Wakati tunawapongeza Kenya tuwalaani pia wasaliti wetu waliokataa katiba inayopendekezwa

Wewe ni wale wapumbavu wa lumumba aliyempiga makofi Warioba ni nani na hakuna hata CCM mmoja alyempa pole!?

Usitake kuudanganya umma wa Watanzania kuhusu kuchakachuliwa kwa rasimu ya Warioba kwa 100% na hata Warioba mwenyewe na Wajumbe wengine kuja juu.

Acha kuandika uzushi humu kama wengine hatujui yaliyojiri. Na huyo fisadi na mimi wapi na wapi?

 
Watu waliopitisha hii katiba watakuwa namatatizo ya akili,asilani ni watu waajabu,watu wa akili hizi wanaweza kuleta Maendeleo au viwanda?,hatari sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wapumbavu ni wale waliokataa Tume huru ya Uchaguzi pamoja na kuhoji Ushindi wa Urais Madarakani mpaka mambo yote yawepo wakati Tume huru ingewawezesha kushika Dola na kurekebisha hayo wanayotaka Kama kweli Tume huru ndio ilikuwa Kikwazo
 
We jamaa ni muongo wa kutupa! Kisa tu upate buku 7 zako! Kikwete alidiriki kuivunja tume ya Warioba kabla haijamaliza kazi yake ya kutoa tafsiri mbali mbali za vipengele muhimu kwenye Bunge la katiba na hata magari waliyopewa na Serikali wakanyang'anywa katika mazingira ya kutatanisha na fisadi Kikwete ili wasiwe na uhuru wa kupinga hoja zake kuhusu rasimu ya Warioba au za yeyote yule katika Bunge la katiba.

Uache kuleta pumba zako humu za kuonyesha ujuha wako hadharani kuhusu rasimu ya Warioba na Tume huru ya uchaguzi. Peleka kule kwa wapumbavu wenzio mtaa wa Lumumba.

Wapumbavu ni wale waliokataa Tume huru ya Uchaguzi pamoja na kuhoji Ushindi wa Urais Madarakani mpaka mambo yote yawepo wakati Tume huru ingewawezesha kushika Dola na kurekebisha hayo wanayotaka Kama kweli Tume huru ndio ilikuwa Kikwazo
 
Mkuu katiba pendekezwa ilikuwa na mambo mengi zaidi ya hili moja la kuhusu kupinga matokeo. Yalikuwamo mambo mengi mle ambayo yalikuwa yamechakachuliwa tokea katika ya mwanzo katiba ya Warioba.

Linganisha katiba pendekezwa na katiba ya Warioba kujiridhisha kwa nini ilikuwa muhimu kuweka mpira kwapani kuonyesha kutoridhishwa na uchakachuaji wa katiba ya wananchi.
 
Huna Haja ya kutoa Matusi!

Unachopaswa kuelewa ni kuwa Wapinzani wanatamani ile Katiba waliyoisusia ndio ingepita kwa kuwa ingepunguza Mamlaka ya Rais Magufuli kuwashughulikia na pia wangekuwa na Tume huru ya Uchaguzi na ule Uchaguzi 2015 ambao 'kura zenu ziliibiwa' mngeweza kuhoji Mahakamani!

Ndio Basi Tena akili zenu zote mkaziweka kwny Mfuko na huo Mfuko akabidhiwa Ibrahim Lipumba akawatoa Nje ya Bunge
 

Kitu kikubwa kilichoondolewa ni Serikal tatu lakin Mengine Mengi yalikuwepo sema kipindi kule Watu waliwekeza zaid kwny Chuki kwa Rais Kikwete wakaona wamkomoe ili Hata Kama Katiba kupita Basi ipitishwe na Rais ajae ( hawakujua Kama atakuwa Huyu JPM)

Jk aliwaomba Basi ipigwe kura ya Maoni ili Raia ajae abaki na kazi ya kusaini tu wakakataa na kudai hata kura ya Maoni itapigwa baada ya Jk kuondoka !

