Wakati wa uchaguzi baadhi walisema jirani zetu wako vizuri kwa kuwa na tume huru na Katiba Mpya

Kwani huko nchi jirani hakuna hiyo haki bin haki? Si tunaamini haki bin haki inapatikana? Si walifikishana hadi Supreme Court, lakini mambo yako Vilevile. Mwarobaini ni hicho kipengele kuingizwa kwenye katiba yetu. Kitawahusu wa vyama vyote. Mtu akishindwa kwenye uchaguzi mkuu akafanye shughuli zingine na asahau kuja kugombea tena. Watu kama akina Raila na Tundu hawangalisumbua tena nchi zao. Na nchi zingalitulia tuli.
Tundu Lissu anasumbua nchi!? Yule anayedai watashinda hata kwa "bao la mkono" utamwitaje!? Aisee! Wewe kweli ni mgonjwa wa akili na Mirembe ndio mahali kwako sahihi kuwepo.
 
Wakati wa uchaguzi wa jirani na ndugu zetu kuna baadhi ya wenzetu Watanzania walisifu sana kuwa wenzetu wako mbali kidemokrasia tujifunze kutoka kwao lakini kwa yanayoendelea kama mambo yenyewe ya demokrasia yako hivyo ni bora tuendelee na katiba iliyopo na tume ya uchaguzi iliyopo kuliko kuelekea huko waliko wenzetu kwa sasa.
Odinga ni mtu hatari kwenye ustawi wa jamii ya kenya. Mtu umeshindwa, umeenda mahakamani umeshindwa. Sasa ameandaa maandano ili tu kuleta taharuki ili aje atake maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu kama hapa kwetu. Eti wameruhusiwa mikutano wakati wakijua ni haki yao halafu wanashangilia. Kwa taarifa yao, CCM kuna watu wana akili sana, mpango wa kuzuia mikutano ulikuwa si wa jpm peke yake kama CDM wanavyofikiri, ni mpango wa CC ya ccm na ndiyo mana mwenyekiti hakuweza kutengua mpaka baada ya miaka miwili kupita. Nadhani pia cdm wamepewa masharti wambomoe jpm katika hotuba zao na kamwe asitajwe mama vibaya. Ni kununuliwa kule kule tu. Bado ndani ya chama kuna hofu kuu ya nguvu ya jpm.
Katika jambo ambalo upinzani ungelitumia kwa sasa kupata popular support basi ni kumtaja jpm kwa wema na kuenzi aliyoyafanya, poor them, ama hawajui siasa au, wametanguliza maslahi binafsi na hawakuwa na lengo la kutwaa uongozi wa kitaifa.
 
Hakuna tatizo mwananchi yeyote kutaka cheo na kukitafuta kwa njia za kidemokrasia, ndio sababu za uwepo wa vyama vya siasa, viongozi na watawala.
Lengo lenu mnataka tu vyeo na kuchumia matumbo yenu
 
Wakati wa uchaguzi wa jirani na ndugu zetu kuna baadhi ya wenzetu Watanzania walisifu sana kuwa wenzetu wako mbali kidemokrasia tujifunze kutoka kwao lakini kwa yanayoendelea kama mambo yenyewe ya demokrasia yako hivyo ni bora tuendelee na katiba iliyopo na tume ya uchaguzi iliyopo kuliko kuelekea huko waliko wenzetu kwa sasa.
Kenya wanapita stages kuelekea mafanikio,
Kitendo tu cha polisi kurespond ni hatua nzuri na hapa kwetu haiwezi kutokea hivyo kwa katiba tuliyonayo
 
Changamoto za demokrasia hazifutiki kwa maandishi (Katiba) peke yake; bali zinadhibitiwa kwa utekelezaji makini wa matakwa ya Katiba ikiwa ni pamoja na kuwa na mifumo thabiti ya utawala. Hapo ndipo mafanikio ya taifa la kistaarabu huwepo na kuonekana.

