Wakati nyoka na mijusi dume wana uume mbili (hemipenes), ona maajabu matatu ya kipekee kwa majike!

Wakati nyoka na mijusi dume wana uume mbili (hemipenes), ona maajabu matatu ya kipekee kwa majike!

Raphael Mtui

Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
78
Reaction score
204
AJABU LA KWANZA: Haijalishi nyoka au mijusi majike watajamiiana na madume mangapi, lakini wana uwezo wa kuamua ni yai la dume yupi ndio lirutubishwe.

Yaani, watajamiiana na madume hata mia mbili, lakini wataamua mfano yai la dume wa hamsini aliyempanda, ndio litakalorutubishwa.

Kama jike anakuwa hajavutiwa na dume husika, watajamiiana tu lakini lakini jike atatumia uwezo aliopewa na Mungu wa kuzuia urutubishaji.

Sio kwamba mbegu au mayai ya dume yanakuwa hayajamwigia, au anazuia yasimwingie, hapana. Yanamwingia vizuri lakini jike ana uwezo wa kuzuia urutubishaji wa hayo mayai na hivyo hayataleta watoto.

Jike akimpenda dume, ndio hapo anaruhusu mbegu za dume huyo 'zitunge mimba'.

AJABU LA PILI: Wataalamu wanasema kuwa, majike WANA UWEZO WA KUTUNZA YAI LA DUME WALIYEMPENDA ILI NDIO LITUMIKE KUJA KURUTUBISHWA.

Yaani, kama jike amempenda dume fulani, na wakajamiiana, lakini kama jike hilo halitaki 'kubeba mimba' (kurutubishwa), wana uwezo wa kutunza hizo mbegu ndani kwa ndani hadi siku atakayoamua sasa 'mimba itungwe' au urutubishaji (fertilization) ifanyike.

Kwa hiyo, WANA UWEZO WA KUAMUA YAI HILO LIRUTUBISHWE LINI, BILA KUJALISHA NDIO WAMETOKA KUJAMIIANA AU LA.

Jike ANA UWEZO WA KUHIFADHI YAI LA DUME ALIYEMTAKA, HADI HAPO ATAKAPOAMUA SASA LIRUTUBISHWE.

Jike ana uwezo wa kutunza yai hilo HADI MIAKA MITANO NA ZAIDI!

Uwezo huu kwa kitaalamu huitwa Cryptic Female Choice.

Hadi leo, wanasayansi hawajaweza kujua hasa jinsi mfumo huu wa Cryptic Female Choice unavyofanya kazi.

Kwa hiyo, majike wana uwezo wa kujamiiana na madume wengi, lakini wana uwezo wa kuchagua ni mbegu ya dume lipi itumike kuleta watoto, na bado wana uwezo wa kuamua ni lini yai hilo lirutubishwe!

AJABU LA TATU: Majike ya nyoka na mijusi WANA UWEZO WA KUAMUA KUCHANGANYA MAYAI YA MADUME WAWILI TOFAUTI, NA HIVYO KUZAA VITOTO VYENYE SURA MCHANGANYIKO (DIFFERENT GENETIC MATERIAL)!

Wana uwezo kuzaa kiumbe chenye sura hata tatu za 'wanaume' tofauti-tofauti.

Kwa hiyo, nyoka jike akipenda na kuvutiwa na madume wawili tofauti, ana uwezo wa kutumia mbegu zao kutengeneza mtoto mmoja.

AJABU LA NNE: Nyoka dume na mijusi dume wana uume mbili!!

Ndio! Wana uume (sijui wingi wa neno uume) mbili, ambazo kwa kitaalamu huitwa Hemipenes.

Kila uume una korodani moja.

Wakati wa kujamiiana uume mmoja tu hutumika, wakati huo mwingine ukisubiri 'mwenzake' achoke, ndipo aingie kazini.

Jamaa wana 'spea' bhana!

Inasemekana wamewekewa hivyo ili madume wafanye kukutana kimwili na majike wengi, ili kuongeza uwezekano wa yai au mbegu zao kuchaguliwa kufanyiwa urutubishaji na majike wanaowapanda ili kizazi chao kiendelee kuwepo.

Hebu nijibu hili swali moja:

Hivi sehemu za siri za nyoka ziko wapi?

Ziko karibu na kule mkiani.

Nyoka wa kike yuko hivi:

Karibu na kule mkiani, kuna 'uwazi' ambao hutumika kama uke, pia hutumika kama njia ya haja ndogo na pia hutumika kupitisha haja kubwa.

Uwazi huu huitwa cloaca.

Uwazi huu hauonekani kirahisi hasa ukitegemea kuwa umefunikwa na magamba ya ngozi yake.

Hapa huenda umejiuliza tena swali la kuhusu nyoka wanajisaidiaje.

Nyoka huwa wanajisaidia mara chache, hasa haja kubwa.

Hii ni kutokana na jinsi wanavyokula maana wao humeza pasipo kutafuna na kusaga kabisa chakula chao.

Hili hupelekea mmeng'enyo kufanyika kwa taratibu sana.

Pia, nyoka hula mara chache.

Wako nyoka ambao hupata haja kubwa mara moja tu kwa mwaka!

Wengine mara moja kwa mwezi, wengine mara moja kwa wiki, wengine mara moja kwa siku.

Lakini kwa ujumla, nyoka hupata haja kubwa baada ya muda mrefu.

Tumalizie na nyoka wa kiume:

Nyoka wa kiume, wao sehemu zao za siri huwa mkiani pia.

