Wakati Trump wa TFF "akiahidiwa" utekaji basi.. Kaka yake Polepole anusurika kutekwa Sweden

Wakati Trump wa TFF "akiahidiwa" utekaji basi.. Kaka yake Polepole anusurika kutekwa Sweden

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Baada ya siku kadhaa za kimya cha TFF, Juzi kiongozi wa kundi hilo Bwana Trump aliibuka na ujumbe wenye mashaka mengi.. Nitaweka video hapo chini

Mashaka hayo yaliyojaa maswali mengi tatanishi kama si kinzani yapo mpaka kwenye taswira yake na body language yake

Kwenye video hiyo anadai alipigiwa simu na mtu kutoka usalama wa taifa na kumuomba waongee kwa maslahi ya taifa na kumuahidi mambo kadhaa... Lakini ya msingi ni kukomesha utekaji, kuwaachia mateka wote na katiba mpya!

Mtu huyo wa Usalama alijitambulisha kwa majina yake halisi lakini kwa sababu zilizo wazi Trump hakutaka kuziweka wazi!

Nina mashaka makubwa na huyo usalama kama ni usalama halisi au ni wale wa Lumumba!
Hii ni mara yangu ya kwanza kusikia mwana usalama wa taifa anafanya reconciliation na mwanachi
Usalama hawafanyi hizo kazi bali hutafuta mtu baki kuwasemea na bila wao kutajwa popote!
Kuna kila dalili Trump kaingizwa cha kike bila kujua ama keshalainishwa!
LAKINI kama ni kweli anayosema Trump ni kweli basi tuna tatizo ama wana tatizo kubwa ndani ya mfumo
Kwamba ndani ya mfumo kuna makundi mawili
1. Kundi Linalohangaika kila kona nje na ndani ya nchi kufubaza yaliyotokea October 29
2. Kundi linaloendelea kubagaza na kuharibu kile kundi la kwanza linachojaribu kukifanya kwa nguvu nyingi na kwa gharama kubwa!

Je hii ni michezo ya kundi fulani ndani ya mfumo?

Jambo la pili ni simu ya Trump toka usalama Kwanini watumie njia nyepesi namna hiyo? Wakati wanatumwa watu kwenda ulaya 'kumteka' Kaka yake Polepole huku nyuma kuna watu wanampigia Trump simu na kumsihi asitishe harakati wayafanyia kazi madai ya TFF
Hivi kati ya Trump na Augustino Polepole ni nani hatari zaidi? Mtanijuza wajuvi!
Kuna kitu hakipo sawa hapa! Kwanini nasema hivyo ? Soma sehemu ya pili hapo chini

TikTok - Make Your Day This post is shared via TikTok Lite. Download TikTok Lite to enjoy more posts: TikTok
Sehemu ya pili
Mwezi uliopita Trump alijitokeza mitandaoni na kumlalamikia mtu mmoja maarufu kwa kuvujisha namba yake kwa wanausalama.. Trump hakuwa tayari kuweka wazi
Nini kilitokea baada ya hapo?
Usalama sasa wana mawasiliano ya Trump na kwa vyovyote yakipatikana hayo ni rahisi ku track location!
Sasa hawa wajuzi kweli badala ya kumsaka mhaini na muasi wamkamate na kumfungulia kesi ya uhaini wao wanyooshe mikono na kuomba suluhu kweli?
Haya ni maajabu!

Je Trump kawa mkate mgumu mbele ya chai?
 
Back
Top Bottom