Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Dalili ya mvua ni mawingu, unaweza ukapuuzia mawingu lakini manyunyu yakianza hupaswi tena kuyapuuzia maana mvua ikishashika kasi huna tena ujanja, ni kuloa tu.
Wasomi waliokosoa mkataba wa bandari kupewa DP world huenda yalikuwa ni mawingu tu, vyama vya siasa (hususani CHADEMA) na wanaharakati walipoingia na kukaa mstari wa mbele kupinga mkataba wa bandari hiyo ilikuwa ni manyunyu ya mvua, na sasa kanisa katoliki kupitia baraza la maaskofu (TEC) wamekuja na mvua kamili ya mashambulizi kuupinga huo mkataba wa bandari.
Kwa wale tunaoweza kuona mbali, muda sio mrefu walutheri (KKKT) watakuja na tamko la kuuzika huo mkataba wa bandari kabla ya mwamvuli wa waprotestant (CCT) kuja na tamko na mwishoni mwamvuli wa wapentekoste (PCT) watagongelea msumari zaidi kuuzika huu mkataba. Safari hii usishangae hadi wasabato kuingia frontline na matamko ya kuupinga huu mkataba.
Kwa kifupi sana, Kanisa hapa Tanzania limejipanga kuleta full scale ya mashambulizi dhidi ya serikali ya mama Samia kuhusu huu mkataba wa bandari na hii ni kutokana na makosa ya kiufundi ya CCM na wapiga debe wa serikali kulazimisha hili suala lionekane linapingwa kwa mlengo wa kidini ili kuwazima wakosoaji. Sasa wakosoaji wameamua kuja na mlango ule ule ambao watawala wameutengenza.
Ushauri wangu kwa mama Samia na serikali yake ni kusoma alama za nyakati tu na kuachana haraka na huu mkataba wa bandari. Huu mziki wa kanisa ni mnene mnoo, wamejipanga vizuri mnoo na wana nguvu ya kupitiliza. Wakati ni ukuta, ukishindana nao utaumia, wakati sahihi wa kuachana na mkataba wa bandari na Dp world ni sasa. Mama Samia tunakupenda sana na tunakutakia mema.