Wakatoliki Wenzangu wa Tanzania tuchangishane upesi tupate Dola 35,000 tukamkomboe Frateri aliyetekwa nchini Nigeria

Wakatoliki Wenzangu wa Tanzania tuchangishane upesi tupate Dola 35,000 tukamkomboe Frateri aliyetekwa nchini Nigeria

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa mujibu wa Matangazo ya BBC Dira ya Dunia ya Leo Jioni walionteka Mwanafunzi wa Upadri (Frateri) Melchiory Dominic (Raia) wa Tanzania na Mwenzake Raia wa Burkina Faso wanahitaji Kikombozi (Ransom ) cha Dola za Kimarekani 70,000 kwa Wote Wawili (yaani Dola 35,000) kwa kila Mmoja ili wawaachie vinginevyo Watawauwa kwa Hasira.

GENTAMYCINE nimemsikia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk. Benson Bana akiongea (Kimahojiano) na BBC Dira ya Dunia leo na kugundua kuwa hana jipya sana sana Kubwabwaja tu kulikuwa Kwingi hali iliyopelekea kuanza kuhisi kuwa huenda Serikali haioni Umuhimu wa Kumkomboa Mtanzania Mwenzetu na wameljachia Kanisa Katoliki kuhangaika na kweli kwa sasa Kanisa nalo linahangaika huku Ndugu zake huyu Frateri walioko Kwao Mkoani Kigoma wakianza Kusali na wakiamini kuwa Ndugu yao ataachiwa Huru bure bila kuwapa Fedha wajtakayo.

Kwakuwa leo ni Siku ya Tano tokea Wawili (Mafrateri hawa Raia wa Tanzania na Burkinafaso) watekwe na Watu hao wasiojulikana huku wakiwa bado hawajapewa Fedha (Kikombozi) walichokihitaji ikifika Siku ya Saba (7) wakiwa bado tu hawajapewa hata kiasi kidogo itakuwa ni vyema sasa kuanza Kujiandaa kwa lolote (liwe baya au zuri) kutoka kwa Watekaji ambao wakihitaji Fedha na wasipopewa Hasira yao kwa Waliowateka huongezeka maradufu na kuamua kufanya yao rasmi.
 
Shirika lake litatoa hela, Dr Bana kasema hizo incidents sio za kushangaza sana kwa huko na wao wanafanya follow up kwa hilo shirika ili litimize haraka demands za hao terrorists. Sdhani kama wana hitaji na michango yetu, kama umeguswa peleka wewe binafsi au shirikisha parokia yako mfanye hivyo.
 
Enzi dini haijawa biashara, hao mateka wasingekubali kukombolewa kwa rupia bali wangekubali kufa mikononi mwa watesaji ili wamshuhudie kristo.

Na si ajabu ngoma ingewageukia watesaji wakafa wao na mateka wakapona kimiujiza.

Hakuna haja ya kulipa kiasi wanachohitaji wahuni hao kwani kufanya hivi ni kuunga mkono matendo ya kigaidi.

Nafahamu wakatoliki kamili hufunga novena ili Mungu wao atende kadiri ya mapenzi yakem
 
Na hyo
Kuna wataalam wa kunegotiate malipo na mateka. Watekaji nyara wana tabia ukilipa haraka wanachotaka, basi wana demand zaidi.
Ila ni heri kulipa wasije mmaliza
Kaz ya kunigotiate na watekaji Niko vzr mno
 
Kwani huko Nigeria hakuna wakatoliki kwa taifa lenye watu zaidi ya milioni 200!
Uzi wangu nimewasema Wakatoliki wa Nigeria au wa hapa Kwetu Tanzania? Na je, umejua nina Makusudi gani kuwataja Kiupekee Wakatoliki wa hapa tu Tanzania?

Ngoja nimuombe tu Roho Mtakatifu (Holly Spirit) aniongoze vyema kwa kunipa Uvumilivu ili nisikujibu hovyo (vibaya) na ukaichukia hii ID yangu Milele.

Amina (Amen)
 
Back
Top Bottom