Wao, wana cloaca ambayo kazi yake ni kujisaidia haja ndogo na haja kubwa.

Pia, wana zile uume mbili nilizosema, hemipenes.

Kwa sababu ya hiyo cloaca na hizo hemipenes, nyoka dume huwa na unene zaidi mkiani kuliko nyoka jike, na hii ndio njia rahisi ambayo hutumika kutofautisha nyoka jike na nyoka dume.

Nyoka mwembamba mkiani ni jike na yule mwenye unene mkiani ni dume.


USIACHE KUJIPATIA VITABU VYETU VIWILI AMBAVYO VIMEKUSANYA ZILE HABARI ZA KUSISIMUA AMBAZO BIBLIA HAIKUPATA FURSA YA KUZIANDIKA, INGAWA NI NZURI NA ZINA MAFUNZO MEMA YASIYOPINGANA NA BIBLIA. WOTE TUNAJUA KWAMBA BIBLIA ISINGEWEZA KUANDIKA KILA KITU HATA KAMA NI KIZURI.

Katika vitabu hivyo:
Utapata kuijua stori ya kweli ambayo wengi hawajawahi kukutana nayo ya Simoni, yule mchawi anayetajwa kwenye Biblia Matendo 8. Huyu twaweza kusema ndiye mchawi mtenda miujiza wa kutisha zaidi kuwahi kutokea na kuutikisa Ukristo kwa matendo yake!

Mtume Petro na Paulo walivyomshughulikia mbele ya umati wote wa jiji la Roma wakati akiwa anapaa, ni tukio tukufu la kupaswa kuhadithia vizazi vyetu, ingawa anguko lake lilisababisha visasi vibaya ikiwemo kuuawa kwa Mtume Petro na Paulo, na tumekueleza kwa kina jinsi walivyouawa na miujiza iliyotokea siku hiyo walipouawa.

Katika vitabu hivyo utapata pia zile nyaraka za mambo ya kale yaliyogundulika hivi karibuni nchini Uturuki, Israeli pamoja na Italia, kuhusiana na habari za Yesu zilizokuwa zimefichwa na wale waliomchukia. Moja ya nyaraka muhimu iliyopatikana ni pamoja na hii yenye mahojiano waliyowahi kufanyiwa enzi hizo Mariamu mama yake Yesu, Josefu baba yake, Martha na Maria dada zake Lazaro, na mtu aitwaye Masaliani.

Utamfahamu Yesu kiundani tangu utoto wake, maisha yake ya kawaida na tabia zake akiwa nyumbani, na alichokuwa akifanya nyumbani hasa kukitokea ugomvi. Pia utafahamu kuhusu tabia ya ajabu aliyokuwa nayo kwenye kula kwake na kuvaa kwake.

Utamwona Mariamu alivyokuwa akiudhika kwa vile Yesu alivyokuwa hahangaiki kutafuta utajiri, mke, umaarufu, wala kujijenga kisiasa, akiamini Yesu angekuwa mfalme wa siasa za kidunia.

Utamwona pia Martha dada yake Lazaro alivyokiri kutamani kuwa mke wa Yesu, lakini soma uone jinsi Yesu alivyokuwa akiishi dhidi ya wadada, hadi watoto wadogo wa kike.

Pia, utayajua maisha ya Yohana Mbatizaji ambayo Biblia haikuandika. Biblia imetuacha na maswali kadhaa kumhusu Yohana Mbatizaji: Mfano, Yohana aliweza vipi kuishi ndani ya jangwa lile hatari la Yudea, tena tangu akiwa mtoto mdogo? Alifikishwaje katikati ya milima hatari ya jangwa lile? Soma utapata majibu na pia utaona jinsi malaika walivyomlea Yohana tangu akiwa mtoto mdogo hadi alipokuwa mtu mzima na kuanza huduma rasmi.

Hatukuacha kukupa vile visa vya kusisimua vya jinsi Pontio Pilato pamoja na Kuhani Mkuu Kayafa walivyokuja kuupojea Ukristo baada ya kushiriki kumtoa Yesu asulibiwe.

Kama unasumbuliwa na yale mawazo kwamba una matatizo magumu sana kiasi kwamba Mungu hawezi kukutoa hapo, tafadhali hakikisha kwa nguvu zako zote unasoma ushuhuda wa maisha ya Bernard kwenye kitabu hiki. Mwone Bernard kutoka Ghana, mtoto wa kahaba aliyekulia majalalani, akaugua ya kufa, akamjua Mungu, hadi kualikwa White House na Rais wa Marekani, leo akiwa ni mtu aliyefanikiwa sana duniani.

Stori ya wale majitu wanefili waliotajwa kwenye Mwanzo sita hatukuiacha, utawajua kwa undani na visa vyao vya kutisha vilivyomfanya Mungu afute dunia kwa mafuriko ya enzi za Nuhu na kuanza upya uumbaji.

Mwisho, tumekupa stori yote kuhusu lile sanduku la Agano, tangu kutengenezwa kwake, miujiza yake, na mambo ya ajabu yaliyotokea siku ile lilipopotea hadi leo.

Kitabu kimoja kina kurasa 92, kingine kina kurasa 104.

Vyote vinapatikana kwa shilingi 20,000 pekee.

Kama unataka hard copy utafikishiwa ulipo. Kama unataka soft copy utazipata kupitia whatsapp.

Wasiliana nasi kwa namba 0762731869.

Hiyo ni namba ya whatsapp na kupiga pia.
 
Back
Top Bottom