Wakazi apata wakati mgumu baada ya kusema kuna rappers wengi Tanzania wakali kumshinda Ngwair


Nyimbo za Ngwea hizo unazoita hits kelele halafu za kitoto, hakuna wimbo hata mmoja hapo ambao unaweza kusikiliza tena leo na ukapata ladha ile ile….. labda ndo maana ya hits? Speaking of hiphop hicho sio moja ya vigezo.

Ngoma hizo hapo nimekutajia, leo hata milele zitabaki vile vile na zinazeeka na wewe….. sijui ndo mnasema classic.!

Ngwea alipatia sana kuondoka mapema, ni 20% mwingine tu Hello
 
Ndio maana nikasema we umeweka opinions mi nimemwaga facts tu.

Ndio utofauti wetu hapo.
With all due respect, sijaona fact yeyote hapo zaidi ya opinions tu pia.
Kwani nini umetoa, numbers? Album reviews? Ratings? Awards?(hiyo tuzo aliyopata A.k.a mimi si ni ya bongo fleva!?) Come on man!

Kwa TZ kupata facts km hizo unapojudge ipi ni album bora (hasa kwenye HipHop) ni ngumu cuz hamna sources i.e charts, majarida, mitandao, tuzo, taasisi km RIAA ambazo zinadeal moja kwa moja na hayo mambo km huko kwa wenzetu! Insbidi tu tutumie opinions zetu.

Vigezo unavyoweza kuvitumia kupima ubora wa album ya hiphop* kwa kuzingatia; 1. Content/ujumbe, namna msanii ameweza kuzigusa aspect tofauti za maisha ya jamii inayomzunguka kama vile siasa, uchumi, mambo ya kijamii kama mapenzi, mahusiano, familia, tambo na majigambo nk. 2. Style/mitindo Ilotumika kusalimisha maudhui ya msanii kama vile masimulizi/storytelling, direct message, partying, nyimbo za taratibu normally za kuskiza tu huwez kuzipiga kwenye bata nk. (kwenye SYJ kuna mpaka mitindo huru/freestylin') 3. Uandishi, hapa lzm ufundi wa uandishi uonekane tena wa kihiphop zaidi. Mpangilio wa bars, vina, set ups, punchlines nk. Yaani mtu akikaa na kuskiza anasema kweli hapa huyu msanii kaandika 4. Flow, mitambao ya kihip hop inayoendana na midundo na mitindo ya kila nyimbo kwenye album. Hapa pia inahusika Sauti ya msanii na ubora wake kuyatamka maneno vizuri sio mtu penye R anaweka L, pia slang ikibidi. 5. Midundo. Midundo iwe makini hapa pia unaweza kujumuisha ufundi wa producer kwenye mixing nk.

Kwa namna yeyote ile hapo hamna kigezo chochote a.k.a mimi iko vizuri zaidi ya SYJ. Au labda kama unataka tuanze sasa kuchambua nyimbo moja moja.

Nyimbo kama Nimezama ya kwenye SYJ unaskiliza jinsi anavyosimulia Tena ni story ametengeneza mwenyewe kwenye kichwa chake, anavyoanza na anavyomaliza hutegemei unabaki tu unatikisa kichwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
1 Kwanini nampenda Nikki mbishi, nikwasababu ni MC ambaye yupo katika kila field ambayo binadamu lazima aweke mguu, ataongela siasa, mambo ya kila siku kwenye jamii, mapenzi, siasa za mziki wenyewe na ataonglea kwenye mziki wake au nje ya studio, it means mziki wake anawakilisha feelings za wengi. Kuna ngoma zake nikisikiza napata hisia kama mm ndo mwandishi. Uwezo wake wa kutengeneza hoja na kuielezea. Kiufupi napata vingi kwa Nikki hata kama hatoi nyimbo ila hata interviews zake yupo black and white, co kama wasanii wengine wanaficha vitu wanaongelea pembeni.
2. Kwanini nampenda one the incredible, nikwasababu ya uandishi wake. Kwa mfano Kuna nyimbo verse inaanza na kumshukuru Mungu, anatoka anaelezea mziki wake na vitu vingine alafu anairidia sentensi ya kwanza kiumahiri kabisa, kwahiyo inabidi ureplay umsikize freshi. Yani ni ngumu sana kutabiri neno linalofata kwenye verses za one, kasikilize KICHWA jinsi anavyounganisha sentensi Moja na nyingine
3 fid q nakubali zaidi flow zake na uandishi wake, ila sipendi swaga zake, sometimes namuona kama bishoo hivi, Kwa mfano Ngoma aliyofanya na chemical naona imejaa makuzimakuzi , ikianza natamani iishe hapohapo.

