Raphael_Mtokambali
New Member
- Oct 30, 2021
- 0
- 12
WAKATI UNATAFUTA MAISHA USISAHAU KUISHI
Endelea kupambana lakini usisahau yakua unapaswa kuayaishi maisha yako maana siku zikiisha kuhesabika na hazito rudi nyuma
Kadiri ya mda na siku zinavyo endelea kusogea basi na wewe unapunguza muda wako wa kuwapo hapa duniani hili ni suala ambalo liko wazi sana
Acha nikusimulie kidogo kisa cha mzee mmoja alie wahi kunisimulia.....
Mwaka 2007 niliwahi kumtembelea babu yangu mmoja kwenye moja ya kijiji kilichopo mkoani Iringa na hii ilikua baada ya kutokutana na babu kwa muda mrefu sana ingawa hapakua mbali sana na kijijini kwetu.
Nilipofika huko baada ya salaamu na kukaribishwa basi kiliandaliwa chakula cha mchana nakumbuka ilikua ni (ugali na nyama pori) nilifurahi sana kupata chakula kile nikiwa na babu yangu.
Baada ya kujumuika pamoja kwenye chakula kile basi bibi alileta karanga na maziwa tukiendelea kutafuna huku tukipiga story za hapa na pale.....
Babu yangu aliniuliza swali "endapo ukipata nafasi ya kusoma na kuwa na maisha yako utapendelea kufanya nini?"
Nilimjibu kwa haraka sana...
"Mimi nataka kuja kuwa na mihela mingi sana na nataka niishi Dar, tena nijenge na nyumba ndefuuuuu(ghorofa)
Babu akaniuliza tena "unajua utaishi hapa duniani kwa muda gani?
Hapo sikumjibu nilipata kigugumizi kidogo.....
Babu akasema..
Hata mimi usinione naishi huku shambani sio kwamba sikutamani kuishi huko Dar au Marekani ila nilishindwa kwasababu nilijipanga sana na hatimae nikajikuta nimeshachoka na sikuweza tena kuikabiri hio mikiki mikiki
Wakati nafanya kazi niliweka sana pesa na baadae nilizimaliza fedha zote kwa kujitibia maradhi na kupambana na matatizo mbali mbali.
Babu akaendelea kunisimulia huku akinisititizia ya kuwa mipango sio matumizi na kupanga bila kuanza ni sawa sawa na hakuna.
Kiukweli babu alikua ananiambia vitu vikubwa sana na wakati huo nilikuwa bado ni kijana mdogo sana ila kidogo kidogo nilikua namuelewa.
Anyway tuache story za mimi na babu hakika ilikuwa ni zamani sana
Sasa acha tuyazungumze ya leo.
Ni ukweli yakuwa tunatafuta maisha sana lakini wengi bado hatuja jua tunatafuta maisha yapi na wapi, lini tutayatumia maana hakuna sayari nyingine ya kukitumia ulicho kipata duniani.
Basi hata sasa yatupasa kuwa na mipango inayoeleza ukomo wa muda maana tunaweza tukatafuta vingi sana na tukakosa muda wa kuvitumia.
Tunapaswa kupambana na kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha tunayapata maisha na wakati huo huo tukiendelea kuyaishi maisha.
Kuweza kujikimu ki makazi, malazi na chakula ni ishara tosha ya kuwa tunaishi.
Basi kama ndivyo yatupasa tuendelee kuishi wakati tunatafuta maisha hakuna maisha mapya na tofauti zaidi ya hayo unayoishi cha zaidi kitakachoongezeka au kupungua ni mtindo wa maisha.
Basi tujifunze yakuwa hata nyakati hizi sisi tunaishi maisha
Wakati unatafuta maisha usisahau kuyaishi maisha yako
Tuendelee kuishi wapendwa
MIMI NI MR 👍
Raphael Mtokambali✍️✍️