Nimesema hili mara nyingi tu, ifahamike Kenya tumeamua hatutajichokea kwa umaskini kama Tanzania, muhimu sana mkafahamu corona bado haipo sana Kenya kihivyo, hii hali tukiamua kuificha kama Tanzania inafichika tu, maana vifo vyenyewe tangu corona itajwe vimefika 200 kwa miezi yote hiyo, ni idadi ya vifo ambavyo vinaweza kufichika kama tungekua nchi maskini isiyowajali watu wake, pia waliopimwa na kukutwa nacho mpaka sasa ni 15,601 na wengi kati yao hawana dalili, ni ile tu walipimwa kisa waliwahi kuhusiana na walioumwa na kugunduliwa.
Kwa kifupi, nashukuru sana serikali yetu kwka jitihada zake za kuendelea kupima kupima kupima na kutolea taarifa ili tusiishi kwa kujidanganya kama wanavyofanya Watanzania, ni bora sana kupambana na hali badala ya uishi maisha ya kujichokea na kujiaminisha vitu vya hovyoo. Corona ipo, sema kwa Tanzania imewekwa kuwa aibu kwamba hata ukiumwa inabidi uifiche na kuifanya siri ya ndani, majirani wakigundua wanakunyanyapaa, maisha ya hovyoo sana kwa kweli halafu ni sera kabisa serikalini.