Katika taifa linalodai kuwa na uhuru na amani, hali ya usalama wa raia imegeuka kuwa ndoto mbaya kwa Watanzania wengi. Matukio ya utekaji, vipigo kwa raia wasio na hatia, kufungwa kwa makanisa, na vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa yameendelea kushika kasi — huku CCM, chama tawala, kikiendelea kunyamaza kana kwamba hayaendi chini ya uongozi wake.
Tumeona watu wakitekwa mchana kweupe – wengine wakirudishwa wakiwa na majeraha, wengine hawajulikani walipo hadi leo. Familia zenye majonzi hazina hata wa kumuuliza, kwani vyombo vya dola vinaonekana ama kushirikiana au kufumbia macho. Huu si uhuru, huu ni utawala wa hofu.
Wakati makanisa yanafungwa bila sababu za msingi, wakuu wa dini wakitishwa au kutiwa mbaroni kwa maoni yao ya kiimani au kisiasa, serikali haijasema neno. Je, hii ndiyo Tanzania ya kidemokrasia tunayojivunia? Mchungaji akizungumza ukweli – ananyamazishwa. Mchora katuni akibeza serikali – anatiwa kizuizini. Raia akilalamika mtandaoni – anapotea au kupigwa.
CCM, kama chama tawala, kina wajibu wa kulinda raia wote bila kujali imani, maoni au chama chao. Lakini hadi leo, hakuna hata tamko moja la kulaani wazi haya matendo ya kihalifu. Ukimya huu si wa bahati mbaya – ni ukimya unaolinda mfumo dhalimu.
Tukiendelea kuipigia CCM kura, tunaridhia mfumo huu. Tunakubali kwamba utekaji ni sawa, kwamba raia kupigwa ni jambo la kawaida, kwamba makanisa kufungwa ni siasa tu. Lakini tusisahau: ukimya wetu wa leo ni mateso ya watoto wetu kesho.
Je, bado tuna sababu ya kuiamini CCM? Au ni wakati wa kusema imetosha?
Hili ni swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kujiuliza kabla ya kupiga kura.