Wakati ni kitu gani? what is time?

Wakati ni kitu gani? what is time?

ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
674
Reaction score
1,621
jamani naomba kupata mawazo yenu

kwa pamoja tukae tufikiri kitu ambacho ni cha kawaida sana lakini hatukifahamu undani wake,wakati ni kitu gani? what is time? tujaribu kutoa michango ya hisia zetu wenyewe sio kutoka ya vitabuni na science,tujaribu kusoma mpaka mwisho

ninaposema wakati sikusudii zamani leo na kesho na muda ujao(future) wala sikusudii asubuhi jiona ,saa saba mchana na saa saba usiku

masaa tunayohesabu,siku miezi na miaka ni vipimo tulivyojiwekea wenyewe ili kujua wapi tupo na muda gani,vipimo hivi vimewekwa kutokana na umbile na mazingira ya dunia yetu kama kila mwezi ni kwa muandamo wa mwezi ambao unakuwa na siku 30 hapo ndio tunapata mwezi,na siku tunaipata jua linapochomoza na kupata masaa 12 ya mwangaza wa mchana na kuzama na usiku kuingia kwa masaa 12 hio ndio tunapata siku moja,

vitu vyote hivi ni wakati (time) mchana usiku,mwezi,siku na miaka karne na vingekuwepo hata kama hatuvipimi na kuvipa majina,mwezi ungekuwa unaandama,jua linatoka na usiku unaingia milele na milele

sasa hapa ndio nataka kujua,kama tunaupima au hatuupimi, wakati ni kitu gani?

my take/ na hizi ni fikra zangu mwenyewe sio za vitabuni

1)time is timeless,wakati ni milele na hauna uhusiano wowote na mchana, usiku, mwezi na miaka,
2)time is the whole existance we are in,miaka 1000 iliyopita,sasa hivi na miaka 1000 baadae vyote vipo katika existance moja yaani vyote vinatokea katika wakati mmoja,kinachobadilika ni mazingira na watu tu lakini existance ipo vile vile,wakati haukimbii miaka ilopita wala haiendi mbele kuifata miaka ya baadae.

kwa maana sisi tunavyohesabu siku kama jana au juzi tunahisi kama ni vitu vilivyopita lakini hivi vitu vinatokea katika wakati uliopo tu(present),

tuchukulie kwa mfano
siku moja jua lisimame angani na uwe mwangaza wa mchana tu milele hapo ndio tutaweza kufahamu kuwa wakati hauende mbele,wala haupiti sisi binadamu ndio tunaupita wakati,wakati haupiti ni uliopo tu yaani present

sisi kama binadamu na vieumbe vyengine tunaingia ndani ya wakati tunapozaliwa na tunauwacha na kuupita wakati tunapokufa,na kwa hesabu zetu tulizojipangia kuuhesabu wakati tunaweza kuishi katika wakati kwa siku chache au miaka mia lakini wakati haubadiliki upo tu kama ulivyoukuta ndivyo unavyouwacha

3)time is only present, wakati ni uliopo sasa tu ,jana juzi mwaka jana miaka ijayo ni hisia na mabadiliko yetu sisi binadamu tu.
the_existence_2_by_roadioarts.jpg
0d67ee8c4bb06a34fa50158c8b8425f1.jpg
 
Muda ni mfululizo wa matukio na nafasi ktk mazingira, matukio hayo yanaweza kua kuvuma kwa upepo, kutembea kwa jua kutoka mashariki to magharibi (tumesema tuondoe dhana za vitabuni, na reality tuionayo ni jua linaizunguka dunia), mgandamizo wa hewa ambao baadae utuletea mawingu na kisha mvua, usiku na mchana.

kwaio hapa vyote ivyo vikitokea ktk mazingira yetu basi ndio tunapata muda, sababu ili tuvijue vinakuja tena baada ya nafasi gani ndio inatulazimu tupige hesabu na mwisho tunapata muda, mfano itakulazimu uhesabu jua litazama mara ngapi ili mvua zije hii ndio kileo mnaita "msimu", je jua hua linazama baada ya nafasi hipi? hapa natumia nafasi nikikuonesha kua kuna nafasi ya jua kua kaaliii, nafasi ya jua kua la kawaida na nafasi ya jua kuishiwa nguvu na kupotea kwaio hii ki leo ndo mnaitaa asubuhi au saa saba jua kali,kwaio hapa ni hesabu za nafasi ndio mkapata hiki mnachokiita leo.

na muda ulianzia misri wakat wanataka kucontrol nafasi iliyokua inakuja mara kwa mara ya mafuriko, na ukielewa hapa ndio unapata concept yangu hapa nnayoisemea ya kua muda ni nafasi na mfululizo wa matukio ktk mazingira.
 
Mkuu ZENJIBARIA swali zuri lakini mbona uko obsessed na TIME pekee? Vipi kuhusu SPACE?

What is SPACE?

Ngoja nijaribu kujibu swali lako zuri kwa kutumia mifano au analogy.

