Wakati tukiwa tunapambana na "Ukatili wa kijinsia kwa Mwanamke, Tusimsahau na mwanaume

Wakati tukiwa tunapambana na "Ukatili wa kijinsia kwa Mwanamke, Tusimsahau na mwanaume

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 49:
✍️Wakati tukiwa tunapambana na "Ukatili wa kijinsia kwa Mwanamke", tusisahau kuwa wapo baadhi ya wanaume pia wanapitia Ukatili wa Kijinsia.

✍️Kwa kuwa dhana ya ukatili ni pana sana, hivyo hatuwezi kuacha kuamini kwamba hata baadhi ya wanaume ni wahanga wa Ukatili wa kijinsia.

✍️Wapo baadhi ya wanaume ni wahanga wa ukatili wa kijinsia, na wapo wanawake wanawakatili wanaume kwa kuwatesa kimwili, kiakili na kihisia.

✍️Lakini linapokuja suala la kupinga ukatili wa kijinsia kama vile uwepo wa mikutano mbalimbali ya kupinga Ukatili wa kijinsia; vichwa vya habari vinawataja wanawake pekee. Bila shaka hata hotuba ya kupinga ukatili itazungumzia upande mmoja tu.

Soma Pia: Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu: Ukatili Dhidi ya Wanaume Umeongezeka

Right Marker
Dar es salaam
 
Tena kwa wanaume ndo umezidi sikuhizi...
Ukimwomba mshkaji pesa ili ikusaidie hata nauli ya kwenda kutafutia kibarua.
Inama!🤒
 
Ukiona Neno Jinsia Jua maana yake ni Mwanamke.

Ukisikia Haki sawa Jua Maana yake ni Haki zaidi kwa Mwanamke.

Zamani Watu walikuwa wana chezesha Miaka yao ili wapate kazi. Ila Tunakoelekea Vijana wa Kiume Itabidi Wachezeshe Jinsia zao kwenye Vyeti ili wapate Ajira.
 
Mwanaume kasahulika sasa
Kwanini asahaulike?
REPETITION LAW.
Mwanamke! Mwanamke! Mwanamke!
 
Back
Top Bottom