Wakati ni huu wa kutumia fursa hizi

peter tumaini

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
573
Reaction score
94
HAKUNA HAKI BILA WAJIBU

Napenda kuwakumbusha wana JF Hususani wadau wa BIZ kuwa nchi yetu ina fursa nyingi sana.
Ni wakati sasa wa kuzitumia.
Baada ya kuhudhuria semina nyingi, warsha, makongamano, midahalo za ujasiliamali nimegundua kuwa fursa zilizopo zimegeuka kuwa sehemu ya kutafutia posho na uandaaji wa maneno matamu na haupo katika utendaji.
Naomba wana JF wa foruma hii tutumie fursa zilizopo kwani ni nyingi haiitaji kwenda semina ili kuzifahamu.
1.KILIMO
kwa sasa unaweza kuanza kilimo cha matunda mfano Maembe ya kisasa yanatumia miaka mitatu anza na ACRE1 baada ya miaka 3 utaona matunda yake. mradi huu hauna gharama sana
Biashara ya juice kwani kuna matunda mengi yanaoza,unahitaji kutafuta eneo zuri na kuanza kwani DAR kuna joto na inanyweka sana
2.UFUGAJI
waweza anza kufuga kuku wa kienyeji wachache na baadae ukaongeza taratibu inategemea na jinsi ya kuwa manage, unaweza kutengeneza chicken butcher au egg house ukauza kwa jumla na reja reja.
3.USAMBAZAJI
kama gari waweza ingia mkataba na kampuni za uzalishaji ukaanza kusambaza bidhaa zao kwa wateja inalipa sana
4.COURRIER
unaweza kununua baiskeli au piki piki ukaanza biashara ya house delivery; kwa kununua bidhaa na kupeleka majumbani kwa watu;hii unaweza anza nayo hata hapa JF kwa kutoa namba za simu na location. pia unaweza uka modify kidogo hata kupokea mizigo kwenye magari na kupeleka.
5.REAL ESTATE.
kama huna mtaji mkubwa waweza anza na kununua kiwanja una sajili kisha unauza kwa faida na unaongeza idadi ya viwanja na baadae utaanza na ujenzi pia.
Biashara ni nyingi na fursa zimejaa tuanze kuzitumia.

MY TAKE.
Wana JF wa BUSINESS FORUM ni wakati wa kila mmoja wetu kuanzisha biashara yake ni tuwe na jadili jinsi ya kukuwa na kukabili changamoto. tuache kufikiria biashara za mitaji mikubwa ambayo hatuna tufikirie biashara za mitaji midogo ambayo tunayo kwa sasa.
Mimi nimeanza natarajia na wewe utaanza.
START TODAY SUCCESS IS WAITING FOR YOU!
 
Mkuu Hongera sana kwa kuanza, na mimi nazania imefika wakati tuwe na Monitoring and Evaluation tools ili to monite kama tunasonga mbele au ni maneno tu,

Ok nice time mkuu
 
Mkuu sio wote waliopo hapa Business Forum,bado wana idea, wengine walishaanza ku-act zamani na wana investmest kubwa/ ndogo ndogo. Hongera kwa kuchukua hatua
 
kwa kweli biashara ni muhimu sana kwakila mtu...haijalishi upo wapi.juzi nakutan ana dada mmoja naongea nae ishuz anadai hana kipaji cha biashara...nikamshangaa nikaachana nae!

nimeanzisha biashara ya MPESA tangu january..mtaji ulikua laki 7 na nimepata faida laki 4 january na laki 5 frbruary..namshukuru Mungu imeniimpress sana na najipanga nifungue vituo kama 4 hivi...laki5*4 =2million rafly
 
mkuu sio wote waliopo hapa business forum,bado wana idea, wengine walishaanza ku-act zamani na wana investmest kubwa/ ndogo ndogo. Hongera kwa kuchukua hatua

basi tuwafahamu, kwani biashara ni siri? Tatizo huku bongo tunafanya biashara kama uchawi vile, make hapa ndo eneo la kutambuana kwamba mimi nadili na hiki, mimi na dili na hiki hata kuunganisha nguvu inakuwa rahisi, mimi si mjui hata mmoja ana dill na nini zaidi ya kuowaona humu,

inatakiwa tuanze kufahamiana kibiashara hata one day tunakuwa tunakutana ana kwa ana kubadilishana mawazo,
 

