Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wanasiasa wa upinzani wanapotoa maoni kwamba kuna vitu vya lazima na msingi zaidi kufanyika Dar es Salaam badala ya kujenga madaraja ya kupita juu ya bahari, huwa wanabezwa sana. Hatukatai hizi flyover zinasaidia sana kupunguza adha ya foleni Dar es Salaam lakini lazima tukiri kwamba flyover sio suluhisho lenye umuhimu sawa na tatizo ambalo linakuwa janga kwa Dar es Salaam, ambapo watu hupoteza maisha na mali zao.
Ni lini ulisikia wakazi wa Dar es Salaam wamepoteza maisha na mali zao kwa ajili ya foleni za Dar za asubuhi na jioni?
Labda sasa wakati wa mvua hizi zinazozaa mafuriko na kuleta majanga ya kupoteza mali za watu na hata maisha, ndipo Watanzania taelewa kwamba madaraja ya kupita juu ya bahari lili Dar es Salaam iwe kama Uaya hayana umuhimu au uharaka kiasi hicho.
Na labda jambo la kukumbuka ni kwamba gharama za daraja moja tu hili la kupita juu ya bahari hapa Dar ni kubwa sana za ukilinganisha na fedha zinazotakiwa kurekebisha miundombinu ya Dar ili watu wasipatwe na majanga wakati mvua za mafuriko zinapotokea.
Kwa hiyo wale mnaoshabikia madaraja ya kuifanya Dar iwe kama Ulaya msilalamike na haya mafuriko - kupanga ni kuchagua, na nyie ndio mnaosema wapinzani wanapinga kila kitu. Sasa ndipo mtajua wapinzani hawapingi kila kitu, bali wanapinga kila uamuzi wa kipuuzi unaofanyika.