Kwa ngwea namuona kama kina daimondi tu, anakichwa Cha kutoa nyimbo za kwenda viral tu basi
 
Sina uhakika kuhusu uwepo wao au kutowepo kwao... Ila hata kama itatokea wapo basi sidhan kama wanaweza kuwa wengi kiasi kwamba ngwair asiwe wa kukumbukwa kwa ukali wake.

Ukiachana na freestyle, idea za nyimbo, na flow, Kingine kinachochangia kuwepo kwa ukali wa ngwair ni zama.

Zama zake alizitendea haki saana.

Ni kama leo maradona ni legend wa mpira... Ila ukikaa ukafatilia alichokuwa anakifanya unadhan anaweza akafikia hata uwezo wa gauchi.!?

Hafiki ila zama zinambeba.

Ngwair kwa zama zake alikuwa mkali saana.
 
Opinions?!!.



1. A.K.A mimi was the best album na ikapewa tuzo ya kili ( album of the year ) how is that an opinion?

2. Hizo nyimbo ulizotuwekea hapa wewe mwenyewe ndio umezirate ulivyotaka, niambie hiyo syj imepata award gani!?


3. Hadi leo nikienda kwenye lounges , clubs nausikia wimbo wa mikasi , wimbo umetoka miaka 17 iliyopita. umesurvive test of time, wakati hakuna hata nyimbo moja ya syj ninayoisikia popote pale.
 
Mkuu uko nayo hyo Ngoma ya umezama unitumie humu au PM?
 
Fid wa kawaida mbele ya kina one na Nikki, nimesema weka content ya nyimbo za ngwea tushindanishe na content hiyohiyo Kwa nyimbo za Nikki mbishi, tuchambue nani mkali
What a joke! [emoji28][emoji28]
 
Unataka Uzani upi, mashairi/melody/kuhit au nini?

Kazisikilize tena hits ulizoweka vs hits za Jay Moe;

1.Mikasi vs Kama unataka dem
2. Gheto langu vs Bishoo
3. She got a gwan vs Mvua na Jua
4. Napokea simu vs Maisha ya Boarding
5. Sikiliza vs Safari Njema
 
Umenikumbusha Mapacha, Ngwea na Nurueli kwenye ngoma ya NIPE JIBU.
 
Huyo Wakazi yupo hai lakini ameshakufa kimuziki,Albert amefariki kitambo lkn yupo hai kimuzidi.


Kuna mdau kasema Albert alikuwa anaimba ngoma za kusifu pombe,wanawake na Drugs.

C'Mon.


Hivi ulishawahi kusikikiza hizi.


1.Masikini Wenzangu ft Mirror
2.Sikiliza ft FA,Lady Jaydee
3.A.k.a Mimi ft T.I.D ilihusu ukimwi.


Ngwair hakuwa msanii alikuwa fullpackage.


Muulize Fid kuhusu CNN ilikuwaje alifuta vesi na kurudia upya? Tena alitangulizwa na bado alikula ComeBack moja ya nguvu. Fid yule wakati huo ndio 2Pac(in majani voice)

Alafu rudi sikiliza Pini linaitwa MSELA akiwa na Nature na KR.



Rest Easy Albert[emoji120]
 
Hivi huyu kaishi state kweli!? Mbona anaonekana mshambamshamba sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…