Wakati wa mvua na mafuriko Dar es Salaam ndipo somo kwamba madaraja ya baharini sio kipaumbele cha kwanza kwa wakazi wa Dar litaeleweka!

Point zuri sana. Siku hizi serikali za mitaa wanatekeleza miradi ya maendeleo aidha kwa maagizo toka juu au kwa ku-promote CCM. Mbaya zaidi ni pale madiwani karibu wote ni wa chama tawala.

Na inavyoonekana tunakoelekea ni kubaya zaidi. Imefikia mahali ambapo miradi ya barabara za kitaifa za Tanroads inaamuliwa kwa mhemuko wa kisiasa unaofuatiwa na simu kwa Mkurugenzi wa Tanroads - "mimi ndie raisi tangaza tenda ya hii barabara hela nitakupa". Hivi raisi ana fungu la bajeti kwa aijili ya kutengeneza barabara za Tanroads zenye kugharimu mabilioni ya fedha?
 
View attachment 1599984

Suluhisho hapa ni hawa walalahoi kujenga nyumba zao kwenye flyover ya Mfugale au Ubungo!
Serikali imeacha wajibu wa kutawala, muda mwingi inautumia kwenye siasa. Taasisi zote za sarikali zimesiasishwa, siasa imebinafsisha taaluma zote. Tatizo lililoifikisha hapo Dar, na miji mingine mingi ni mipango miji mibovu, na mipango iliodunguliwa na wanasiasa kujipa maeneo yasiyo ya makazi na kuanza kuyajenga, na maji kukosa mwelekeo.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
sasa kama ni hivyo post yako yote inakosa maana.

kwahiyo kipaumbele cha watu wa dsm ni kipi??
Hilo ndio jambo ambalo mlipaswa kuwasikiliza wapinzani pale waliposema madaraja juu ya bahari ya Hindi kwenda Masaki sio kipaombele. Tatizo mliwakatisha na kuwazomea kabla hawajajieleza.
 
Hapana Mkuu, hiyo sio mentality nzuri. KUmbuka mashabiki wa kisiasa wapo CCM na hata Chadema. Kusema flyover ya Dar haimsaidii mtu wa Bukoba, kwani MV Kagera inamsaidiaje mtu wa kwetu Kishimundu?

Suala ni kwamba, kwa watu wa Dar es Salaam wenyewe, flyover ni muhimu kuwa nayo, lakini kama tungekaa na kufanya umakini wa kuamua kati ya flyover na kutengeneza system ya maji ya mvua ambayo itaondoa kabisa tatizo la mafuriko Dar, tungeamua nini kianze?
 
Mvua zinanyesha kwa msimu but foleni ipo mwaka mzima! Hasara inayosababishwa na foleni nikubwa ukilonganisha na mafuriko pia watu tunawaambia hameni mnang'ang'ania alafu mnakuja kipiga kelele hapa.
Hata foleni za mwaka mzima ni udhaifu wa serikali. Haina sera nzuri ya usafiri wa umma. Angalia mabasi ya mwendo kasi, hayana tofauti na mabasi ya kwenda mikoani kuhusu uwezo wa ubebaji. Wanaosimulia mabasi ya Icarus enzi za UDA, yaliokuwa na uwezo wa kuacha kituo wazi kilicho kuwa na abiria zaidi ya mia mbili!

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hilo ndio jambo ambalo mlipaswa kuwasikiliza wapinzani pale waliposema madaraja juu ya bahari ya Hindi kwenda Masaki sio kipaombele. Tatizo mliwakatisha na kuwazomea kabla hawajajieleza.
Uliiona foreni ya jana?

Upinzani wanasema wanataka uhuru,sio maendeleo ya vitu.

Labda ungeeleza ni kwa namna gani uhuru unaweza kumsaidia mkazi wa kigogo kuogelea kwenye maji ya mafuriko.
 
Hujui unachoongea mkuu,sijui kama unaishi dar ama wapi.

Kinachofanya maji yafurike dsm wakati jiji lililoko mlango wa bahari ungekijua, ungeelewa ni kwanini watu wameachana na hilo wazo.

Maji ya mvua dsm yanatoka juu pembezoni yanakuja dsm city cetre ili kuingia baharini, yakikuta bahari imesogea yanaingia bila shidayakikuta bahari iko kawaida yanarudishwa, hapo ndipo shida inapoanza.

Kwa aina hiyo ya mafuriko haihitaji tu uwekezaji bali kuhamisha jiji kabisa kuyapisha maji.hapo ndipo tutakuwa tumeyaweza mafuriko na kuwaridhisha wana Chadema.
 
Pumbavu! Yaani unataka kuniambia dar nzima ipo bondeni hata sehem zenye miundombinu yao vip fikiri inje ya box
Mvua zinanyesha kwa msimu but foleni ipo mwaka mzima! Hasara inayosababishwa na foleni nikubwa ukilonganisha na mafuriko pia watu tunawaambia hameni mnang'ang'ania alafu mnakuja kipiga kelele hapa.
 
Ingekuwa wewe ndio Rais hao watu wa jangwani ungewasaidiaje kwa mfano?
Maana hao walishaambiwa wahame hapo hilo eneo sio zuri kwa makazi ya watu na wakapewa viwanja mabwepande wakauza na kurudi tena hapo jangwani ili mradi tu wakae karibu na mjini
Bado hujaelewa point yangu...

Ni kwamba tunapaswa kujenga daraja jangwani.. Lianzie Faya hadi Mapipa.

Huoni mvua zikinyesha mawasiliano yanakata kati ya Magomeni na Kariakoo???

Me sijaongelea wakaazi wa Jangwani...

Kuna ofisi za DART pia pale...

Hukuwa umenielewa Mkuu...
 
Kama ni hvyo hakuna sababu ya kulaumu maana ndio plan ijayo watamalizia kwenye junction kubwa zote za jiji ikiwemo ya magomeni.
 
Nadhani kuna sehemu huko Dar palipaswa kuwa mashamba ya mpunga au sehemu ya wazi au pori la akiba, sasa kwa kuwa viongozi wetu walikosa welidi au kwa tamaa zao waka amua kuuza viwanja tena kwa walala hoi sasa madhara yake ndio hayo.
 
Unaakili za kipuuzi sana ,hujatembea umekulia buza ukasoma buza na bado utafia buza
Ulichocha kueleza ni kuwa ishu za mitaro na sewage ni kazi za halimashauri na sio serikali kuu. Halimashauri za jiji la Dar kwa miaka 10 sasa zimekuwa zikiendeshwa na chama/vyama gani?
Walitimiza wajibu?
 
Ungejua utamu wa Crispi za mihogo na mishikaki ya Kokobichi ungeunga miguu ujenzi wa flaiova hiyo. Hero wangejenga kuanza Salenda kupita kwenye mikoko kwenda Mkwajuni angalau huko kuna magari mengi muda wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…