Marekani bado wanahangaika na matukio ya January 6, 2021 na madai ya Trump kuhusu uchaguzi wa 2020. Hatua za kikatiba na kisheria zinaendelea kuchukuliwa kupitia Bunge na mahakama. Nchi iko shwari.

Kusema tuendelee na katiba iliyopo na tume ya uchaguzi iliyopo ni kudharau Watanzania, kuwafanya mazuzu na kutaka nchi iendelee kuishi katika mazingira ya kishenzi (primitive) mithili ya banana republic. Lazima tustaarabike. Maamuzi ya wananchi lazima yaheshimiwe na haki zao kusimamiwa. Kenya bado wako mbele. Let's keep watching.

Sisi hatuna cha kujivunia. Viongozi wakubwa wa nchi wanafikia hatua ya kudai hadharani kwamba "tutashinda hata kwa bao mkono", "hata mpigie kura wengine, CCM ndiyo itakayounda serikali", halafu mambo ya ovyo yanafanyika kama ya chaguzi za 2019 na 2020. Ndio tudai tuko vizuri hivi hivi tulivyo kuliko Kenya?
 
Odinga ni mtu hatari kwenye ustawi wa jamii ya kenya. Mtu umeshindwa, umeenda mahakamani umeshindwa. Sasa ameandaa maandano ili tu kuleta taharuki ili aje atake maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu kama hapa kwetu. Eti wameruhusiwa mikutano wakati wakijua ni haki yao halafu wanashangilia. Kwa taarifa yao, CCM kuna watu wana akili sana, mpango wa kuzuia mikutano ulikuwa si wa jpm peke yake kama CDM wanavyofikiri, ni mpango wa CC ya ccm na ndiyo mana mwenyekiti hakuweza kutengua mpaka baada ya miaka miwili kupita. Nadhani pia cdm wamepewa masharti wambomoe jpm katika hotuba zao na kamwe asitajwe mama vibaya. Ni kununuliwa kule kule tu. Bado ndani ya chama kuna hofu kuu ya nguvu ya jpm.
Katika jambo ambalo upinzani ungelitumia kwa sasa kupata popular support basi ni kumtaja jpm kwa wema na kuenzi aliyoyafanya, poor them, ama hawajui siasa au, wametanguliza maslahi binafsi na hawakuwa na lengo la kutwaa uongozi wa kitaifa.
Kuandamana siyo tatizo, kulalamika siyo tatizo, kupinga matokeo ya uchaguzi siyo tatizo, alimradi kila kitu kinafanyika kwa taratibu zinazokubalika.

Kwa nchi kama yetu, ambayo wananchi wengi hawana uelewa namna mifumo ya kidemokrasia inavyofanya kazi, baadho ya watu wasio na uelewa, huona maandamano kama ni kitu cha ajabu na ni uasi.

Maandamano ni njia ya wananchi wengi kufikisha malalamiko yao kwa watawala. Na watawala wenye weledi, hiyo inakuwa ni njia ya kuthibitisha jambo linalolalamikiwa linakubalika na watu wengi kwa kiasi gani. Njia ya pili, kunapokuwa na malalamiko ya wananchi, na mtawala hana uhakika jambo hilo linaungwa na watu wengi kiasi gani, ni kura ya maoni. Lakini kura ya maoni ni aghali na ni mchakato unaochukua muda mrefu.

Japo huwa kuna vyombo vya uwakilishi, lakini siyo wakati wote vyombo hivi huwakilisha matakwa na hisia za wananchi. Mathalani. Mbunge anapotoa mawazo yake Bungemi, anaweza kusema kuwa anawakilisha matakwa ya wananchi wa jimbo analowakilisha, lakini inaweza isiwe kweli, yakawa ni mawazo yake binafsi.

Maandamano yaliyoratibiwa vizuri, ndiyo njia bora kabisa ya kuelewa hisia za wananchi, hasa yanapokuwa nonconfrotational.
 
