Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ni jambo la kushangaza Sana, wakati wananchi wa Uingereza wakiandamana na kushinikiza Waziri Mkuu wao, Boris Johnson, ajiuzulu kwa ajili tu ya wafanyakazi wa Ikulu walifanya karamu wakati wa corona, hapa kwetu nchini, imedaiwa kuwa Askari Polisi amemchoma sindano ya sumu, mfanyibiashara, wa madini Musa Hamisi na kumwuua na maiti yake kuitosa Baharini na wakampora fedha yake shilingi milioni 60!
Ni tukio la kinyama mno na halifikiriki kuwa lingeweza kutekelezwa na watanzania wenzetu.
Wakati huko Uingereza wananchi wa huko wanafanya maandamano makubwa ya kumshinikiza Waziri wao mkuu ajiuzulu mara moja kutokana na kitendo hicho cha wafanyakazi wake wa Ikulu kuandaa karamu wakati wa corona.
Sisi watanzania tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida, wala hatustuki, utadhani kuwa hakuna tukio kubwa lililotokea hapa nchini!
Najiuliza hivi watanzania tumelogwa na nani, ambaye ametufanya tusijielewe na kuchukua hatua mara moja?