Kuna vipimo au measures au metrics zonazotumiwa kupimia vitu.

Mfano:
Mji wa DSM sio mji wa MWANZA. Hii miji imetenganisha na SPACE.

Hivyo hivyo mechi ya mpira inayoochezwa leo uwanja wa taifa sio mechi ya timu hizo hizo mbili uliochezwa uwanja wa taifa wiki iliyopita.

Sasa naomba ufuatilie kwa ukaribu sana nitakachokisema:

1. SPACE (au simply DISTANCE) is the METRIC used to measure physical separation between cities e.g., DSM and MWANZA [given TIME].

2. TIME is the METRIC used to measure temporal separation between events e.g., soccer matches. [given SPACE]

Please note.
When measuring TIME you must freeze SPACE and when measuring SPACE you must freeze TIME - au instantaneously.

Hii ndio maana ya hayo maneno kwenye mibano.

Najua pengine nimeleta maswali mengi kuliko majibu.
 
Muda or time to me ni kile ambacho ninaweza kukifanya katika siku husika or in some moment of my life.
 
Mfano Wa Uzi Kama huu alikua naona mkuu monstagla mgalanjuka missed him soo much alikua ni MTU makini na akishuka vitu Kama HIV komplicated lazima ukae

Sent from my RIDGE 4G using JamiiForums mobile app
 
I was asked this question like a year Before, But the debate went far anD we got into what is also calleD SPACE due to the relativity of these things..
But my understanDing about time is that if u think of time as Days, weeks, months, years,seasons or whatever tht falls into such measures that is not real,Briefly it is an Illusion
So time is Infinity
Do you think time came into existance before GoD?.Or GoD and time are all One?..

Sent from my GT-S6790 using JamiiForums mobile app
 
Wakati si kitu chochote, wakati unaonekana kutokea pale vitu vinapopishana mwendo. Ukisimamisha vitu vyote, utasimamisha wakati.

Wakati ni kama mawimbi yanayotokea katika maji ukirusha jiwe kwenye maji.Ukiondoa maji,huwezikuwa na mawimbi.

In fact,huhitaji hata kusimamisha vitu vyote ili kusimamisha wakati.

Ukiweza kwenda at the speed of light, wakati unasimama.

Ukiipita speed of light, wakati unarudi nyuma.

Lakini huwezi.Kitu chochote chenye mass, hata ndogo vipi,hakiwezi kufikia speed of light, kwa sababu kitakuwa na infinite mass and zero space, that is a singularity.

Ila, photons za mwanga na electromagnetic particles nyingine nyingi zinakwenda kwa speed of light.

Kwa mujibu wa hizo particles, ulimwengu hauna wakati, wakati uliopita, uliopo na ujao wote upo pamoja.

Ukisoma Einstein's Relativity haya mambo yameelezewa vizuri sana.
 
Mfano Wa Uzi Kama huu alikua naona mkuu monstagla mgalanjuka missed him soo much alikua ni MTU makini na akishuka vitu Kama HIV komplicated lazima ukae

Sent from my RIDGE 4G using JamiiForums mobile app
Kulikua na mtu anaitwa Kiranga pia... @monstagla Eiyer sijui kama bado humu
 
Wakati si kitu chochote, wakati unaonekana kutokea pale vitu vinapopishana mwendo. Ukisimamisha vitu vyote, utasimamisha wakati.
Kwa hiyo mtu aliyekufa kwake yeye hakuna muda?!
Kwamba hata kama alikufa BC ikitoke akafufuka leo, atahisi ni kama nusu saa tu tangu afe mpaka saiv...
Hii naweza kuiamini kwa kias fulani. Mfano mtu umelala usingizi ule wa pono, basi ukiamka utahisi haujalala sana!

Ukiweza kwenda at the speed of light, wakati unasimama.

Ukiipita speed of light, wakati unarudi nyuma
Kivipi mkuu?, hebu tudadavulie kidogo, mtu akivaa saa na akafanikiwa kwenda kwa spidi ya mwanga, Je saa itasimama? Au unamaanisha nini mkuu?!

Lakini huwezi.Kitu chochote chenye mass, hata ndogo vipi,hakiwezi kufikia speed of light, kwa sababu kitakuwa na infinite mass and zero space, that is a singularity.

Ila, photons za mwanga na electromagnetic particles nyingine nyingi zinakwenda kwa speed of light.
Hivi inakuwaje zile photon hazina mass, wakati ni particles?

Ila, photons za mwanga na electromagnetic particles nyingine nyingi zinakwenda kwa speed of light.

Kwa mujibu wa hizo particles, ulimwengu hauna wakati, wakati uliopita, uliopo na ujao wote upo pamoja.
Kwa hiyo unamaanisha photoni za mwanga wa jua hazitumii muda wowote kusafiri kutoka jua mpaka duniani? au hapa unamaanisha nini mkuu?!