1) Madaraka ya Rais yalipunguzwa
2) Tume ya Uchaguzi ingekuwa huru
3) Matokeo yote ya Uchaguzi yangewezekana kuhojiwa Mahakamani
Siasa ni mbinu kwanini wasingekubali kupata Katiba Mpya then wakishinda wataongeza Hilo la Serikal 3
Wangejua za mbinu ya Raila Odinga alie kibali kuijiunga na KANU ya Daniel Arap Moi ili apate fursa ya kuivuruga na akafanikiwa Nyie mnaendesha Sisa za Kishamba
 
Acha uongo wewe! Sasa kama unaonyesha ujuha humu unataka tukuite genius!?

Lini Wapinzani walikwambia wanaitamani katiba iliyochakachuliwa? Na yupi aliyetoa hilo tamko na wapi!?

Matatizo yako unataka kulazimisha uongo wako ili uwe ukweli, nimekwambia ujuha wako si humu nenda nao lumumba.

Huwezi kuchakachua rasimu ya Warioba kwa 100% halafu bado ukawa na uhuru wa kuhoji wizi wa chaguzi na kura.

 
[QUOTE="BAK, post: 23177464, member: 1397"

Huwezi kuchakachua rasimu ya Warioba kwa 100% halafu bado ukawa na uhuru wa kuhoji wizi wa chaguzi na kura.[/QUOTE]

Unajua maana ya 100%?
 

Nakubaliana nawe mkuu. Ilikuwa tactical mistake. Tunayo mengi ya kujifunza tokea Kenya.

Kama Odinga alijiunga KANU ili kuja kuiangusha miaka kadhaa baadaye tunapaswa kujipanga sana. Si lazima kupata yote leo. Tunaweza pata kiasi leo mengine tukaendelea kuyapigania kuliko kuyakataa yote.

Tunayo safari ndefu pale tutakapoweza kumwona mtu kama Tundu Lissu kajiunga na CCM si kwa conviction bali kwa maslahi mapana ya nchi hii ambayo yanapaswa kutambulika zaidi kuliko itikadi za vyama. Vyama vitakuja na kupita lakini nchi itaendelea kuwapo. Ni wajibu wetu sote bila kujali tuko wapi kuweka maslahi ya taifa mbele.

Hata Mh. Magufuli alipaswa weka maslahi ya taifa mbele na kuitendea haki nchi hii kwa kuipa katiba inayostahili.
 
Lipumba aliongoza Malofa kususia Katiba Pendekezwa yenye Sheria ya kuhoji ushindi wa Rais Uchaguzin na kupunguza Madaraka ya Rais
'Mtaka vyote kwa Pupa hukosa vyote'
Katiba yetu ni ile rasimu iliyoratibiwa wa jaji warioba, sio ile ya ccm.
 
Katiba yetu ni ile rasimu iliyoratibiwa wa jaji warioba, sio ile ya ccm.

Endeleeni kusubiri dodo kwny mnazi

UNIP ya Keneth Kaunda Zambia iliangushwa 1991 bila ya Tume huru wala Katiba Mpya

KANU ya Daniel Arap Moi iliangushwa 2007 bila ya Katiba Mpya wala Tume huru ya Uchaguzi

Life President Hasting Kamuzu Banda wa Malawi aliondolewa bila ya Tume huru wala Katiba Mpya

mnapaswa kupigania uwepo wa Wapinzani Wenye akili kuitoa CCM sio Katiba Mpya Kama wanavyowahadaa kwa kuwa Mataifa Mengi tu yaliwatoa watawala bila ya Katiba Mpya

Kitakachoiondoa CCM ni uwepo wa Wapinzani Wenye Vichwa vya kufikiri sio kufugia Nywele,
Kikwete anaingia Bungeni mnamzomea mnatoka Nje akistaafu anaingia Bungeni mnampokea kwa nderemo na vifijo

Mwanasiasa mnamwita Mwizi Fisadi Chama chake kinamkata mnampa Tiket ya kuwa Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…