Wakati unaishi hostel, ni tukio gani lilitokea ambalo hutokaa ulisahau?

Applicant

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2020
Posts
1,962
Reaction score
1,751
Nakumbuka wakati tupo zetu chuo kuna hostel moja hivi tulikua tunaishi, ni Hostel ya Mtu binafsi, wanaume tulikua tunakaa Floor ya chini, juu gorofani walikua wanakaa wanawake, ilikua ni Gorofa moja tuu, mimi na jamaa zangu wawili tulikua tunatabia ya kumrekodi mtu kisirisiri bila yeye kujijua, halafu tukishamrekodi tunachomeka memorycard kweny sabufa tunaweka sauti mpaka mwisho hadi juu huko wanawake wanasikia.

Sasa kuna siku nikaenda kwa mshkaji wangu mmoja hivi alikua anafua, huyo jamaa alikua na mwanamke wake mmoja hivi, huyo demu alikua anampenda sana huyo mshkaji, sasa wakati jamaa anafua pale, mimi nikaenda na simu ikiwa tayari inahesabu sekunde nishabonyeza kitufe cha kurekodia, nikafika pale alipokaa anafua nikampa hai pale nikaanza kumpigisha story.

Nikaanza kumpigisha story za demu wake namwambia " duh! Mwanangu yule mtoto mzuri sana pale umepata! "

Mshikaji akawa anajibu tuu hajui kama anarekodiwa "aaah wapi, kidemu chenyewe chembamba kama muwa mi nakipendea tuu pesa, kwakua kinanipa pesa ndio maana nipo nacho! "
mazungumzo hayo na mengine mengi jamaa akawa anafunguka tuu anamponda manamke wake! Tulicheka sana aisee wakati huo anaendelea kufua, basi mi nikamuaga nikaondoka zangu nikaenda kwenye chumba ninachokaa na washkaji zangu.

Haahahaaha aisee sijui tulikua tunawaza nini, wale jamaa zangu wakawa wanaisikiliza wanacheka sana.

Sasa mida ya saa5 hivi usiku watu wote wamelala, pametuliaaaa! Jamaa mmoja tunae kaa nae pale ndani si akaweka memory kwenye sabufa, akaitafuta ile record halafu akaweka sauti hadi mwisho, baada kama ya dakika 5 tukasikia ukunga wanawake wanalia "jamaniii jose anakufaaa uku njoeni mumsaidie! " aisee ilikua hatari, wakati ule kumbe jamaa alikua yupo zake table pamoja na wenzake anasoma, tunafika pale tunamkuta jamaa kakakamaa anatoa mapovu mdomoni! Ilibidi tum'bebe fasta tukamuwahisha kwenye bajaji fasta tukawahi hospital.

Ilikua noma sana aisee kumbe jamaa ana kifafa na matatizo mengi tuu akipata taarifa ya mshituko anakata moto.

Baada ya kutoka hospital ilibidi sisi ndio tumuombee msamaha kwa mwanamke wake asimuache maana jamaa tulimkosea sana, mwisho wa siku mwanamke wake akaelewa wakawa poa.

Nakumbuka mwenye hostel alitaka atufukuze lakini tukaomba radhi akatusamehe.

Tokea siku hiyo nikaachana na mambo ya masihara kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ayo sio masihara, Bali mlikuwa mlikuwa na tabia ya umbea, ushangingi na ushoga, kwa maelezo yako utakuwa umesoma vyuo vyenye usajili wa veta, wasomi wa vyuo vikuu upuuzi kama huo hawezi kutokea kamwe (udom, udsm, mzumbe, st john, st joseph, nk)

Sent using komputa mpakato
 

mkuu punguza hasira msamehe[emoji23][emoji23]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo nilichosoma hakina hata usajili wa veta yaani hakijulikani kabisa, ni MADRASA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mtoa mada naomba unisamehe Sana kwa haya machache.. Ila mtoto matako Sana wewe. Nimesoma Uzi wako mpaka Nimetamani ungekua karibu ningekupa kelbu moja Matata Sana. Kama huvuti bangi Basi utakua mlevi na Kama vyote hutumii kawaulize wazazi wako Kati yao Nani ana asili ya uchawi.
Sisi tumepitia Maisha ya Chuo na tumefanya mengi Ila kwa huo upumbavu wenu Wala sio vitu vya kujivunia mpaka kuandika Jf, MODS naomba muondoe huu Uzi.. Kaka wa watu angekufa ndo mngefurahi? Huwezi jua kwann alikua anampondea yule Dada (Insecurities kwa Vijana wa kiume hasa wakiwa na wenzao kuonyesha Ni namna gani alivo shababi) Ila deep inside unakuta ndo chaguo lake.. the way ulivyo andika Ni Kama you are proud kwa kile mlichofanya, sikufichi Kama ningekua nawafahamu au yule Jamaa namjua, ningeinunua hiyo kesi alafu we na kundi lako Ningewafanyia venye mashoga wanapaswa wafanyiwe.. I hate people that hurt other people bila sababu.. Futa huu Uzi mdogo angu Mapema Sana!
 
Nilikuwa wa kwanza kufika room kwetu kwa hiyo kama siku tatu nilikaa peke yangu. Siku hiyo ilikuwa jumapili nimetoka kanisani nikawa napitia pitia niliyojifunza siku hiyo huku simu yangu nimeweka chaji. Si pale kitandani nikapitiwa usingizi nakuja kushtuka baadae tayari ni usiku kama saa mbili naangalia simu kwenye chaji haipo, nikasikitika pale wee nikasema anyway imeshatokea ngoja nishuke chini kula natafuta pochi niliyokuwa nimebeba kanisani haipo, imebebwa, bahati mbaya na wallet yenye pesa vitambulisho nayo niliweka humo, yule mwizi alikuwa mshenzi yaani aliniachia begi la nguo tu hadi Bible alienda nayo.
 
Mbona wanaume mnamshambulia mtoa mada as if huyo Jose alikuwa anafanya sawa, mimi naona walifanya kazi nzuri ya kumuumbua mnafiki....hayo ndio yalikuwa malipo ya ushenzi aliokuwa anafanya
Huwezi ukatibia ushenzi kwa ushenzi. Yani mtu anarekodi sauti na kuplay kwenye spika? Huu ni ungedere mkubwa kabisa. Angempelekea yule binti na kumpa asikilize hoja yako ingesimama ingawa nao ni umbea katika wapendanao.
Na mwisho kasema walisameheana, alipata faida gani kuwafarakanisha.
 
Kiukweli hata mimi ningembutua tabia za kishoga anakuja kujisifia hapa mpuuzi sana.

Kwahiyo wewe na mafala wenzako mkawa mnajiona wajanja? Nguruwe
 
We mkuu akili yako sijui hata ikoje mi huwa sikuelewi kabisa mkuu Kama zezeta hivi yaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…