Ukisoma Einstein's Relativity haya mambo yameelezewa vizuri sana.
Hata hivyo nakushukuru sana mkuu japo naomba uendelee kututoa tongotongo haya mambo!!
Einstein relativity theory ni ngumu sana hasa kwa mtu ambaye hana basics za physics na mathematics!! Ataishia kusema tu wazungu wanatudanganya!!
 
Kwa hiyo mtu aliyekufa kwake yeye hakuna muda?!
Kwamba hata kama alikufa BC ikitoke akafufuka leo, atahisi ni kama nusu saa tu tangu afe mpaka saiv...
Hii naweza kuiamini kwa kias fulani. Mfano mtu umelala usingizi ule wa pono, basi ukiamka utahisi haujalala sana!

Unaongelea wakati wenyewe ulivyo au mtu anavyouona wakati? Wakati wenyewe haupo.Ni mazingaombwe yanayotokea baada ya vitu vingine kusogea .

Mtua liyefariki hana viungo vya kuujua wakati wakati kafariki.

Kivipi mkuu?, hebu tudadavulie kidogo, mtu akivaa saa na akafanikiwa kwenda kwa spidi ya mwanga, Je saa itasimama? Au unamaanisha nini mkuu?!

Kwanza kabisa, chochote chenye mass hakiwezi kufikia speed ya mwanga.

Kinadharia,ukifikia speed ya mwanga (by that I mean speed ya mwanga katika vacuum) saa yako itasimama kwako.Utaweza kwenda popote na kurudimuda huo huo,muda utaacha kuwa unapita, muda utakuwa umesimama.

Hivi inakuwaje zile photon hazina mass, wakati ni particles?

Photons ni massless na hazina rest energy. Pia si particle wala waves,ni particles na waves hapo hapo, kwa mujibu wa wave particle duality. Ukitakakutafuta rest mass yake zinakuwa kama wave.
Is a photon really massless?

Wave–particle duality - Wikipedia

Kwa hiyo unamaanisha photoni za mwanga wa jua hazitumii muda wowote kusafiri kutoka jua mpaka duniani? au hapa unamaanisha nini mkuu?!

Photons za jua zinatumia takriban dakika nane na sekunde ishirini kutoka katikajua mpaka kufika duniani.

Hii inamaanisha, jua likizimika ghafla saa sita kamili mchana Dar, hatutafahamu kwamba jua limezimika mpaka saa sita na dakika nane na sekunde ishirini, kwa sababu bado tutakuwa tunapata mwanga uliokwishatoka katika jua kabla halijazimika kwa dakika nane na sekunde ishirini.

Ninaposema photon hazina muda ni kwamba,kutoka kwenye photon zenyewe, kama zingekuwa na uwezo wa kuiangalia dunia, zingeona zinaishi dunia ambayo haina muda,kila kitu kinatokea muda huo huo.

Yaani, kuanzia pale saa sita kamili zinapotoka kwenye jua mpaka pale saa sita na dakika nane na sekunde ishirini zinapofika duniani, kwa zenyewe photon hakuna tofauti ya muda,ni kama vitu vyote vinatokea wakati mmoja huo huo tu.

Kwa sababu zinakwenda kwa speed ya mwanga na ukienda kwa spidi ya mwanga, muda unasimama kako wewe, ingawa wengine wasioenda kwa speed ya mwanga muda utaendelea kuwa kawaida.

Hata hivyo nakushukuru sana mkuu japo naomba uendelee kututoa tongotongo haya mambo!!
Einstein relativity theory ni ngumu sana hasa kwa mtu ambaye hana basics za physics na mathematics!! Ataishia kusema tu wazungu wanatudanganya!!

Kuna vitabu wameelezea haya mambokwa watu ambao hawajasoma physics sana, wameelezea vizuri tu. Kamamtu anajua Kiingereza tu anaweza kusoma. Mimi niliKIfurahia sana "A Brief History of Time:FromThe Big Bang To Black Holes" cha Dr. Stephen Hawkings miaka michache baada ya kutoka.

A Brief History of Time - Wikipedia

This Quora thread explains how a photon can have no rest mass and yet they are particles

https://www.quora.com/How-can-photons-have-no-mass-and-yet-still-have-energy-given-that-E-mc-2

I am watching a very interesting Albert Einstein show from The National Geographic called "Genius". This is based on Walter Isaacson's book.

Genius
 
Kulikua na mtu anaitwa Kiranga pia... @monstagla Eiyer sijui kama bado humu
Mkuu nipo...

Wakati mwingine nabaki kuwa msomaji tu ili nijifunze kwa wengine....

Namfahamu sana Monstgala ,jamaa alikuwa vizuri sana kwenye haya mambo na sijui kapotelea wapi....

Hata Stefano Mtangoo naye yupo vizuri pia....

Wapo wengi tu na wakati mwingine ukikuta wanajadili mambo unakuwa unasoma tu ili ujifunze pia....
 
Back
Top Bottom