuchangia 80% ya Dar es Salaam.

Magufuli, ulichokuwa unakitaka wakati unawashambulia matajiri ili "waishi kama shetani" sasa unakipata muda si mrefu. Sasa ndio utajua kuwa kodi inatoka kwa kina Massawe na sio kutoka TTCL au ATCL.
 
Back
Top Bottom