Odinga ni mtu hatari kwenye ustawi wa jamii ya kenya. Mtu umeshindwa, umeenda mahakamani umeshindwa. Sasa ameandaa maandano ili tu kuleta taharuki ili aje atake maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu kama hapa kwetu. Eti wameruhusiwa mikutano wakati wakijua ni haki yao halafu wanashangilia. Kwa taarifa yao, CCM kuna watu wana akili sana, mpango wa kuzuia mikutano ulikuwa si wa jpm peke yake kama CDM wanavyofikiri, ni mpango wa CC ya ccm na ndiyo mana mwenyekiti hakuweza kutengua mpaka baada ya miaka miwili kupita. Nadhani pia cdm wamepewa masharti wambomoe jpm katika hotuba zao na kamwe asitajwe mama vibaya. Ni kununuliwa kule kule tu. Bado ndani ya chama kuna hofu kuu ya nguvu ya jpm.
Katika jambo ambalo upinzani ungelitumia kwa sasa kupata popular support basi ni kumtaja jpm kwa wema na kuenzi aliyoyafanya, poor them, ama hawajui siasa au, wametanguliza maslahi binafsi na hawakuwa na lengo la kutwaa uongozi wa kitaifa.
Mkuu hivi vyeo vingine vya Expert Member havina demotion ni promotion tu; kungekuwepo na demotion nadhani watu wengi wangekuwa demoted.
 
Wakati wa uchaguzi wa jirani na ndugu zetu kuna baadhi ya wenzetu Watanzania walisifu sana kuwa wenzetu wako mbali kidemokrasia tujifunze kutoka kwao lakini kwa yanayoendelea kama mambo yenyewe ya demokrasia yako hivyo ni bora tuendelee na katiba iliyopo na tume ya uchaguzi iliyopo kuliko kuelekea huko waliko wenzetu kwa sasa.
Mkuu si unawaona wana andamana kudai Wacho dai? na wasema watafanya hivyo mara mbili kwa wiki mpaka madai yao yapatiwe ufumbuzi. Mkuu wanafanya hivyo kwa mujibu wa Katiba yao.
 
Odinga ni mtu hatari kwenye ustawi wa jamii ya kenya. Mtu umeshindwa, umeenda mahakamani umeshindwa. Sasa ameandaa maandano ili tu kuleta taharuki ili aje atake maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu kama hapa kwetu. Eti wameruhusiwa mikutano wakati wakijua ni haki yao halafu wanashangilia. Kwa taarifa yao, CCM kuna watu wana akili sana, mpango wa kuzuia mikutano ulikuwa si wa jpm peke yake kama CDM wanavyofikiri, ni mpango wa CC ya ccm na ndiyo mana mwenyekiti hakuweza kutengua mpaka baada ya miaka miwili kupita. Nadhani pia cdm wamepewa masharti wambomoe jpm katika hotuba zao na kamwe asitajwe mama vibaya. Ni kununuliwa kule kule tu. Bado ndani ya chama kuna hofu kuu ya nguvu ya jpm.
Katika jambo ambalo upinzani ungelitumia kwa sasa kupata popular support basi ni kumtaja jpm kwa wema na kuenzi aliyoyafanya, poor them, ama hawajui siasa au, wametanguliza maslahi binafsi na hawakuwa na lengo la kutwaa uongozi wa kitaifa.
Kwenda zako huko, huu ujinga waambie wajinga wenzako hapo Lumumba. Eti mpango wa cc. Cc hii hii ambayo alilotaka Magu ndio lilikuwa sheria! Mwishoni utadai hata kununua wabunge na madiwani wa upinzani ulikuwa ni mpango wa cc.
 
Matusi ndiyo jadi yenu.
Utaniambia pia kwamba hujui cc ya CCM ni chombo cha maamuzi? Hiyo ndo hupanga ikisaidiwa na sekretarieti then hupelekwa kwa halmashauri kuu kwa kupitisha. Hicho ni chombo kipo kisheria na kikatiba ya ccm
 
Back
Top Bottom