kwanza mimi nataka mtu aliyemahiri kwa lugha ya nchi yetu anitafsirie maana ya neno rape.
Pili nataka aloanzisha hii issue anifafanulie pale anaposema "wakati date rape inapokuwa sio ubakaji". Kama si ubakaji kwa nini inaitwa rape? au kuna neno rape katika kiswahili lenye maana nyengine zaidi ya ubakaji?
Tatu kwa nini tunatumia kiingilishi wakati hatukijui uzuri? kuna kosa gani kusema kiswahili?
Nne: tafsiri ya kubaka kwa ufupi tu ni kumuingilia kimwili mtu (mwanamme, mwanamke, au mtoto) kwa kutumia nguvu na bila ridhaa ya anaeingiliwa. Kwa mtoto hata kama atatoa ridhaa bado inahisabiwa ni kubaka. Maneno "kutumia nguvu bila ya ridhaa" ni muhimu hapa kwani kuna watu humu duniani wenye fantasy za maajabu inapokuja kwenye sex,, amini usiamini lakini wapo watu katika dunia hii ambao wana act kuwa wanabakwa na wapenzi wao, ajabu lakini ni kweli. kama huamini do search on internet na utaona.