Wakati wa kuhamishia Afrika iwe Makao Makuu ya dini zote duniani umefika

Hatupendwi kwa sababu hatujipendi, hebu angalia nchi kama, Vietnam, Cambodia na Laos, ni nchi ambazo USA waliwapiga mabomu mpaka kuwarudisha karne ya 5. Leo wameendela kutushinda, ni miaka 25 - 30 tuu iliyopita walipianaza kujiendeleza, leo ni matajiri kutusgihinda, na hawana rasilimali kama zetu.

Vietnam tuliwapa miche ya korosho, leo wanaongozo dunia kwa zao hili, wana viwanda vya kila aian ya kubangua, kukereketa, ku-Roast na packaging, na wanauza dunia nzima, wananunua korosho zetu na kuzi process na kuziuza USS na Europe. Sisi tunauza zikiwa kama tulivyozivuna.

Mungu katupa kila kitu, ila akili, kujiamini, kuaminiana, kuheshimiana, jitihada na ubunifu.

Angalia hata viwanda vyetu vya watanzania , utaona vinamilikiwa na wahindi au waarabu, wabantu ni nadra sana.

Tusijidanganye na hizi dini tulizoletewa hatuabudu ipaswavyo, sisi tunazidisha hadi tunakuwa watumwa wa waliotuletea na sio watumwa wa mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yabaki hukohuko kwa matumizi yao wenyewe, ikija COVID-19 wanayafunga makufuli kwa muda usiojulikana. Tangu lini nyumba ya Mungu ikatiwa kufuli, Imani dhaifu kabisa. Nyumba ya Mungu inaweza kufungwa na mtu mmoja? Huyo sio Mungu tunayemfahamu sisi wengine

Mungu wa Africa Ni zaidi ya CORONA
 
Lipo jambo unaweza fikiri ni Shari kwako kumbe ni heri kwako, na lipo jambo unaweza fikiri ni heri kwako kumbe ni Shari kwako, Katik hili tatizo LA COVID 19 Magufuli JPM alifikiri litakuwa ni Shari kwake Hatimaye limemtakatisha sana duniani kwa msimamo wake.....hatimaye mataifa karibia yote makubwa yanafuata mbinu na maarifa aliyoyatumia wakati huo dunia ilimdharau.....some time Magufuli huwa namuelewa na kumkubali sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Kenyatta kashatangaza hatua za kujiunlock, shida yetu wakoloni tunalia vilio vyao lakini wao hawalii vilio vyetu. Vilio vyetu kwao ni fursa ya neema. Kuujuwa ukweli huu lazima kubadili mitaala yetu na kurejeshwa upya darasani?

Kaka yetu kenyetta saa yake inakamata majira ya Marekani na Ulaya tu Basi.
 
Wakoloni na wamisionari walikuwa wakisali misa moja je, wakoloni hawakutupora mali zetu mchana kweupe?

Sisi waafrika Ni mzuzu kwelikweli, na CORONA ndio imekuja kutufunua macho. Israeli, Maka, Madina, USA (IN GOD WE TRUST), ITALY, IRAN, kote walifunga nyumba za ibada kwa makomeo na makufuli ya shaba mtu asikanyage humo. Walitudanganya Sana. Saudi Arabia dini ni mojawapo ya vitegauchumi vikuu, watu kwenda huko kuhiji wanazoa mabilion ya fedha kutoka hata kwa watu maskini wanaotoa fedha zao za viinua mgongo. Leo hii Saudia sio kwamba inasikitika waislam wamekosa ibada ya Hijja, bali wanasikitika kwa kukosa makusanyo ya Hijja. Italy, Israeli, Iran hivyohivyo. Wamezoa ardhi zetu kila pembe za mataifa yetu kwa kigezo Cha nyumba za ibada, wakfu, shule, nk lakini ukivaa miwani na kuangalia mapato (michango, sadaka, mavuno, zaka, biashara) yanayopatikana humo huwa yanaishia kwenda hukohuko kwenye hizo nchi. Mapato hayo hayo ndiyo hayohayo yanayorudi kwetu kuvuruga chaguzi zetu, kutuchagulia viongozi kwa manufaa yao, kununua vibaraka, kugharamia ugaidi, kuhalalisha ushoga, nk.

Jamani amkeeeeeeniii bwana Mungu wetu yuhaaai na yuko nasi hukuhuku, endelea kumuomba hutabaki Kama ulivyo leo. Piga nyungu, kula malimao tangawizi mdalasini asali alivyotubariki tutasongaaaaaa.
 


Wewe Sio bure bali unaye pepo, nende kapige nyungu ili aondoke.
 
Ambaye bila yeye tungeshamalizwa na wenzetu weupe kupitia HIV, Malaria, TB, vyakula, misaada, nk ili tufe wooote ili wao warudi na wakae hapa Africa ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Mungu na utajiri wote wa dunia.


Hilo ni neno muhimu sana kwa Waafrika kujua.
 
Afrika ndio makao makuu ya dini, magonjwa, rushwa, ujinga na umaskini. Hilo linajulikana wazi duniani kote.
 
Allah Khabar..
Ukisema "Mungu Mkubwa" badala ya Allaah Akbar Mungu atakusikia zaidi na kukuinulia uso. Mungu wa kweli hawezi kukuambia utoe sadaka ya tende wakati wewe kwenu unalima ming'oko. Hivyohivyo hawezi kulazimisha uongee Kiarabu au Kilatini au Kihebrew wakati wewe kwenu unaongea kimatumbi.

Aje Nani atupe akili mpaya?
 
Anasoma mulemule kwa walewale akitegemea kuona malaika, na mitume yenye rangi nyeusi ya kiafrika.
Kila kabila duniani lina mitume yake, manabii wake na watakatifu wake, na ndiyo maana kabila hilo lipo hadi leo. Kila kabila limepitia majanga mengi kwa miaka na karne nyingi sana. Bila shaka namna limevuka hizo taabu zote Kuna watu wenye nguvu nyingi na utukufu walio karibu Sana na Mungu wao. Ni makosa makubwa familia, ukoo na kabila kuacha kuwatambua na kuwathamini watu hao. Vinginevyo taifa hilo litaangamia na kufutika kabisa duniani.

Wako watu, familia, koo au makabila ambayo eti yameshapoteza mila na desturi zao na kuzikumbatia mila za wakoloni Kama kuabudu, lugha, kuvaa na taratibu nyingine. Watu hao wajiandae na mweleka wa kishindo siku si nyingi.
 
Bila ya kumsahau mtakatifu Meko na wana praise wake wapendwa mataga.
 
🤣🤣🤣Kwa kweli Corona ametutoa kidedea!!!! Africa💕
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…