Daudi Kempu
Member
- Dec 6, 2024
- 26
- 56
Kadri unavyoendelea kujieleza kwa watu wasiokuelewa, ndivyo unavyoongeza nafasi ya wao kukuumiza ama kukifumua kidonda chako upya.
Mtu asiyekuelewa, atajitahidi kukuonyesha kila kinachokukuta ni uzembe na makosa yako mwenyewe.
Mtu asiyekuelewa, atakuhukumu, atakufanya ujishuku na pengine utaanza kujihukumu na kupuuza mchakato wako wa kujiponya.
Mtu asiyekuelewa ni wazi hakuamini, hata ukimwambia unapambana kuushona moyo wako uuvae tena, atakukatisha tamaa, atakwambia huwezi.
Mtu asiyekuelewa, atakukosea na abadani hatoona kosa lake; kuna mara ataona alikukosea kwakuwa ulitaka akukosee.
Nyamanza tu, ikibidi kuongea wakati wa mchakato, ongea na mtu mmoja anayekuelewa, atakayekwambia una nguvu na uwezo wa kupona na kusonga mbele.
Wakati mwingine, hata mgonjwa anachohitaji ni kuambiwa inuka uende na si jicho la huruma lisilo na imani.
Katika hali yoyote unayopitia mpendwa, inuka, angalia ulipo chanika, jishone, songa mbele.
Ikiwa unapumua, tambua kuwa, unayo nafasi ya kukabili na kubadili chochote. Usijikatie tamaa.