sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Socialite maarufu kwenye mtandao wa X na shabiki wa muziki wa hip-hop ambaye anatrend sana kwa kuchambua wanamuziki maarufu aitwae Wakazi ametishia kuwapiga block kituo cha radio cha EFM.
Ametoa mkwara huo baada ya kuoneshwa video ambayo watangazaji wa EFM walikuwa wanacheka kusikia Wakazi ajulikani anaimba vitu gani.
Socialite huyo ambaye ugeuka mbogo akiulizwa hitsong yake ni ipi? Alionekana kujaa jazba na kutokuwa mvumulivu kusikia maoni kuhusu yeye kama yeye alivyojipa jukumu la kutoa maoni kuhusu kazi za wasanii wengine.
Tunamshauri Wakazi asifikie kuwablock EFM maana akifanya hivyo itaathiri sana biashara ya hiyo radio, yeye ni mtu muhimu sana kwenye hii game anahitajika sana na media kama EFM, maisha bila Wakazi yatakuwa magumu sana.
Atoe msamaha na kusahau yapite yanazingumzika.