Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Msanii kutoka Tanzania, Wakazi amesema kwamba Diamond Platinumz ni maarufu ila sio mzuri katika uiambaji.
Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, Wakazi alisema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya umaarufu na ubora wa msanii, na hivyo kuwa maarufu haimaanishi kuwa mzuri katika sanaa ya muziki.
Aidha, Wakazi alikubali kwamba Diamond Platinumz ni miongoni mwa watu watatu maarufu nchini Tanzania ila kwa usanii bado kuna mengi anayopaswa kuyafanya. Wakazi aliweka wazi kwamba kuna watu wanaoimba na kufanya zaidi ya Diamond Platinumz.
Baadhi ya wandani wa Diamond Platnumz walionekana kughadhabishwa na kauli hiyo huku wakitema cheche kali. "Huo umaarufu kaupata kwa sababu gani? Unaweza kuwa bora na watu wasikufahamu?" Wengine waliuliza.
Kauli hii inajiri baada ya Diamond Platnumz kusema kwamba hataki kushindanishwa na wasanii wa ndani ya Tanzania, na kwamba alitaka kushindana na wanamuziki wa kimataifa.
Aidha Wakazi ameweka wazi kuwa kutokana na kusema kauli hiyo amepigiwa simu za vitisho lakini ameonyesha kubaki na msimamo wa kauli yake.
======
Picha: Webiro Wakazi Wassira
Ameandika Webiro Wakazi Wassira katika akaunti yake ya Twitter
"Kuna tofauti kati ya UMAARUFU na UBORA wa Musicians. Being popular doesn’t necessarily translates to being The Best. That being said, nakubali kuwa Diamond Platnumz is Top 3 in popularity, ila kwa Ubora (artistry) that is a reach… Kuna watu wanaupiga mwingi zaidi yake".
"Nadhani mtazamo wa ukali wa msanii ndio unategemea ntu na ntu! Kwenye ubora, nazingatia vigezo vya kiufundi, pia kufanya kwa muda mrefu bila kushuka kiwango huku unaendelea kuzingatia vigezo hivyo. Ila kuwa “mkali” au “msanii pendwa” ni sikio lako. Umaarufu unatokana na mengi".
"Wanasema Ukweli unauma… Hii imeuma sana inaonyesha, hadi napigiwa simu za vitisho"?
Pia soma: Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'