Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Baadhi ya wakatoliki wanatia aibu sana katika hili sakata la anayedaiwa ni paroko kukamatwa kwa shutuma za mauji ya binti albino Asimwe.
Maoni yao hao wakatoliki naoweza kusema ni "radicals" yanatia kichefuchefu na kuonyesha jinsi gani dini bila kujali ni ya upande gani inavyoweza kutafuna na kufifisha kabisa uwezo wa binadamu kufikiri kama watu huru.
Hawa radicals ambao wamejitokeza katika sakata hili niwaweke katika makundi mawili. Kuna kundi la kwanza wanaosema wazi eti paroko hawezi kufanya mambo kama hayo, kundi la pili wamejificha kidogo wanasema hivyo kwa kificho kwa kutilia shaka na kuififisha taarifa ya polisi kwamba wamekosea kumtambua huyo mtuhumiwa.
Makundi yote mawili ni maamuma haswa wanaoongozwa na kutanguliza hisia za kidini mbele kuliko utashi wa kawaida wa binadamu anayefikiri sawa sawa.
Viongozi wa kanisa Katoliki wakataeni wafuasi wa aina hii kwani ni aibu kwa kanisa lenu, wakataeni kwa kuwaambia ukweli kwamba wapo mapadri wengi tu wa kikatoliki waliowahi kupatikana na hatia za mauaji dunia hii, waambieni kwamba hapo jirani tu Rwanda kuna Maaskofu, mapadri na masista zaidi ya 20 walifikishwa mahakamani kuhusika na mauaji ya kimbari, na hii ni historia fupi tu, historia ndefu ina mambo mengi zaidi.