Applicant
JF-Expert Member
- Feb 12, 2020
- 1,962
- 1,751
Nakumbuka wakati tupo zetu chuo kuna hostel moja hivi tulikua tunaishi, ni Hostel ya Mtu binafsi, wanaume tulikua tunakaa Floor ya chini, juu gorofani walikua wanakaa wanawake, ilikua ni Gorofa moja tuu, mimi na jamaa zangu wawili tulikua tunatabia ya kumrekodi mtu kisirisiri bila yeye kujijua, halafu tukishamrekodi tunachomeka memorycard kweny sabufa tunaweka sauti mpaka mwisho hadi juu huko wanawake wanasikia.
Sasa kuna siku nikaenda kwa mshkaji wangu mmoja hivi alikua anafua, huyo jamaa alikua na mwanamke wake mmoja hivi, huyo demu alikua anampenda sana huyo mshkaji, sasa wakati jamaa anafua pale, mimi nikaenda na simu ikiwa tayari inahesabu sekunde nishabonyeza kitufe cha kurekodia, nikafika pale alipokaa anafua nikampa hai pale nikaanza kumpigisha story.
Nikaanza kumpigisha story za demu wake namwambia " duh! Mwanangu yule mtoto mzuri sana pale umepata! "
Mshikaji akawa anajibu tuu hajui kama anarekodiwa "aaah wapi, kidemu chenyewe chembamba kama muwa mi nakipendea tuu pesa, kwakua kinanipa pesa ndio maana nipo nacho! "
mazungumzo hayo na mengine mengi jamaa akawa anafunguka tuu anamponda manamke wake! Tulicheka sana aisee wakati huo anaendelea kufua, basi mi nikamuaga nikaondoka zangu nikaenda kwenye chumba ninachokaa na washkaji zangu.
Haahahaaha aisee sijui tulikua tunawaza nini, wale jamaa zangu wakawa wanaisikiliza wanacheka sana.
Sasa mida ya saa5 hivi usiku watu wote wamelala, pametuliaaaa! Jamaa mmoja tunae kaa nae pale ndani si akaweka memory kwenye sabufa, akaitafuta ile record halafu akaweka sauti hadi mwisho, baada kama ya dakika 5 tukasikia ukunga wanawake wanalia "jamaniii jose anakufaaa uku njoeni mumsaidie! " aisee ilikua hatari, wakati ule kumbe jamaa alikua yupo zake table pamoja na wenzake anasoma, tunafika pale tunamkuta jamaa kakakamaa anatoa mapovu mdomoni! Ilibidi tum'bebe fasta tukamuwahisha kwenye bajaji fasta tukawahi hospital.
Ilikua noma sana aisee kumbe jamaa ana kifafa na matatizo mengi tuu akipata taarifa ya mshituko anakata moto.
Baada ya kutoka hospital ilibidi sisi ndio tumuombee msamaha kwa mwanamke wake asimuache maana jamaa tulimkosea sana, mwisho wa siku mwanamke wake akaelewa wakawa poa.
Nakumbuka mwenye hostel alitaka atufukuze lakini tukaomba radhi akatusamehe.
Tokea siku hiyo nikaachana na mambo ya masihara kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app