Mkuu kwenye kijani hapo, hapa Tanzania kuna watu huwa wanaona mtu kuwa na biashara ni kujizalilisha, hata mimi ilishawahi kunitokea, mawazo mgando mkuu, una kuta hao ndo wahanga wa ajira, yaani yeye haoni kama kuna kitu kingine cha muhimu katika dunia hii zaidi ya ajira yake anayo lipwa mshahara mwisho wa mwezi
 

Mkuu, hili nalo neno. But hata Malila hujui kwamba amebobea kwenye Kilimo na Ufugaji? Au kanyagio kwenye utengenezaji wa vyakula vya wanyama? Kuna thread hapo juu kwenye sticky na wamejielezea vya kutosha
 
mkuu, hili nalo neno. But hata malila hujui kwamba amebobea kwenye kilimo na ufugaji? Au kanyagio kwenye utengenezaji wa vyakula vya wanyama? Kuna thread hapo juu kwenye sticky na wamejielezea vya kutosha

mkuu nawafahamu lakini kampuni zao zinaitwa nini mimi sijui au wanaendesha kienyeji mimi sijui, mimi ninacho penda ni kila mtu anaweka jina la kampuni yake na shughuli zake ili kama ni kumtafuta atafutwe, watu hufanya biashara na kampuni na si mtu
 
 
Sijawahi kuvutiwa na JM isipokuwa baada ya kusoma thread hii. Kilimo cha maembe kinalipa. Eka mbili zilipoanza kuzaa sikukosa 14m, miaka ilivyozidi kusonga naomba ibaki siri yangu
 
theoretically speaking, you are right. Which one among those u are doing?
 
theoretically speaking, you are right. Which one among those u are doing?
Hapo utakua unatafuta mengineyo, kama wewe unaona idea inafaa just take and go your way ila tukianza kiilizana wangapi wanafanya wakati jambo linaelewaka hatutafika.
Lets do what we can and never fail before you try.

Thanks
 

Mkuu umenifungua macho coz ni kwa muda nimekua nikitamani sana kufanya biashara hii ya uwakala wa Mpesa na tigopesa lakini sijapata information nzuri na jinsi gani ya kuanza. Mimi ntakupm lakini naomba kama inawezekana utusaidie uzoefu wako ktk hili coz najua wapo wengine ambao wanapenda kuanza. Kama inawezekana weka taarifa hapa.
Asante kwa kutujuza ulivyoanza
 
mkuu nawafahamu lakini kampuni zao zinaitwa nini mimi sijui au wanaendesha kienyeji mimi sijui, mimi ninacho penda ni kila mtu anaweka jina la kampuni yake na shughuli zake ili kama ni kumtafuta atafutwe, watu hufanya biashara na kampuni na si mtu

Mkuu huwa tunakutana sana, na matangazo ya mikutano huwa tunaweka hapa wazi kabisa,labdahayo matangazo huwa yanakupitia mbali. Ukiona kitu inaitwa Chai day basi ujue hiyo siku ni kunywa chai tu huku tukibadilishana mawazo na kuunganisha nguvu ktk maeneo tunayoweza.
 
Mkuu...mie ni mjoli wako kwenye ile amana ya Mkuranga... nchi iliniweka pending nikapigika mbovu.. mwezi huu narejea kuwa mashoka na majembe....
 

yanawezekana mkuu tusiwaachie wachina na sisi tukaanza kulalamika tu.
 
Sijawahi kuvutiwa na JM isipokuwa baada ya kusoma thread hii. Kilimo cha maembe kinalipa. Eka mbili zilipoanza kuzaa sikukosa 14m, miaka ilivyozidi kusonga naomba ibaki siri yangu

Hongera mkuu,ila usifanye siri wape fursa watz wapunguze umaskini.
Pamoja sana mkuu.
 
wapi maembe yanastawi mkuu?tujuzane na nitaanzaje??naomba ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…